Unique Flower
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 12,838
- 25,282
Sawa....Mpe hug zito simu haitoshi
Ila siku hizi umenitenga sanaSawa....
Tunapowaleta kina nani??Unaona eeeeh..
Sasa sisi hiyo kasheshe ndo maisha yetu kila siku huku mnapo waleta 🤓🤓🤓🤓🤓🤓
Unategemea takua serious na life kweli hapo...🤓🤓🤓🤓😂😂😂
Jamanj Ua langu la kipekee,sema sipo online kila siku napotea hata siku nne so hutuonani,,,we damu yangu kabisa na unajua Hilo😘Ila siku hizi umenitenga sana
Polee sanaMaisha ni lazima yaendelee.
Nakiri kwamba nilikuwa malaya sana zamani lakini nikaamua kubadilika baada ya kugundua kwamba mahusiano mengi kwa wakati mmoja yanapoteza muda, rasilimali fedha, yanadhoofisha mwili, akili n.k.
Nimekuwa kwenye mahusiano serious kwa takribani mwaka na nusu na Mwl mmoja wa Shule ya msingi. Mpole, msikivu, mcha Mungu, mnyenyekevu, sio mbinafsi, mshauri mzuri na zaidi ya yote amekuwa mfano bora wa mama wa familia. Nikaamua kumpenda kwa dhati. Nikawaambia hadi ma-x wangu. Nikawa najiachia nae, nikamtambulisha kwa baadhi ya wana.
Nikakaa kitako na Baba nipeleke barua ya posa, binti akaridhia. Barua ikaandikwa, mwanangu mmoja ambaye ameshaoa akakubali kuwa mshenga. Barua ilikuwa ipelekwe tangu j5 ya wiki iliyopita ila nikapata dharura tukaahirisha. Ilikuwa baada ya kupeleka posa ndio nikamtambulishe home.
J'mosi ya juzi akaanza kubadilika kuanzia kwenye mawasiliano na kila kitu. Jana nampigia simu aniambie barua tupeleke lini, akashtuka kama hajui kinachoendelea! Akajibu nisubiri kwanza, mara anaomba tupeane muda kuna mambo ajiridhishe!
Nikajiongeza, nikamwambia muda siwezi kumpa kwasababu tulishalizungumza hili. Aseme tu kama anadhani hatuwezi kuwa pamoja tena nitamuelewa. Akasisitiza nimpe muda! Nikamjaribu kwa kumwambia tuachane ili tusipotezeane muda (kumbuka hapa nilikuwa namjaribu); ili nione anawaza nini.
Lahaulaa, akasema 'SAWA'. Nikaishiwa nguvu. Nilikuwa barabarani nikasimama kwanza kwasababu nilipatwa na wenge nikahisi naweza kusababisha ajali.
Ina maana ile kupenana muda ilikuwa ni gia tu, alishaamua tuachane. Sikumtafuta tena tangu jana na yeye kakaa kimya mpaka muda huu!
Huyu ni msichana aliyeniaminisha kwamba hawezi kuniacha. Kwamba hata nikijaribu kumuacha atafanya jambo baya (ni kama alikuwa anatishia kujiua).
LAWAMA ZANGU ZOTE NAZIELEKEZA KWA RAFIKI YAKE MWENYE JINA LINALOANZA NA HERUFI 'J', ANAYEISHI MKOA UNAOANZA NA HERUFI 'M'. Mpenzi wangu alikuwa anamsikiliza sana, na mara nyingi wamekuwa wakiniongelea, nina kila sababu ya kuamini kwamba ushauri wake umechangia kumfanya mwanamke wangu afikie uamuzi huu. Huyu dada yeye kaolewa, leo kaamua kumfanyia figisu rafiki yake! We dada wewee....
Biblia imesema tushukuru kwa kila jambo. Pengine kuna jambo Mungu ameniepusha nalo. Naumia ila najikaza.
Ctrl+ CNdio mnaringaga mnaaita wanawake majinA mabovu , hamuwaheshimu ,wala kuwajali eti mashangazi na mtakuwa single hivi hivi wanaume mnatakiwa muwe na staha na mipaka, na muwe makini, kwa kila jamboo sio muwe waongeaji ,tulieni hamzai mnazalisha so kuweni nastara kubwa akili kuliko wanawake zenu . Ila humu wengi mnalaana fulani,mnadharau sana. Mkiachwa ndio mnajirudi
Sijaelewa
Haya ila mzima ??Jamanj Ua langu la kipekee,sema sipo online kila siku napotea hata siku nne so hutuonani,,,we damu yangu kabisa na unajua Hilo😘
Dah! Mkuu, Mimi unanionea bure tu. Sijawahi kumdharau mtu humu.Ndio mnaringaga mnaaita wanawake majinA mabovu , hamuwaheshimu ,wala kuwajali eti mashangazi na mtakuwa single hivi hivi wanaume mnatakiwa muwe na staha na mipaka, na muwe makini, kwa kila jamboo sio muwe waongeaji ,tulieni hamzai mnazalisha so kuweni nastara kubwa akili kuliko wanawake zenu . Ila humu wengi mnalaana fulani,mnadharau sana. Mkiachwa ndio mnajirudi
Salama vipi wewe?nimeona Kuna sehemu unawanga wanaume wa humu wanaringa imekuwaje tena?Haya ila mzima ??
Eti eh basi tuombe Mungu akupatie mke mwemaDah! Mkuu, Mimi unanionea bure tu. Sijawahi kumdharau mtu humu.
Sawa mkuu. Yote kheri.Thats karma,,kama kuna wakati uliwahi kuumiza mioyo ya wanawake wasiokuwa na hatia. Mungu anakupitisha kwenye tanuli lile lile ili ujue ni namna gani watu wanaumia sababu ya mapenzi.
Pole sana ili usiwe mtumwa wa mapenzi kubali kuachika.
Sent using Jamii Forums mobile app
Pisi zipo nyingi Mzee unaumia kisa mtu hujazaliwa nae achana nae utapata pisi nono ..tuliza wenge Mzee au ndio mara ya kwanza kupenda??
Kabisa mkuu.Ila kwenye mapenzi,ujasiri sawa lakini sijui kuna nini hakuna cha msomi,mjanja,mjuaji,wa mjini,mboga1,mboga7,waziri,yaani ni taaabu na kujilisha upepo!
Sio vigari vya chini kama crown, naendesha Discovery 4 Hybrid, la juujuu.daaah mkuu "la juu", unamaana gani? au ndo
Mkuu umeongea point sana vijana wanakosea sana mwanamke ndo anatakiwa ndo kulazimisha ndoa ila siyo mwanaumePole Mkuu Amicus Curiae huwa naelewa sana falsafa zifuatazo katika mahusiano.
1. Ni makosa makubwa mwanamke kufahamu kuwa bila yeye mambo yako yatakwqma, hakika mwanamke akilijua hilo lazima akusumbue tu.
2. Hii inabebana na iyo ya kwanza, kamwe mwanaume haupaswi kujishusha mbele ya mwanamke hasa mwanamke uliye naye kwenye mahusiano. Huna sababu ya kujieleza kwa jambo lolote kwake. Ila muhimu wewe muheshimu tu na mipaka izingatiwe.
3. Usimuombe mwanamke kumuoa wewe fanya mambo yako hadi siku yeye atakapoomba wewe umuoe na kamwe usikubali akuendeshe au kukulazimisha kumuoa
Sasa Mkuu huyu mwanamke alijua bila yeye mambo yako hayataenda, huyo usihangaike naye kabisa funga ukurasa focus kwenye mambo mengine.
Pole sana Mkuu Amicus Curiae