Niliyoyashuhudia ziara ya Rais Obama 2013 sitayasahau

Mambo mawili muhimu uliyoyasahau kuyaeelezea ni kuhusu mtandao wa mawasiliano ya simu za mkononi kukatwa na walinzi wa taifa kuwekwa kando.

Simu zilibakia kuwa ni culculator na torch mode.

Wakazi wote wa Dsm walifanywa wachumba kimawasiliano, wakawa wanatembea kwa miguu kupeana taarifa maana kitendo cha bwana mkubwa kutia mguu, simu zikawa ni makopo ya kuchezea gemu na midori, hakuna chanzo kilichoeleza simu zimekatwa na nani na zimekatiwa wapi.

Na jeshi letu la nchi kugeuzwa migambo pale jeshi la Marekani liliponza kufanya doria na wanajeshi wetu kutakiwa wajiweke kando, mbali kabisa na shughuli hizo hadi ziara ya wakubwa itakapomalizika.
 
Mimi nakumbuka ubungo yote mdudu wa malaria ayeyeitwa mbu alitoweka kwa wiki mbili. Hapo ndipo nikajifunza malaria na mradi wa watu.
 
Wenzetu wapo mbele ya muda sana🤠🤠😀😀😐😐
 
Waafrika bado sana asee uyu uyu bwege akienda Uk.russia .China shughuli zinaendelea kama kawaida..ata south Africa sizani kama ni maboya kama sisi
Jambo kubwa uelewe ni kwamba, hatuaminiki kwa sababu ya rushwa na ufisadi.

Kwa hiyo wakiingia kwenye nchi za namna hiyo, hawataki kabisa Rais wao ahudumiwe na staff ama walinzi wa kwetu, kazi zote za kiutawala na kiulinzi hufanya wao, maana nchi za mafisadi ni rahisi sana kwa staff kufika bei kununuliwa na kufanya madhara.
 
kuna wanafunzi wa azania walikuepo kwenye kumpokea obama

alikuwepo uncle wangu hapo.. aliniambia hivi

uncle alipokuwa akitusogelea obama kutupungia mkono wanafunzi wote tulihisi kama mazonge hivi,

kama wamekula madawa kiasi kwamba huwezi fanya chochote kupiga kelele wala sijui kama unataka kuleta fujo

aliniambia alizani ni yeye tu sasa kwenye kushare na wanae wakamwambia sisi pia tulijisikia hivyo hivyo

mpaka leo nashindwa kuelewa ilikuwa ni issue gani hapo
 
Hofu tu amna kitu cha ajabu ni kama uone dude kubwa mbele yako
 
Umenifanya nimecheka sana🤣🤣
 
Tukumbuke kwamba Tanzania wana historia nayo mbaya katika masuala ya ugaidi. Ubalozi wao ulishawahi kukumbwa na tukio.

Kituko zaidi walikiona watumishi wa airport kule, kwani wao waligeuzwa kuwa kama abiria tu, shughuli zote walihodhi USA, hadi uwanja wa jeshi ulikuwa chini yao. Chochote walichokiona ni tishio kiliondolewa hata kama kilikuwa kwenye eneo la jeshi, Ile miti ilipunguzwa matawi yaani wakazi wa eneo lile hakuna rangi walikosa kuiona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…