Best Daddy
JF-Expert Member
- Apr 2, 2019
- 950
- 1,672
- Thread starter
- #41
Sawa.Kila kolo atatoka mafichoni
Tena waombe saana washinde mechi yao ya mwisho dhidi ya SBS
Bila ya hivyo hali itakua mbaya saaana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa.Kila kolo atatoka mafichoni
Tena waombe saana washinde mechi yao ya mwisho dhidi ya SBS
Bila ya hivyo hali itakua mbaya saaana
Unawaonea tu hao Makolo, sijazungumza kwa niaba yao.Kimsingi kinachowauma makolo ni recovery ya haraka ya yanga na namna yanga wanavyopanda kwa speed pale juu.
Mpira wa Yanga ni mtam sana mpenda soka yoyote angependa kuiangalia Yanga hii ya GUSA ACHIA twende kwao
Na niwaambie makolo wenda mkafungwa goli nyingi sana na yanga derby ijayo
Umesoma uzi mkuu? au sijaeleweka.Mbumbumbu kazi mnayo, niliwai kusema mda si mrefu mtatoka kwenye mashimo yenu Mmoja baada ya mwingine,, wakati yanga anafungwa mechi tatu mfululizo ulikuwa unampenda kuziangalia hizo mechi lakini yanga karudi kwenye makali yake ghafla unatoa milio kwamba utaki kuwaangalia Tena🤔🤔🤔
Kwaiyo yanga wangeendelea kufungwa ungeendelea kuangalia mechi zao na ingekuwa burudani kwako?
Yanga Bingwa.Umezunguka kweli msee😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄.kataa hofu,hofu inaua🤣🤣🤣🤣 YANGA BINGWA😄
Kwamba mechi dhidi ya Mashujaa ilikuwa nyepesi!!!?? Au ulihadithiwa? Ile mechi ingewezekana kuisha 3-3 kama si ubora wa kikosi cha Yanga. Tupunguze mahaba, tuangalie mpira kwa uhalisia wake.Happy Holiday! Natumaini mnaendelea vizuri wana-Jamiiforums. Msukumo wa kuandika andiko hili umetokana kuangalia mechi tatu, pale ambapo Yanga amekutana na Mashujaa, Tanzania Prisons na hii mechi yake ya mwisho dhidi ya Dodoma Jiji.
Nimekua shabiki kindaki ndaki wa mpira wa Tanzania, nimeudhuria mechi nyingi sana hasa za Yanga katika msimu uliopita. Nimefurahi sana kwa wakati ule, lakini wakati naandika andiko hili nikiri kusema sitakuja kutazama tena mechi za Yanga isipokuwa zile mechi za kimataifa, au watakapo kutana Yanga vs Simba/Azam.
Kupitia mechi hizo hapo juu, sijui niseme ni uwezo mkubwa wa Yanga, au uwezo mdogo wa timu pinzani au kuna sababu nje ya uwanja au vyote kwa pamoja . Ila hizo mechi zilikua kama futuhi, ni maigizo yaani ni kichekesho. Kuna wakati unajiuliza inakuwaje hizi timu zinashiriki ligi kuu. Wachezaji wa timu pinzani wanashindana kufanya makosa, wachezaji wanashindana kutoa zawadi, labda kwa kuwa ni msimu wa Christmas.
Sizungumzi haya sababu za kuwa Yanga hapaswi kushinda, Hapana. Ila nazungumzia ushindani umepotea kabisa. Tofauti na miaka ya nyuma. Hizi mechi zote tajwa Yanga ameshinda sio sababu ya ubora wake, ila sababu ya udhaifu wa mpinzani. Ni ushindi mwepesi sana.
Mechi zote Yanga angekua makini hata kidogo tu, alikuwa na uwezo wa kupata hata magoli zaidi ya 10 maana ilikuwa ni washindwe wao tu. Hapo hapo ukitazama timu hizo tajwa zinapokutana na vilabu vya Simba na Azam basi ushindani unakua ni mkubwa sana.
Kuokoa soka letu, tulitazame hili kwa undani, tupate tatuzi za kinadharia na kivitendo ndani na nje ya uwanja. Either kuna baadhi ya vilabu vina influence katika timu hizi ndogo au gap kati ya Yanga na hivi vilabu vingine ni kubwa sana kusema kwamba inawathiri wachezaji kisaikolojia hata kabla hawajakutana nao.
