Nimeacha Rasmi Kutazama Mechi za Yanga NBC PL

Nimeacha Rasmi Kutazama Mechi za Yanga NBC PL

Tawiireeeee kakaka tawireeeee
Umewaona leo wadogo zao wa kule singidani??
Nakwambia ipo siku huu upupu utaisha...
 
Happy Holiday! Natumaini mnaendelea vizuri wana-Jamiiforums. Msukumo wa kuandika andiko hili umetokana kuangalia mechi tatu, pale ambapo Yanga amekutana na Mashujaa, Tanzania Prisons na hii mechi yake ya mwisho dhidi ya Dodoma Jiji.

Nimekua shabiki kindaki ndaki wa mpira wa Tanzania, nimeudhuria mechi nyingi sana hasa za Yanga katika msimu uliopita. Nimefurahi sana kwa wakati ule, lakini wakati naandika andiko hili nikiri kusema sitakuja kutazama tena mechi za Yanga isipokuwa zile mechi za kimataifa, au watakapo kutana Yanga vs Simba/Azam.

Kupitia mechi hizo hapo juu, sijui niseme ni uwezo mkubwa wa Yanga, au uwezo mdogo wa timu pinzani au kuna sababu nje ya uwanja au vyote kwa pamoja . Ila hizo mechi zilikua kama futuhi, ni maigizo yaani ni kichekesho. Kuna wakati unajiuliza inakuwaje hizi timu zinashiriki ligi kuu. Wachezaji wa timu pinzani wanashindana kufanya makosa, wachezaji wanashindana kutoa zawadi, labda kwa kuwa ni msimu wa Christmas.

Sizungumzi haya sababu za kuwa Yanga hapaswi kushinda, Hapana. Ila nazungumzia ushindani umepotea kabisa. Tofauti na miaka ya nyuma. Hizi mechi zote tajwa Yanga ameshinda sio sababu ya ubora wake, ila sababu ya udhaifu wa mpinzani. Ni ushindi mwepesi sana.

Mechi zote Yanga angekua makini hata kidogo tu, alikuwa na uwezo wa kupata hata magoli zaidi ya 10 maana ilikuwa ni washindwe wao tu. Hapo hapo ukitazama timu hizo tajwa zinapokutana na vilabu vya Simba na Azam basi ushindani unakua ni mkubwa sana.

Kuokoa soka letu, tulitazame hili kwa undani, tupate tatuzi za kinadharia na kivitendo ndani na nje ya uwanja. Either kuna baadhi ya vilabu vina influence katika timu hizi ndogo au gap kati ya Yanga na hivi vilabu vingine ni kubwa sana kusema kwamba inawathiri wachezaji kisaikolojia hata kabla hawajakutana nao.

Natambua kuwa tuna tamani vilabu vyetu vishinde kwa namna yeyote, lakini katika hili haihitaji uwe shabiki wa Yanga au Simba au hata mpira kuliona hili. Athari yake ni kuwa hii ligi itaenda kuwa dhaifu au kwa lugha ya kisoka kujulikana kama Farmers League.

Mdau wa soka mtazamo wako ni upi?
Kwani ulivyoanza kuangalia NBCL ulitupa taarifa?
 
Kwanza unapoleta hoja lazima utueleze ubora wa mpinzani mfano Dodoma jiji au prisons, utuambie current form ya hizo timu.. je ukipima kiubora unaona ni mpinzani sahihi iwapo yanga au timu kubwa Inakuwa na shauku ya kupata matokeo mazuri?
Pia angalia namna yanga inacheza kwa sasa ukilinganisha na siku chache zilizopita.
Kama mtu wa mpira jaribu kuangalia ata falsafa basi ambayo yanga inatumia kwasasa,, unaona kabisa muda wote wapo kwa mpinzani wanakaba kwa nguvu kias wanawanyima utuliv wapinzan na magoli yanatokea.
NB makosa wanayofanya yanga wanapofungwa na timu zingne ndo makosa wanayofanya timu ndogo wanapofungwa na yanga .. KUWA MVUMILIVU
Maana yake Yanga ni bora sana kwa wakati huu. Sawa.
 
