Futa namba zake na kila kumbukumbu uliyobaki nayo kuhusu yeye iondoe, jibu la mwisho ulilompa la kukubaliana na wazo la kuachana nae ndo iwe meseji yako ya mwisho kwake usitake tena kujua chochote kuhusu yeye endelea na maisha yako.
Usimpigie simu wala kutuma meseji yoyote ya kuonyesha bado unamuhitaji huo ni udhaifu, ukiweza kufanya hivyo ndani ya mwezi mmoja tu unamsahau akiona matokeo hayo asiyo yatarajia ataanza kukutafuta yeye lakini usirudi nyuma akituma meseji usijibu chochote zifute pamoja na namba yake, jenga maisha yako.