Upendo iswa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2018
- 345
- 548
- Thread starter
-
- #61
Familia yetu haitabariki hata kidogo mimi kuishi na mwanaume pasipo ndoa.Mbona simpo Best umnaishi then after five years mnaenda kubariki ndoa
Shida nyie mnapenda ndoa za mwendokasi harakaharaka ndo shida
Sent using Jamii Forums mobile app
Meli imeanza kuzama hiyo..tafuta mitumbwi ambayo ipo pembezoni mwa meli ufike nchi kavu salama. Nicheki tuyajenge ila kama unalilia unampenda jitayarishe kushuhudia ndoa ya mwenzio soon. Kwani mlikutana wapi na katika mahusiano yenu anajulikana kwenu na wewe unajulikana kwao?Labda kweli ametafuta kisingizio cha kuniacha. Ila alikuwa anasisitiza sana niolewe kimyakimya ila hili halikuniingia akilini
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwao najulikana sana kwetu baadhi ya ndugu wanamfahamu. Yaani mimi baada ya kwenda kwa mwanaume wazazi wa mwanaume waende kwetu kusema kuwa nimeolewa na mtoto waoMeli imeanza kuzama hiyo..tafuta mitumbwi ambayo ipo pembezoni mwa meli ufike nchi kavu salama. Nicheki tuyajenge ila kama unalilia unampenda jitayarishe kushuhudia ndoa ya mwenzio soon. Kwani mlikutana wapi na katika mahusiano yenu anajulikana kwenu na wewe unajulikana kwao? Mpo katika mahusiano kwa muda gani..kuna sehemu sijaelewa ama sijui kusoma. Umesema anataka familia yenu iende kwao kutoa taarifa kuwa ww unaolewa na mtoto wao ama nipe ufafanuzi. Ila pokea ushauri wa wengi mara nyingi tamaa inauwezo mkubwa wa kuudanganya moyo. Jambo lingine mna umri gani wewe na muoaji kimyakimya.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sina hofu na hiliEti wataalamu, hii ni namba ngapi..? Kitu kama C ila bado inavimba, jua linasoma machweo ila bibie hastuki.... usiku utapokwisha.
Inanibidi nikubaliane na matokeo tuUnapigwa matukio ila kichwa ngumu jiongeze best
Kweli ananipenda kwa dhati ila kutokana na msimamo nilionao amekata tamaa kabisa hana upendo kama zamaniLa maana kama kijana anakupenda kwa dhati (japo hatuna kipimo cha upendo) msikilize na wazazi wanaelewa hili " kuna siku utaachana na wazazi wako na utaambatana na umpendae". Kisheria ukikaa na mwanaume zaidi ya miezi 6 ni mke na mme . Wazazi watajulishwa kwa kutumia hekima za wazee
Sent using Jamii Forums mobile app
Eti anakupenda kwa dhati🙄🙄Kweli ananipenda kwa dhati ila kutokana na msimamo nilionao amekata tamaa kabisa hana upendo kama zamani
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kipindi hicho upendo ulikuwepo sana tuEti anakupenda kwa dhati[emoji849][emoji849]
Kuna aina ya Wanaume kumtamkia mwanamke kwamba mahusiano yamefikia mwisho ni jambo gumu kwao aina hiyo ni kama huyo wako,hiyo kesi yako haitaji kuumiza kichwa kwamba jamaa hakutaka kukuoa.
Wazo hili nilimpa hakubaliani naloMwambie akajitambulishe nyumbani au atume wazee.
Na atoe mahari, ndoa mtafunga siku nyingine.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kama anakupenda yaelekea huyu jamaa yako hawathamini wala kuwaheshimu wazazi wako. Wazazi wa jamaa yako kama nao wanaafikiana naye basi nao pia hawawaheshimu wazazi wako.Kweli ananipenda kwa dhati ila kutokana na msimamo nilionao amekata tamaa kabisa hana upendo kama zamani
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo hakuna penziEti anakupenda kwa dhati🙄🙄
Tunda ashawahi kulila?Wakuu kuna jambo linanitatiza.
Nimekuwa na mahusiano kwa miaka miwili sasa huyu mwenzangu anataka tuchukuane kimya kimya (sogea tuishi) pasipo ndoa rasmi. Anaeleza kuwa baada ya mimi kwenda kwake wazazi wake waende nyumbani kwetu kutoa taarifa kuwa nimeolewa!
Kwa upande wangu nimejaribu kumueleza kuwa siyo jambo la busara mimi kufanya hivyo nahofia wazazi wangu kusononeka (nitakosa baraka za wazazi)
Nimejaribu kumweleza tutambulishane rasmi tufunge ndoa simple tu isiyokuwa na shamrashamra ila amekuwa mgumu kuelewa.
Ameamua kuniacha kisa nimekataa kuolewa kimyakimya pasipo kuwaeleza wazazi kuwa nimepata mchumba.
Bado nampenda sana nifanyeje ili tuweze kufikia suluhu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeshangaa mkuuHapo hakuna penzi
Naona binti anajiaminisha anapendwa kwa dhati! Dah!Nimeshangaa mkuu