Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

Habari Kaka, mimi ni Binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba wangu. Huyu Kaka nilikaa naye kwenye mahusiano kwa miaka mittano. Lakini alianza kubadilika ghafla mpaka akampa mwanamke mwingine ujauzito wakawa wanaishi naye. Alishanitambulisha mpaka kwao lakini baada ya kumpa huyo dada ujauzito aliniambia kuwa wazazi wake hawanitaki kwakua hawana uhakika kama nina kizazi au la hivyo wamemuambia kuwa amuoe huyo mwanamke mwingine.

Nilimuambia nimbebe mimba yake akagoma na kuniambia tuendelee kuwa marafiki tu lakini suala la ndoa haliwezekanai. Niliumia sana akawa anakuja kwangu ila anaishi kwa ule mwanamke mpaka alipojifungua. Baada ya kuanza kukusoma niliona kama ananipotezea muda hivyo niliamua kuchana naye. kuna Kaka alikua ananitongoza nikaamua kumkubalia na tukaanza mahusiano, huyo Kaka alikua siriasi kwani baada ya miezi minne tu alikuja kujitambulisha kwetu, akatoa mahari na mipango ya ndoa ilianza.

Baada ya kuona kuwa naolewa X wangu alinitafuta, aliomba tuonane na mimi kwakukua nilikua na mtu wangu basi nilikubali. Huko alianza kunielezea matatizo na mwanamke wake, aliniambia kwanza ni mchafu, mchotyo, hapendi ndugu zake na anafikiria kumuacha kwani Mama yake hamtaki tena anatamania angenioa mimi. Tuliongea mengi sana lakini sikumsikiliza, ila alianza kuomba msamaha, akawa anatuma mpaka na rafiki zake.

Kwakua ni mtu ambaye nilikua nampenda nilijikuta kuwa narudi wkake, nikajikuta sina hamu tena na mchumba wangu na mwisho nikaamua kumuambia mchumba wangu mpya kuwa tuliharakisha lakini mimi simpendi hivyo nataka tuachane. Alilia sana akaumia kw2ani alidai nimemuaibisha kwao kwakua kila kitu kilishaandaliwa ila sikua na namna, niliona hakuna haja ya kuingia kwenye ndoa na mwanaume ambaye simpendi wakati mtu ninayempenda amerudi.

Ndugu zangu walinisihi sana nisimuache lakini nilishafanya maamuzi. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, baada ya kuchana na mchumba wangu huyu mwanaume alinishawishi kubeba mimba yake ili iwe rtahisi yeye kunitambulisha kwa wazazi wake kwani hawawezi kunikubali kama hawajui kuwa nazaa. Nilibeba mimba yake kweli na sasa hivi nina ujauzito wa miezi nane ila kuna mambo yamebadilika Kaka naomba unisaidie kwani nimechanganyikiwa.

Kwanza bado anaishi na X wake, mwanzo aliniambia kuwa wanaishi pamoja kwasababu ya mtoto ila yeye hana mapenzi naye kwani hata tendo la ndoa hawafanyi. Lakini Kaka mimi mimba yangu ina miezi nane nimechunguza nimegundua kuwa kumbe hata huyo mwanamke naye ana mimba ya mtoto wa pili. Kumbuka aliniambia wanalea tu mtoto, sasa Kaka namuuliza kwanini amempa ujauzito ananiambia ilikua ni bahati mbaya.

Anadai kuna siku alirudi nyumbani kalewa ndiyo mwanamke akammbaka na kumlazimisha kufanya naye mapenzi lakini yeye hamtaki. Tuligombana sana nikamuambia kuwa amuache huyo mwanamke, basi siku iliyofuata alichukua vitu vyake kwa huyo mwanamke na kuhamia kwangu. Aliniambia kuwa kaamua kumuacha mwanamke wake, lakini Kaka sio hivyo nimechunguza nimegundua kuwa kule kwa yule mwanamke kamuaga kuwa anasafiri kikazi na wala hajamuambia kuhusu mimi.

Nimemuambia si nina mimba basi anipeleke kwao kunitambulisha ananizungusha ananiambia kuwa Mama yake sasa hivi ana presha kwahiyo tutamchanganya tusubiri mpaka apone ndiyo anipeleke. Kaka naomba nisaidie, mwanuame kaja anaishi kwangu, ana kazi nzuri lakini hatoi chochote, kila kitu nahudumia mimi, yaani hata umeme ukikatika hawezi kununua. Kifurushi cha Azam kikiisha basi kama kuna mpira atanunua cha wiki nisiponunua ila ndiyo basi, naomba nisaidie kuna mapenzi kweli hapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
We nae unaleta mambo ua iddi makengo humu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mpaka sasa hv bado unafikiria tu utoe maamuz gani katika ilo swala?. Yani uende kuishi getoni kwa mwanaume bila wazazi wako kujua?, afu bado wasema wampenda tu?. Pole sana huyo hakupendi, ngoja upate mimba ndiyo uje uone rangi yake ipoje. Mimi ata iweje, ata nikiachwa Mara 20 lakini sitakubali sogea tuishi ata siku moja.