Hao Dodoma jiji kaka wakicheza na Simba ni kama mangariba...yanataka damu ni miguvu kwa kwend mbele...
Niliitazama mechi zake na dodoma au hata mashujaa. Labda tuseme Simba kwa sasa ni mid team, lakini Yanga uwezo wake ni mkubwa sana.
 
Tawiireeeee kakaka tawireeeee
Umewaona leo wadogo zao wa kule singidani??
Nakwambia ipo siku huu upupu utaisha...
Si mchezo aisee. Hata hizi motisha zinapaswa kutazamwa upya, kwanini zinawekwa kwa timu moja pekee. Kama ni matokeo chanya kwanini ilitolewe kwa timu zote zenye ubora.
 
Kuokoa soka letu, tulitazame hili kwa undani, tupate tatuzi za kinadharia na kivitendo ndani na nje ya uwanja. Either kuna baadhi ya vilabu vina influence katika timu hizi ndogo au gap kati ya Yanga na hivi vilabu vingine ni kubwa sana kusema kwamba inawathiri wachezaji kisaikolojia hata kabla hawajakutana nao.

Natambua kuwa tuna tamani vilabu vyetu vishinde kwa namna yeyote, lakini katika hili haihitaji uwe shabiki wa Yanga au Simba au hata mpira kuliona hili. Athari yake ni kuwa hii ligi itaenda kuwa dhaifu au kwa lugha ya kisoka kujulikana kama Farmers League.

Mdau wa soka mtazamo wako ni upi?
Naomba tutafute mbinu ya kuokoa ligi yetu tunayoinasibu kuwa ni bora.
 
Mwanzo ilikua ni ngumu sana kuthibitisha, ila kama mamlaka hawata simama hata katika hii Mechi dhidi ya Singida, basi wajiudhuru tu maana kazi imewashinda.
 
Nimekua shabiki kindaki ndaki wa mpira wa Tanzania, nimeudhuria mechi nyingi sana hasa za Yanga katika msimu uliopita. Nimefurahi sana kwa wakati ule, lakini wakati naandika andiko hili nikiri kusema sitakuja kutazama tena mechi za Yanga isipokuwa zile mechi za kimataifa, au watakapo kutana Yanga vs Simba/Azam.
Tulionya mapema kuwa hii mipango haisaidii, wote tumeona kimataifa Yanga alivyo-struggle while mechi za nyumbani anatamba tu.
 
Umoja wa timu zinazo fadhiriwa na GSS wameweka mkakati kuwa ni lazima mshindi wa Ligi atoke kwenye Umoja wao.
Wameunda hadi Wasap Group la kuwasiliana.
Mkakati ni kuwa Simba akaziwe kwa ahadi hadi za pesa.
Sijaona timu inawekewa ahadi ya pesa ili Uto wafungwe.

Tunamsubiri Mkuu wa mkoa siku ya mechi zao kama ataweka zawadi ya pesa ili Pamba ishinde.
 
Tulionya mapema kuwa hii mipango haisaidii, wote tumeona kimataifa Yanga alivyo-struggle while mechi za nyumbani anatamba tu.
5imba alofungwa mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 alihongwa bei gani?
 
5imba alofungwa mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 alihongwa bei gani?
Andiko langu linazungumzia msimu huu, labda sijakuelewa point yako Mkuu.
 
Ila kupitia mechi ya leo naamini TFF na bodi ya ligi lazima wataamka kutoka usingizini. Ni fedheha kubwa kwa ligi yetu.
Nakumbuka Singida hawa walivyo fungwa na Simba baadhi ya wachezaji walikuwa wanalia mpira ulipo isha.
Leo wanatoka uwanjani huku wanatabasamu.
 
Back
Top Bottom