Natambua kuwa tuna tamani vilabu vyetu vishinde kwa namna yeyote, lakini katika hili haihitaji uwe shabiki wa Yanga au Simba au hata mpira kuliona hili. Athari yake ni kuwa hii ligi itaenda kuwa dhaifu au kwa lugha ya kisoka kujulikana kama Farmers League.
Mdau wa soka mtazamo wako ni upi?
Kk umemaliza kilakitu sitoweka comment Zaid ntaharibu🤣🤣yaani upate mashaka na mechi za yanga uache kupata mashaka na mechi za simba
sema yanga akianza fanya vizuri maneno ya namna hii yanakuwa mengi mno
ukatizame mechi za yanga na simba, huyu huyu kachapwa mara 4 mfululizo
mechi ya yanga na azam huyu huyu alipigwa 4 kama dodoma jiji
we kuwa mkweli presha imekupanda baada ya yanga kuanza kushinda usijifiche kwenye kichaka cha mechi za yanga zikoje
Penati za so called ni mapungufu ya referee, ambayo hutokea sababu uwezo mdogo, makusudi ya referee na sio timu pinzania. Ila huu uzi umejikita katika timu pinzani na sio wasimamizi wa mchezo ambayo in issue nyingine kabisa.Nimesoma kote ila ulivyoleta story kuwa hizo timu nyingne sijui wakikutana na Simba basi wanawakazi, kiukweli sijaendelea kusoma tena.
Ww mechi za Simba huwa unaangalia kweli? Magoli ya penalt za mchongo alafu unasema wanawakazia!!
Nilikua KMC Complex tulitoka na kila mtu alikubalia ile magoli yote yalikuwa sababu ya uzembe wa Khomein, ila mechi ilikuwa nyepesi sana kwa Yanga. Truth must be told.Kwamba mechi dhidi ya Mashujaa ilikuwa nyepesi!!!?? Au ulihadithiwa? Ile mechi ingewezekana kuisha 3-3 kutokana na ushindani waliotoa mashujaa
timu gani pinzani haiiogopi yangaPenati za so called ni mapungufu ya referee, ambayo hutokea sababu uwezo mdogo, makusudi ya referee na sio timu pinzania. Ila huu uzi umejikita katika timu pinzani na sio wasimamizi wa mchezo ambayo in issue nyingine kabisa.
Yes niliwahi kusikia hili. Hivyo tunakubaliana kuna wakati sababu nje ya uwanja kama zile za kiongozi au kiushabiki hupelekea kuathiri ushindani ya ndani ya uwanja.timu gani pinzani haiiogopi yanga
rejea kauli za dube na kiemba wakiwa azam una ambiwa mechi na yanga viongozi wana weka mipango madhubuti ya kushinda na wakipoteza wanaumia sana tofaut na mechi za simba
wapinzani wa yanga wote wanatamani kukaza sana shida wanazidiwa sana
Hizi ndo Akili za Washabiki wa Mpila wa Tanzania Taja Mechi Tatu za Simba za hivi Karibuni Na mechi Tatu za Yanga hizi Zilizopita Alafu linganisha Kiwango cha Ushindani Ndani ya kiwanja Kuanzia kimbinu na kiufundi Ndo utajigundua kuwa Yanga imekufanya uwe Zwazwa Kichwani.yaani upate mashaka na mechi za yanga uache kupata mashaka na mechi za simba
sema yanga akianza fanya vizuri maneno ya namna hii yanakuwa mengi mno
ukatizame mechi za yanga na simba, huyu huyu kachapwa mara 4 mfululizo
mechi ya yanga na azam huyu huyu alipigwa 4 kama dodoma jiji
we kuwa mkweli presha imekupanda baada ya yanga kuanza kushinda usijifiche kwenye kichaka cha mechi za yanga zikoje
Uzuri wa Maigizo huwa na Muda wa Kuanza na muda wa kwisha.sasa mpinzani akiwa dhaifu si ndio unatumia udhaifu huo huo kushinda game, mpinzani akifanya makosa unatumia makosa hayo hayo kushinda game, yaani ukiona mpinzani amefungwa ujue alifanya makosa na mwenzake akatumia hiyo nafasi, hata man yu amefungwa kwa sababu alifanya makosa, ila ukiangalia ubora wa kikosi cha mbwa mwitu na man yuu huwez kudhani man yuu atafungwa
We hujui chochote kuhusu Yanga mmeenda mpilani na vibukta kisa Ally kamwe mmepaka hina nywele kisa Kamwe mmevaa Misuli kisa Kamwe Mmejipaka mafuta wenyewe kisa Ally kamwe mmeenda na Gari la maji taka Nyumbani kwa Lloyd Nchunga Eti Wavumilivu au UlikuwA Bado Mbwinde ujaja Mjini?Nimeamini kweli uelewa Tz umeshuka sana. Yaani hawa walopokaji wa timu akilopoka jambo hata liwe la kutunga tu kwa ufikiri wake tu lakini atapata kiwango kikubwa cha wafuasi wake kwa lugha zake tu. Hasa mashabiki wa mikia wanaamini sana kwa wasemaji wao.
