Nimeacha Rasmi Kutazama Mechi za Yanga NBC PL

Inaonyesha ndoto zako zimejaa majibu hayo manne na unaamka godoro likiwa limeloana kwa ndoto hizo.
Huwezi kushindana na Mimi kwenye hoja, Bado upo bongo lala nakupa facts unabaki na umbumbumbu wako
 
Refa ndio wa kwanza mzee, hii mipango inahusishwa watu wengi, mtoa mada kaniquote na kuwataja marefa ila kiukweli hata timu pinzani(wacheza) wapo kwny huo mchongo!
Duh! Hii kesi inazidi kuwa kubwa, watuhumiwa wanazidi kuongezeka. Kwa hiyo hadi wachezaji wa SFAXIEN walihusika katika mchongo wa kuipa Simba ushindi.
 
Ndio maana nimekwambia ukiwa mbumbumbuu/shabiki maandazi kama ww huwezi ona makosa ya timu yako.
Ile mechi kilichosababisha vurugu ni nn kama sio refa??
 
Kwani tunaongelea makosa au kubebwa? Umesema mtandao wa kuipa ushindi Simba ni mrefu na mpana sana unahusisha marefa na wachezaji.

Inaonyesha marefa wanawanong'oneza wachezaji wa timu pinzani "nendeni mcheze faulo" halafu anageuka anawanong'oneza na wachezaji wa Simba "nendeni mjiangushe niwape penati". Hahahah!

Umeshawahi kujiuliza kwa nini hiyo michongo ya Simba isubiri dakika za majeruhi na siyo kufanyika mapema kama magoli ya Yanga yanavyopatikana?
 
Kwani tunaongelea makosa au kubebwa? Umesema mtandao wa kuipa ushindi Simba ni mrefu na mpana sana unahusisha marefa na wachezaji.

Inaonyesha marefa wanawanong'oneza wachezaji wa timu pinzani "nendeni mcheze faulo" halafu anageuka anawanong'oneza na wachezaji wa Simba "nendeni mjiangushe niwape penati". Hahahah!
Kwaiyo ile mechi ya Simba na wale waarabu hukoona refa alichofanya au unajizima data??
Tufanye yaishe mzee, Simba inacheza vizuri sana na wanapata penalt za halali kabisa hamna mchongo kabisa na marefa wanachezesha fair kabisa , na Simba ikiwahaijafunga wanaongeza dakika 3 za nyongeza na sio 7 au 9!
 
Swali langu ni, wachezaji wa Sfaxien nao walihusika na huo mchongo? Unaweza kuwa na hoja maana Kibu alipiga free header!
 
Unapataje mashaka na Yanga iliyo na quality kuzidi timu zote kwenye ligi
Yanga ni bingwa mara ya 3 mfululizo
Yanga amecheza final ya mashindano ya CAF
Yanga amecheza robo final na Mamelod
Yanga yupo CAFCL
Yanga amemfunga Simba mara nne mfululizo
Ni mwehu tu atapata mashaka juu ya ushindi wa Yanga
Anashika nafasi ya ngapi huko caf
 
Swali langu ni, wachezaji wa Sfaxien nao walihusika na huo mchongo? Unaweza kuwa na hoja maana Kibu alipiga free header!
Kwasababu wengi wenu ni Mbumbumbuu(ref Aden Rage) ndio maana hunielewi!
 
Unapataje mashaka na Yanga iliyo na quality kuzidi timu zote kwenye ligi
Yanga ni bingwa mara ya 3 mfululizo
Yanga amecheza final ya mashindano ya CAF
Yanga amecheza robo final na Mamelod
Yanga yupo CAFCL
Yanga amemfunga Simba mara nne mfululizo
Ni mwehu tu atapata mashaka juu ya ushindi wa Yanga
Nakazia
 
Bahati Mbaya Unashabikia Mchezo bila kuhufahamu Mchezo Wenyewe inaonekana hujawahi kucheza hata kidogo Utotoni mkiwa mnatazama mpila Muwe Ushabiki mnauacha majumbani mwenu.
Mkuu ninauishi mpira toka udogoni mpaka sasa. Labda ungesema hoja yako kutoka kwenye maandishi yangu tungeelewana
 
Happy Holiday! Natumaini mnaendelea vizuri wana-Jamiiforums. Msukumo wa kuandika andiko hili umetokana kuangalia mechi tatu, pale ambapo Yanga amekutana na Mashujaa, Tanzania Prisons na hii mechi yake ya mwisho dhidi ya Dodoma Jiji.

