Best Daddy
JF-Expert Member
- Apr 2, 2019
- 950
- 1,672
Happy Holiday! Natumaini mnaendelea vizuri wana-Jamiiforums. Msukumo wa kuandika andiko hili umetokana kuangalia mechi tatu, pale ambapo Yanga amekutana na Mashujaa, Tanzania Prisons na hii mechi yake ya mwisho dhidi ya Dodoma Jiji.
Nimekua shabiki kindaki ndaki wa mpira wa Tanzania, nimeudhuria mechi nyingi sana hasa za Yanga katika msimu uliopita. Nimefurahi sana kwa wakati ule, lakini wakati naandika andiko hili nikiri kusema sitakuja kutazama tena mechi za Yanga isipokuwa zile mechi za kimataifa, au watakapo kutana Yanga vs Simba/Azam.
Kupitia mechi hizo hapo juu, sijui niseme ni uwezo mkubwa wa Yanga, au uwezo mdogo wa timu pinzani au kuna sababu nje ya uwanja au vyote kwa pamoja . Ila hizo mechi zilikua kama futuhi, ni maigizo yaani ni kichekesho. Kuna wakati unajiuliza inakuwaje hizi timu zinashiriki ligi kuu. Wachezaji wa timu pinzani wanashindana kufanya makosa, wachezaji wanashindana kutoa zawadi, labda kwa kuwa ni msimu wa Christmas.
Sizungumzi haya sababu za kuwa Yanga hapaswi kushinda, Hapana. Ila nazungumzia ushindani umepotea kabisa. Tofauti na miaka ya nyuma. Hizi mechi zote tajwa Yanga ameshinda sio sababu ya ubora wake, ila sababu ya udhaifu wa mpinzani. Ni ushindi mwepesi sana.
Mechi zote Yanga angekua makini hata kidogo tu, alikuwa na uwezo wa kupata hata magoli zaidi ya 10 maana ilikuwa ni washindwe wao tu. Hapo hapo ukitazama timu hizo tajwa zinapokutana na vilabu vya Simba na Azam basi ushindani unakua ni mkubwa sana.
Kuokoa soka letu, tulitazame hili kwa undani, tupate tatuzi za kinadharia na kivitendo ndani na nje ya uwanja. Either kuna baadhi ya vilabu vina influence katika timu hizi ndogo au gap kati ya Yanga na hivi vilabu vingine ni kubwa sana kusema kwamba inawathiri wachezaji kisaikolojia hata kabla hawajakutana nao.
Natambua kuwa tuna tamani vilabu vyetu vishinde kwa namna yeyote, lakini katika hili haihitaji uwe shabiki wa Yanga au Simba au hata mpira kuliona hili. Athari yake ni kuwa hii ligi itaenda kuwa dhaifu au kwa lugha ya kisoka kujulikana kama Farmers League.
Mdau wa soka mtazamo wako ni upi?