Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Kwao najulikana sana kwetu baadhi ya ndugu wanamfahamu. Yaani mimi baada ya kwenda kwa mwanaume wazazi wa mwanaume waende kwetu kusema kuwa nimeolewa na mtoto wao

Sent using Jamii Forums mobile app
Una miaka mingapi na jamaa yako ana miaka mingapi...mnakwaruzana kila mara katika mahusiano yetu. Hivi umemaliza chuo kama ndio unaufaulu wa GPA ngapi? Maana hautakiwi hauelewi kapu limeshavuja hilo endelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama anakupenda yaelekea huyu jamaa yako hawathamini wala kuwaheshimu wazazi wako. Wazazi wa jamaa yako kama nao wanaafikiana naye basi nao pia hawawaheshimu wazazi wako.
Hili ni kweli ndugu zake wanashauri nikubali kuolewa bila kufuata utaratibu hata kama wazazi wangu watasononeka sitarudi tena kwetu kwa sababu nitakuwa tayari nimeshaolewa
Hili jambo halikuniingia akilini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ikimbie zinaa, ni vema ukarejea kwa Mungu ukatubu dhambi zako na uombe toba na rehema Mungu ni mwaminifu atakupa wa kufanana nawe mtafunga ndoa yenu takatifu na mtafurahia maisha, kamwe usije ukafuata ya mwilini utapotea.
 
Nahisi ana sababu alikuwa anaitafuta... kaipata sasa.. Binafsi sioni kwanini uolewe kimya kimya kwa maana hata taarifa isitolewe.. WHY...?? Kimya kimya inayokubalika ni ile ya kutokuwa na sherehe kabisa au kuwa na sherehe inayohusisha wachache wa karibu.. Lakini ukimwa wa kutotoa taarifa na huku unaenda kuolewa..!! hell NOOOO.... HUYU, kama nilivyosema, alikuwa anakutafutia sababu ya kukuacha... na kasimamia hiyo ambayo binafsi naona haina mashiko....

Ndoa za kiafrika familia lazima ihusike.. ahata kama ni kwa taarifa tu
 
Una miaka mingapi na jamaa yako ana miaka mingapi...mnakwaruzana kila mara katika mahusiano yetu. Hivi umemaliza chuo kama ndio unaufaulu wa GPA ngapi? Maana hautakiwi hauelewi kapu limeshavuja hilo endelea

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina miaka 27 mwanaume 33 hatujawahi kukwaruzana katika mahusiano yetu. Ndiyo nimemaliza chuo GPA haina mashiko hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo nimemwambia ila anataka kwanza nikae kwake ili wazee wake watakapo kwenda waseme kuwa tayari nimeshaolewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Anaishi kwake au anaishi kwao?

Kama anaishi kwake tu tena ikiwa ni mbali na home itakuwa ngumu kidogo kwako kuamini lengo lake. Lakini kama anaishi kwao au mazingira ya karibu na home kwao. Inaweza kuwa ana nia ya kuoa kweli. Tatizo hamjaaminiana tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwezi legeza huu msimamo wangu ni kitu ambacho hakiwezekani ila napenda anielewe umuhimu wa kufunga ndoa rasmi , pia atambue nahitaji baraka za wazazi wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sema wazi tu kuwa unataka upate leseni rasmi ya kuzini au kwa kiswahili rahisi ni leseni ya kungonoka bila woga tena. Ati upate baraka za wazazi. Kwani sasa mnapo ngonoka huwa unaenda kuomba radhi kwao asubuhi au huwa unaenda tu kuoga na kubadili nguo??
Mambo ingine Tz ni kama kuivuruga akili tu.
Amua uende kwake haraka sana la sivyo usije hapa ukilia kuwa; Aliniacha jana tu leo ako na wawili
 
Weee mdada, kwann unalazimisha kufit mahali ambapo sio kwako.


Tulia kua kimya...kama anakupenda atarudi tuu mwenyewe.
 
Amtumie mara ngapi? Women always learn the hard way!!

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Anaishi kwake, nia ya kuoa anayo ila kuchukuana pasipo utaratibu hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo leseni rasmi ina umuhimu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…