Nimeachana Rasmi na Flutter. Sasa ni ios/SwiftUI

Umetema madini matupu.. wewe utakuwa ni mkali sana naomba tulink kwenye hii kazi
 
Umetema madini matupu.. wewe utakuwa ni mkali sana naomba tulink kwenye hii kazi
Mkuu njia za kujifunza ni zile zile unazotumia, unaanza na tutorial then una shift to documentation. Kwa sasa mimi natumia zaidi documentation maana zile basic ninzao hivyo nikiwa na shida na kitu sikijui kabisa basi nasearch kisha nasoma either Medium au kwenye official documentation.

Mwisho mkuu tembelea repo huko github kujifunza zaidi huko duniani wanaandikaje code maana sisi tunajifunza ila huko duniani wanaandika. Hii itakusaidia kuendana na best practise za kucode.
 
Safi sana mkuu,mimi hii ishu ni ya hela sana Acha tu.
Last app kama hii tuliingiza more than 10 m per month nikaona nijifunze mwenyewe aisee ni tight sana.
 
Mie ndio nilianzia huko... kuchokonoa codes so najua changamoto za PHP hasa ukitaka ulink na Database pia huwa inasumbua sana zile files za Sql, pole sana..

Alafu ukute code zimenyongorotwa na Javascript na PHP huo mtungo wake lazima uombe poo
Mkuu mimi naomba unisaidie roadmap ya backed kama hutojali nisije ingia mkenge wa huyo jamaa hapo juu.
 
Safi sana mkuu,mimi hii ishu ni ya hela sana Acha tu.
Last app kama hii tuliingiza more than 10 m per month nikaona nijifunze mwenyewe aisee ni tight sana.
Safii ni kupambana isipite siku hujagusa mzgo.. kila siku inatakiw uchape chape vi code hata kwa notepad
 
Unajua Lugha ngapi mpaka sasa?
mi bado beginner mkuu, nimemaliza kujifunza HTML na CSS, ndo nimeanza JavaScript, plani yangu before ilikua nikimaliza, front end ni ingie Dart na Flutter, ila naona bora nimalize na Back end kabisa, so bado sijapata pa kuelekea baada ya JavaScript, either niendelee na php, ila kutokana na huyo jamaa hapo juu, ni kama naona ntapotea.
So nahitaji roadmap kamili ya backend.
NB: Mi najifunza kama hobby tu, sina mpango wa kuja kuitumia kwa ajili ya kujipatia kipato.
 
Ni chaguo sahihi kujifunza backend kwanza kabla ya kuhamia kwenye mobile development.

Huu sio ushauri ila ni pendekezo tu.. sababu ushaanza web dev ni lazima ujifunze javascript hivo Fanya backend kwa javascript yani node js & express js.

Mimi natumia node js & express.. inachukua muda kujifunza kwa beginner, ila implementation yake ni imenyooka & it's the most popular backend kwa sasa na iko powerfull kuliko php/laravel
 
..
 
Sasa... piga PHP na Javascript vizuri uijue

Why PHP?
Php unaweza set strings zikafunction kama HTML yaan ukacheza na PHP and Css ukawa umemaliza kazi. Yeaaah.

Pia bila PHP hapo hakuna backend.. so piga PHP itakusaidia sanaaa tena cheza nayo parallel PHP na Javascript kwa Mazoezi ya Web development sana sana.

Najua Database huwezi iepuka utatumia strings za PHP kujua ni vip Database inafanyaje kazi hasa ukitak ku query taarifa lazima uitengenezee backbone huko ktk root folder.

Ukishayajua hayo nenda huko ktk mafultter etc.. maana mtu unawez tengenez app vzr ila ukaombwa ufanye duplication yake kwa Webapp ukawa unashangaa..

And uzur sahiv dunia inarahisishwa..

Unaweza Tengeneza webapp then ukaifanyia mafekeche kwa same Codes ukatoa mobile app kwa kutumia various compiling mechanisms.. instead of ku code upya.
 
Flutter bado haipo stable, ila ndio framework bora zaidi kwa cross-platform frameworks,
Ufanisi wa App hasa una tegemea na developer pia technology unayo tumia

Kwa mfano combination ya flutter na Laravel inatoa App yenye ufanisi sana,

Ukitumia Flutter na forebase pia ni unyama

Issue flutter + plain php au vue, utaiona mbaya,
 
Nashukuru sana mkuu, nitalifanyia kazi hili.
 
Shukrani sana mkuu, ngoja niyafanyie kazi haya.
 
Mkuu kwanini unasema bila php hakuna backend, wakati php imeachwa nyuma sana kwenye upande wa backend
 
Mkuu kwanini unasema bila php hakuna backend, wakati php imeachwa nyuma sana kwenye upande wa backend
PHP inaenda sambamba na JavaScript kama ilivyo Wali na Maharage jinsi inavyonoga.

Na kwa upande wa Webapp PHP kwangu ndio best backend language na hasa nikikode pamoja na JavaScript.

Php imeachwa nyuma.. like seriously?
 
PHP inaenda sambamba na JavaScript kama ilivyo Wali na Maharage jinsi inavyonoga.

Na kwa upande wa Webapp PHP kwangu ndio best backend language na hasa nikikode pamoja na JavaScript.

Php imeachwa nyuma.. like seriously?
Kwa real time data node js iko juu ukiilinganisha na php. Kiufupi interms of speed node iko juu
 
ujue syntaxes za lugha zinafanana, iwe php au node, etc
kusema kwamba uanze na lugha-a kisha uje lugha-b, naona kuna ukakasi hapo as hayo yakuanza yupi yanakuja yenyewe automatikali

sema tu, kwakua wewe ni kwa hobby, anza na php, shared hosting(bei kitonga) zote zina support hiyo
ukianza na node, itakuhitaji uwe na vps au dedicated server, tayari ushaongeza complications ku install ujinga ujinga huko kwenye server,


japo kuna namna ya ku-install node packges na kun run node apps kwa shared hosting. ambazo itakulazimu utumie php


na kumbuka tu izo node na express ni frameworks , usizikimbilie hizo kabla kuanza na ile raw JS ya kule upande wa HTML
 
Napenda sana nyuzi za haya masuala maana nimeanza kujifunza taratibu, hivyo naomba unipe muongozo ili kufikia web developer au app developer ni vitu gani vya kuanza kujifunza kwa mtiririko mzuri. Asante
 
Shukrani kwa mawazo yako mkuu, so kwa ushauri wako baada ya JS, inabidi nikasome tu php na nisiende node.js.
kama sijakwelewa vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…