Nimekua shabiki kindaki ndaki wa mpira wa Tanzania, nimeudhuria mechi nyingi sana hasa za Yanga katika msimu uliopita. Nimefurahi sana kwa wakati ule, lakini wakati naandika andiko hili nikiri kusema sitakuja kutazama tena mechi za Yanga isipokuwa zile mechi za kimataifa, au watakapo kutana Yanga vs Simba/Azam.

Kupitia mechi hizo hapo juu, sijui niseme ni uwezo mkubwa wa Yanga, au uwezo mdogo wa timu pinzani au kuna sababu nje ya uwanja au vyote kwa pamoja . Ila hizo mechi zilikua kama futuhi, ni maigizo yaani ni kichekesho. Kuna wakati unajiuliza inakuwaje hizi timu zinashiriki ligi kuu. Wachezaji wa timu pinzani wanashindana kufanya makosa, wachezaji wanashindana kutoa zawadi, labda kwa kuwa ni msimu wa Christmas.

Sizungumzi haya sababu za kuwa Yanga hapaswi kushinda, Hapana. Ila nazungumzia ushindani umepotea kabisa. Tofauti na miaka ya nyuma. Hizi mechi zote tajwa Yanga ameshinda sio sababu ya ubora wake, ila sababu ya udhaifu wa mpinzani. Ni ushindi mwepesi sana.

Mechi zote Yanga angekua makini hata kidogo tu, alikuwa na uwezo wa kupata hata magoli zaidi ya 10 maana ilikuwa ni washindwe wao tu. Hapo hapo ukitazama timu hizo tajwa zinapokutana na vilabu vya Simba na Azam basi ushindani unakua ni mkubwa sana.

Kuokoa soka letu, tulitazame hili kwa undani, tupate tatuzi za kinadharia na kivitendo ndani na nje ya uwanja. Either kuna baadhi ya vilabu vina influence katika timu hizi ndogo au gap kati ya Yanga na hivi vilabu vingine ni kubwa sana kusema kwamba inawathiri wachezaji kisaikolojia hata kabla hawajakutana nao.

Natambua kuwa tuna tamani vilabu vyetu vishinde kwa namna yeyote, lakini katika hili haihitaji uwe shabiki wa Yanga au Simba au hata mpira kuliona hili. Athari yake ni kuwa hii ligi itaenda kuwa dhaifu au kwa lugha ya kisoka kujulikana kama Farmers League.

Mdau wa soka mtazamo wako ni upi?
Achana na mambo ya Yanga na mpira kwa ujumla wake. Badala yake hamia kwenye channel inayo onesha Bongo muvi.
 
Mkuu ninauishi mpira toka udogoni mpaka sasa. Labda ungesema hoja yako kutoka kwenye maandishi yangu tungeelewana
Haya maandishi hayatoki kwa mtu anayeuishi mpila kauli zinatoka kwa mpenzi wa timu ambaye yuko radhi Chongo Aite Kengeza.
 
Mkuu sipo hapa kukuprove ni kwa namna gani nauelewa na kuuishi mpira kama hili hulitaki sema hoja yako tuzungumze. Naona mada inazidi kuhama na hatutafika muafaka.
 