Nakumbuka hata kipindi cha manara yuko simba ilikuwa wakisikia tu usemi fulani kutoka kwa manara kesho yake mitaani utawakuta mashabiki wa Simba wanapita na ile lugha yake.
Hawawezi kujifikiria na kuchanganua jinsi waonavyo wao. Wanaamini sana kutoka kinywani kwa walopokaji wao
Huyu kajitahidi anajaribu kuona kama ni ya kwake,lakini yote kwa yote anafuata mle mle kwa mlopokaji wao.
Hapo ujue bado zitakuja tred nyingi za mlengo ule ule wa lugha ya ahemed.
Kwenye mihemko ya kufuata usemi wa msemaji wa timu nawasifu sana mashabiki wa YANGA,hawana hiyo sana. Na ni wavumilivu sana mashabiki wa YANGA
Match Fixing wachezaji Hawasimami tu kama Milingoti au minara ya Simu Hivi kweli kichwani Wenyewe Wapo?Nimetazama mechi zote
Ni matokeo ya kimchezo na Yanga anapata mechi ngumu na kufungwa.
Kama ingekuwa ivo kwanini Yanga anafungwa
Wapinzani wanapata on target
Yanga anataka card
Yanga wachezaji wanaumia
Si angekuwa anafika na kushinda
Kiwango chao halisi ni Kule wanakoshika Nafasi ya Kwanza kutoka chiniMbona unang'ang'ania kuhofia tu wakati nimetoa sababu za kufungwa zaidi ya hiyo? Mimi na nadhani na mleta mada hatujatoa jibu la moja kwa moja la kwa nini hizi timu zinafungwa na Yanga katika mazingira yanayoonekana ni ya kizembe.
Au labda sijaelewa hoja yako ni ipi hasa.
Yanga alivompiga 5imba mara nne mfululizoMatch Fixing wachezaji Hawasimami tu kama Milingoti au minara ya Simu Hivi kweli kichwani Wenyewe Wapo?
Afadhali umemjibu. Anadhani match fixing ikiwepo, wachezaji wanakuja wanachuchumaa uwanjani halafu timu nyingine inajifungia tu magoli.Match Fixing wachezaji Hawasimami tu kama Milingoti au minara ya Simu Hivi kweli kichwani Wenyewe Wapo?
5imba kafungwa mara nne mfululizoAfadhali umemjibu. Anadhani match fixing ikiwepo, wachezaji wanakuja wanachuchumaa uwanjani halafu timu nyingine inajifungia tu magoli.
simba vs kagera, vs kengold, vs jkt magoli ya kufunga 8 ya kufungwa 2Hizi ndo Akili za Washabiki wa Mpila wa Tanzania Taja Mechi Tatu za Simba za hivi Karibuni Na mechi Tatu za Yanga hizi Zilizopita Alafu linganisha Kiwango cha Ushindani Ndani ya kiwanja Kuanzia kimbinu na kiufundi Ndo utajigundua kuwa Yanga imekufanya uwe Zwazwa Kichwani.
Jifunze kujibu hoja maana una maswali 100 katika mtihani wewe majibu yako ni matatu tu, "5imba" kufungwa mara nne mfululizo, "5imba" kufungwa goli 5 na "5imba" kucheza kombe la kina mama.5imba kafungwa mara nne mfululizo
Kuna mechi fixing?