Nimeacha rasmi kuwa shabiki wa mpira wa miguu na hizi ndizo sababu zangu

Nimeacha rasmi kuwa shabiki wa mpira wa miguu na hizi ndizo sababu zangu

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
1. Ushabiki wa mpira ni Aina Fulani hivi ya uwendawazimu, inahitaji akili ya mwendawazimu kuwa shabiki wa mpira wa miguu. Kwa mfano : Mashabiki wa timu kuomba mpira uishe pindi timu Yao inapokuwa inaongoza . Kwanini unataka mechi iishe haraka wakati wewe umeenda kuangalia mpira?

2. Tofauti Kati ya roho ya uchawi na mindset ya shabiki WA mpira wa MIGUU Ni sifuri. Ukitaka kujua wachawi huwa Wana waza Nini kuhusu wewe , wewe jitazame unawaza Nini kuhusu timu yako pinzani.. HII roho ya uchawi miongoni mwa shabiki WA mpira wa MIGUU inafanya mpira usiwe mchezo WA furaha. Kwa mfano shabiki WA Yanga kuchukia Simba kufika robo fainali au shabiki WA Simba kufurahia Yanga kutolewa makundi. I don't want to share my energy with these kind of people.

3. Mashabiki wa mpira kutokuubali ukweli Kwa Sababu ya roho ya KICHAWI inayo fanya Kazi ndani yao. Kwa mfano shabiki WA Yanga anaweza kusema Huyu Mikson au Chama Ni bonge la garasa au kumsikia shabiki WA Simba akisema " Aucho nae mchezaji? Ukitumwa mchezaji unaweza kumpeleka Aucho Kweli? I am not feeling comfortable to stay around people who think this way.

Hivi ndivyo wachawi wanavyo kataaga Kwa maneno mafanikio ya watu wengine... Mwaka 97 Kuna ndugu yangu Fulani alipata nafasi ya kwenda kusoma Scotland mtaani ikawa inasemwa anaenda kusoma Uingereza basi mchawi mmoja WA mtaani akawa anasema " Nyie Uingereza mnapajua au mnapasikia? Huyu mwanafudenge kaenda kusoma Scotland, Scotland sio Uingereza, unafanya mchezo Na Uingereza wewe..

One year later jamaa akamtumia mama Ake picha zake akiwa Scotland, Bahati mbaya picha zikavuja wachawi wakazipata, sikia maneno Yao " Huyu sio xxx ninae mjua Mimi, huyu WA kwenye picha mbona mwarabu kabisa".

Siku zote mindset ya mchawi huwa Ni kuwa around Na watu ambao Wana fit kwenye category ya partners in sufferance. Kwa Bahati mbaya Sana hivi ndivyo ilivyo akili ya shabiki WA mpira wa MIGUU.

Itaendelea
 
Uko nje ya mada kabisa, jikite kwenye lengo la post acha kuharibu nyuzi za watu.
Ameathiriwa Na roho ya uchawi ambayo mashabiki wengi wa mpira WA MIGUU wanayo. Mchawi huwa ana attack kitu kizuri ULICHO nacho Na shabiki WA mpira wa MIGUU ana attack vitu vizuri alivyo navyo mpinzani wake.
 
Uko nje ya mada kabisa, jikite kwenye lengo la post acha kuharibu nyuzi za watu.
1639248901509.png
 
mayele mzee wa kucheza ufyetele

View attachment 2040906
Yaani ndio haya anayosema mleta thread yaani ulivyo nizaidi ya chizi. Unashangaa Mayele kutotoka na goli utafikiri Simba wameingia kucheza na yanga pasipo kuhitaji kupata goli. Kagere na Morrison wameweza kuipatia simba point tatu? Au simba haikuwa na umuhimu wa kushinda hii mechi?
 
Ameathiriwa Na roho ya uchawi ambayo mashabiki wengi wa mpira WA MIGUU wanayo. Mchawi huwa ana attack kitu kizuri ULICHO nacho Na shabiki WA mpira wa MIGUU ana attack vitu vizuri alivyo navyo mpinzani wake.
Umeathirika kisaikolojia, nakushauri kwa timu hiyo ambayo unashabikia una kila sababu ya kuiona chawi.

Hama club tafuta club nzuri itakayokua inakupa furaha uwanjani
 
Kwa ulicho kiandika hapa ni dhahiri hujawahi kuwa shabiki wa mpira full stop!.
 
Yaani ndio haya anayosema mleta thread yaani ulivyo nizaidi ya chizi. Unashangaa Mayele kutotoka na goli utafikiri Simba wameingia kucheza na yanga pasipo kuhitaji kupata goli. Kagere na Morrison wameweza kuipatia simba point tatu? Au simba haikuwa na umuhimu wa kushinda hii mechi?
Kwani nani ulimuona akimtaja taja kagere kwamba ndio mchezaji tegemezi kama ambavyo nyinyi mlivyokua mnampa promo huyo pimbi?

Tulichoka na kelele zenu, saizi mmesanda msha loose hope mnajidai eti mnasusa mpira
 
Hivi ukicheza bao si unataka umfunge mwenzako ili ushinde ? Sasa kama hutaki ushindi unashindana nini na mpizani wako,lazima utamwombea mabaya ili ushinde
 
Kila la kheri,kwenye maisha mapya,mpira wa bongo ndo ulinishinda lakini majuu sina shida
Hata majuu pia siwezi shabikia Tena halafu u cannot blv nilifanikiwaga kuacha kabisa kushabikia mpira wa miguu from 2005 to 2017. Yani wakati makambo anachezea Yanga Kwa mara ya Kwanza Wala sikuwa Na habari yoyote Na mpira, wakati Amisi Tambwe ana kiwasha Yanga sikuwa Nafatilia kabisa mambo ya mpira. Nadhani labda Sababu nilikuwa nashika mamilioni mengi that time. Nilikua nawaona mashabiki wa mpira WA MIGUU kama wajinga jinga Fulani hivi wasio jielewa. I wonder how I became one of them.
 
Ungekuwa unauchukia umasikini kama unavyo ichukia Yanga ungekuwa Bakhresa.

Back
Top Bottom