Kwanza unapoleta hoja lazima utueleze ubora wa mpinzani mfano Dodoma jiji au prisons, utuambie current form ya hizo timu.. je ukipima kiubora unaona ni mpinzani sahihi iwapo yanga au timu kubwa Inakuwa na shauku ya kupata matokeo mazuri?
Pia angalia namna yanga inacheza kwa sasa ukilinganisha na siku chache zilizopita.
Kama mtu wa mpira jaribu kuangalia ata falsafa basi ambayo yanga inatumia kwasasa,, unaona kabisa muda wote wapo kwa mpinzani wanakaba kwa nguvu kias wanawanyima utuliv wapinzan na magoli yanatokea.
NB makosa wanayofanya yanga wanapofungwa na timu zingne ndo makosa wanayofanya timu ndogo wanapofungwa na yanga .. KUWA MVUMILIVU
 
Happy Holiday! Natumaini mnaendelea vizuri wana-Jamiiforums. Msukumo wa kuandika andiko hili umetokana kuangalia mechi tatu, pale ambapo Yanga amekutana na Mashujaa, Tanzania Prisons na hii mechi yake ya mwisho dhidi ya Dodoma Jiji.

Nimekua shabiki kindaki ndaki wa mpira wa Tanzania, nimeudhuria mechi nyingi sana hasa za Yanga katika msimu uliopita. Nimefurahi sana kwa wakati ule, lakini wakati naandika andiko hili nikiri kusema sitakuja kutazama tena mechi za Yanga isipokuwa zile mechi za kimataifa, au watakapo kutana Yanga vs Simba/Azam.

Kupitia mechi hizo hapo juu, sijui niseme ni uwezo mkubwa wa Yanga, au uwezo mdogo wa timu pinzani au kuna sababu nje ya uwanja au vyote kwa pamoja . Ila hizo mechi zilikua kama futuhi, ni maigizo yaani ni kichekesho. Kuna wakati unajiuliza inakuwaje hizi timu zinashiriki ligi kuu. Wachezaji wa timu pinzani wanashindana kufanya makosa, wachezaji wanashindana kutoa zawadi, labda kwa kuwa ni msimu wa Christmas.

Sizungumzi haya sababu za kuwa Yanga hapaswi kushinda, Hapana. Ila nazungumzia ushindani umepotea kabisa. Tofauti na miaka ya nyuma. Hizi mechi zote tajwa Yanga ameshinda sio sababu ya ubora wake, ila sababu ya udhaifu wa mpinzani. Ni ushindi mwepesi sana.

Mechi zote Yanga angekua makini hata kidogo tu, alikuwa na uwezo wa kupata hata magoli zaidi ya 10 maana ilikuwa ni washindwe wao tu. Hapo hapo ukitazama timu hizo tajwa zinapokutana na vilabu vya Simba na Azam basi ushindani unakua ni mkubwa sana.

Kuokoa soka letu, tulitazame hili kwa undani, tupate tatuzi za kinadharia na kivitendo ndani na nje ya uwanja. Either kuna baadhi ya vilabu vina influence katika timu hizi ndogo au gap kati ya Yanga na hivi vilabu vingine ni kubwa sana kusema kwamba inawathiri wachezaji kisaikolojia hata kabla hawajakutana nao.

Natambua kuwa tuna tamani vilabu vyetu vishinde kwa namna yeyote, lakini katika hili haihitaji uwe shabiki wa Yanga au Simba au hata mpira kuliona hili. Athari yake ni kuwa hii ligi itaenda kuwa dhaifu au kwa lugha ya kisoka kujulikana kama Farmers League.

Mdau wa soka mtazamo wako ni upi?
You nailed it
 
Kwanza unapoleta hoja lazima utueleze ubora wa mpinzani mfano Dodoma jiji au prisons, utuambie current form ya hizo timu.. je ukipima kiubora unaona ni mpinzani sahihi iwapo yanga au timu kubwa Inakuwa na shauku ya kupata matokeo mazuri?
Pia angalia namna yanga inacheza kwa sasa ukilinganisha na siku chache zilizopita.
Kama mtu wa mpira jaribu kuangalia ata falsafa basi ambayo yanga inatumia kwasasa,, unaona kabisa muda wote wapo kwa mpinzani wanakaba kwa nguvu kias wanawanyima utuliv wapinzan na magoli yanatokea.
NB makosa wanayofanya yanga wanapofungwa na timu zingne ndo makosa wanayofanya timu ndogo wanapofungwa na yanga .. KUWA MVUMILIVU
Sio kweli, match fixing tupu
 
Back
Top Bottom