Niliyoyashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau

Ulitumia akili usingetoka kweli mpaka aondoke
 
Miaka hii unashangaa prediction ya mvua mkuu?
 
nakumbuka kuna mtu fulani mchizi alikuwa analala chini ya daraja la reli karibu pale majani ya Chai, kuingia barabara ilipokuwa zamani Tigo makao makuu.. Sasa kumbe FBI washamfuatilia yule msela zaidi ya mwezi, anaenda kariokoo anachukua mabox matupu anakuja anatandika hapo analala chini ya kidaraja fulani kilikuwa pale...Jamaa wanazoom kama mwezi hivi, wakajua hana issue.. Basi ilivyokaribia ujio wa Obama, FBI wakawambia polisi wetu, kuna mtu analala pale kwenye daraja.. Tumemchunguza hana madhara, ila kamtoeni pale ... Polisi, unavyojua walimshukia kama mwewe, hinginja hingija, tupa kule, mtama , tanganyika jeshi.... Wale FBI wanawashangaa hawa polisi, wakawambia huyo hana madhara ...

Yaani hiyo kitu ilikuwa hatari tupu..
 
Polisi wetu vichekesho
 
Makazi mwenge by then pale mitaa ya mpakani mwenge umati mkubwa wa watu mabarabarani tukiwa tuna bung'aa / shangaa shangaa na gari zilipita kwa mwendo wa speed Kali..

Inasemwa Kuna nyambizi pia ma monuary za kivita ziliweka kambi baharini pia angani kulikua na dege kubwa lisilo onekana limesimama kwa ulinzi..

😊
 
Kuhusu nyambizi inawezekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…