Hiifadhi heshima yako na ondoka kwenu kwa heshima, weka historia njema mtaani. Ata kama hujafunga ndoa lkn amekuja amejitambulisha na ametoa posa kama tamaduni yetu ya kiafrika inavyosema. Ss ya nini ujishushie heshima sbb ya mwanaume asiyekupenda wala kukujali?. Kwani yuko peke yake?, jiamini utapata mwingine achana naye. Yani ukamfulie, ukampikie, na huduma ya papuchi umpe kwa kukutorosha bila wazazi wako kujua?. Amka we mdada hizi si zama za kulazimisha mapenz kwa mtu.
 
Hivi mpaka sasa hv bado unafikiria tu utoe maamuz gani katika ilo swala?. Yani uende kuishi getoni kwa mwanaume bila wazazi wako kujua?, afu bado wasema wampenda tu?. Pole sana huyo hakupendi, ngoja upate mimba ndiyo uje uone rangi yake ipoje. Mimi ata iweje, ata nikiachwa Mara 20 lakini sitakubali sogea tuishi ata siku moja.

Hiifadhi heshima yako na ondoka kwenu kwa heshima, weka historia njema mtaani. Ata kama hujafunga ndoa lkn amekuja amejitambulisha na ametoa posa kama tamaduni yetu ya kiafrika inavyosema. Ss ya nini ujishushie heshima sbb ya mwanaume asiyekupenda wala kukujali?. Kwani yuko peke yake?, jiamini utapata mwingine achana naye. Yani ukamfulie, ukampikie, na huduma ya papuchi umpe kwa kukutorosha bila wazazi wako kujua?. Amka we mdada hizi si zama za kulazimisha mapenz kwa mtu.
Nimekuelewa sana mkuu sikuwa tayari kabisa kutoroka kwetu niende kwa mwanaume pasipo kufuata utaratibu
Kweli huyu mwanaume hana complication za sherehe, ila nilimshauri anitolee posa nikiwa bado kwetu hakutaka kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vizuri sana kwa msimamo ulio nao. Usitoke kwenu mpk atoe posa.
Nimekuelewa sana mkuu sikuwa tayari kabisa kutoroka kwetu niende kwa mwanaume pasipo kufuata utaratibu
Kweli huyu mwanaume hana complication za sherehe, ila nilimshauri anitolee posa nikiwa bado kwetu hakutaka kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko hivi unapopenda kwa dhati hupendwi na pale unapopendwa kwa dhati hupendi.
Sio lazima iwe hivii,Kuna wakati unapopenda kwa dhati,unapendwa piah kwa dhati

Sent using Jamii Forums mobile app,using POP 2 power
 
Wakuu kuna jambo linanitatiza.
Nimekuwa na mahusiano kwa miaka miwili sasa huyu mwenzangu anataka tuchukuane kimya kimya (sogea tuishi) pasipo ndoa rasmi. Anaeleza kuwa baada ya mimi kwenda kwake wazazi wake waende nyumbani kwetu kutoa taarifa kuwa nimeolewa!

Kwa upande wangu nimejaribu kumueleza kuwa siyo jambo la busara mimi kufanya hivyo nahofia wazazi wangu kusononeka (nitakosa baraka za wazazi)

Nimejaribu kumweleza tutambulishane rasmi tufunge ndoa simple tu isiyokuwa na shamrashamra ila amekuwa mgumu kuelewa.

Ameamua kuniacha kisa nimekataa kuolewa kimyakimya pasipo kuwaeleza wazazi kuwa nimepata mchumba.

Bado nampenda sana nifanyeje ili tuweze kufikia suluhu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo ni gia za kuachwa kama gia zingine, alishausoma huo udhaifu ndio akapitia hapo hapo.
 
Unajua nyie wanawake mkishauriwa mnaenda kufanya opposite, mtu kashakuonyesha kuwq wewe huna thamani kwake ya nini kuupa kiherehere moyo!?. It's better uumie utakuwa fine baada ya muda coz no love pains inadumu maisha, wounds heal. Inaonekana unampenda na anachukulia for granted, jitambue thamani yako na mapenzi yasibadilishe misimamo.

Man of the hour.
 
Back
Top Bottom