Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

Pole sana.. usijizuie kuumia ila ukubali hiyo imeenda.
Mapenzi yanauma sana [emoji22]
 
Maisha ni lazima yaendelee.

Nakiri kwamba nilikuwa malaya sana zamani lakini nikaamua kubadilika baada ya kugundua kwamba mahusiano mengi kwa wakati mmoja yanapoteza muda, rasilimali fedha, yanadhoofisha mwili, akili n.k.

Nimekuwa kwenye mahusiano serious kwa takribani mwaka na nusu na Mwl mmoja wa Shule ya msingi. Mpole, msikivu, mcha Mungu, mnyenyekevu, sio mbinafsi, mshauri mzuri na zaidi ya yote amekuwa mfano bora wa mama wa familia. Nikaamua kumpenda kwa dhati. Nikawaambia hadi ma-x wangu. Nikawa najiachia nae, nikamtambulisha kwa baadhi ya wana.

Nikakaa kitako na Baba nipeleke barua ya posa, binti akaridhia. Barua ikaandikwa, mwanangu mmoja ambaye ameshaoa akakubali kuwa mshenga. Barua ilikuwa ipelekwe tangu j5 ya wiki iliyopita ila nikapata dharura tukaahirisha. Ilikuwa baada ya kupeleka posa ndio nikamtambulishe home.

J'mosi ya juzi akaanza kubadilika kuanzia kwenye mawasiliano na kila kitu. Jana nampigia simu aniambie barua tupeleke lini, akashtuka kama hajui kinachoendelea! Akajibu nisubiri kwanza, mara anaomba tupeane muda kuna mambo ajiridhishe!

Nikajiongeza, nikamwambia muda siwezi kumpa kwasababu tulishalizungumza hili. Aseme tu kama anadhani hatuwezi kuwa pamoja tena nitamuelewa. Akasisitiza nimpe muda! Nikamjaribu kwa kumwambia tuachane ili tusipotezeane muda (kumbuka hapa nilikuwa namjaribu); ili nione anawaza nini.

Lahaulaa, akasema 'SAWA'. Nikaishiwa nguvu. Nilikuwa barabarani nikasimama kwanza kwasababu nilipatwa na wenge nikahisi naweza kusababisha ajali.

Ina maana ile kupenana muda ilikuwa ni gia tu, alishaamua tuachane. Sikumtafuta tena tangu jana na yeye kakaa kimya mpaka muda huu!

Huyu ni msichana aliyeniaminisha kwamba hawezi kuniacha. Kwamba hata nikijaribu kumuacha atafanya jambo baya (ni kama alikuwa anatishia kujiua).

LAWAMA ZANGU ZOTE NAZIELEKEZA KWA RAFIKI YAKE MWENYE JINA LINALOANZA NA HERUFI 'J', ANAYEISHI MKOA UNAOANZA NA HERUFI 'M'. Mpenzi wangu alikuwa anamsikiliza sana, na mara nyingi wamekuwa wakiniongelea, nina kila sababu ya kuamini kwamba ushauri wake umechangia kumfanya mwanamke wangu afikie uamuzi huu. Huyu dada yeye kaolewa, leo kaamua kumfanyia figisu rafiki yake! We dada wewee....

Biblia imesema tushukuru kwa kila jambo. Pengine kuna jambo Mungu ameniepusha nalo. Naumia ila najikaza.
Polee sana
 
Ndio mnaringaga mnaaita wanawake majinA mabovu , hamuwaheshimu ,wala kuwajali eti mashangazi na mtakuwa single hivi hivi wanaume mnatakiwa muwe na staha na mipaka, na muwe makini, kwa kila jamboo sio muwe waongeaji ,tulieni hamzai mnazalisha so kuweni nastara kubwa akili kuliko wanawake zenu . Ila humu wengi mnalaana fulani,mnadharau sana. Mkiachwa ndio mnajirudi
Ctrl+ C
Amicus Curiae Ctrl + V
✍️✍️✍️✍️✍️
 
Kwenye mapenzi mara nyingi watu wanadandia mahusiano ya watu bila wenyewe kujua......unakuta mtu ana mtu wake wanapendana sema kwa muda huo walikuwa wametofautiana akaamua kuwa na wewe kama njia ya kupunguza upweke na mawazo.....mwisho wa siku akipatana mtu wake wewe unapigwa kibuti mfano wa shuti la Kibu alilomfunga mdaka mishale........


Ogopa sana yule mtu mnaanza tu mahusiano lakini anakuja na mahaba utasema maji yaliyotegeshwa yakamwagika........
 
Jamanj Ua langu la kipekee,sema sipo online kila siku napotea hata siku nne so hutuonani,,,we damu yangu kabisa na unajua Hilo😘
Haya ila mzima ??
[/QUOTE]
Salama vipi wewe?nimeona Kuna sehemu unawanga wanaume wa humu wanaringa imekuwaje tena?
 
Ndio mnaringaga mnaaita wanawake majinA mabovu , hamuwaheshimu ,wala kuwajali eti mashangazi na mtakuwa single hivi hivi wanaume mnatakiwa muwe na staha na mipaka, na muwe makini, kwa kila jamboo sio muwe waongeaji ,tulieni hamzai mnazalisha so kuweni nastara kubwa akili kuliko wanawake zenu . Ila humu wengi mnalaana fulani,mnadharau sana. Mkiachwa ndio mnajirudi
Dah! Mkuu, Mimi unanionea bure tu. Sijawahi kumdharau mtu humu.
 
Mkuu umefanya jambo zuri...Wana JF - ukiachwa, kubali kuachika.....Hongera sana..Endelea na Maisha..Na utapata hitaji la moyo yako..
 
Thats karma,,kama kuna wakati uliwahi kuumiza mioyo ya wanawake wasiokuwa na hatia. Mungu anakupitisha kwenye tanuli lile lile ili ujue ni namna gani watu wanaumia sababu ya mapenzi.

Pole sana ili usiwe mtumwa wa mapenzi kubali kuachika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu. Yote kheri.
 
Wewe ndiyo yawezekana kweli umeacha umalaya lkn mwezako bado malaya kama ulivyokuwa wewe! Halafu unataka kummiliki?? Jiongeze na uachane naye.
 
Pole Mkuu Amicus Curiae huwa naelewa sana falsafa zifuatazo katika mahusiano.

1. Ni makosa makubwa mwanamke kufahamu kuwa bila yeye mambo yako yatakwqma, hakika mwanamke akilijua hilo lazima akusumbue tu.

2. Hii inabebana na iyo ya kwanza, kamwe mwanaume haupaswi kujishusha mbele ya mwanamke hasa mwanamke uliye naye kwenye mahusiano. Huna sababu ya kujieleza kwa jambo lolote kwake. Ila muhimu wewe muheshimu tu na mipaka izingatiwe.

3. Usimuombe mwanamke kumuoa wewe fanya mambo yako hadi siku yeye atakapoomba wewe umuoe na kamwe usikubali akuendeshe au kukulazimisha kumuoa

Sasa Mkuu huyu mwanamke alijua bila yeye mambo yako hayataenda, huyo usihangaike naye kabisa funga ukurasa focus kwenye mambo mengine.

Pole sana Mkuu Amicus Curiae
Mkuu umeongea point sana vijana wanakosea sana mwanamke ndo anatakiwa ndo kulazimisha ndoa ila siyo mwanaume
 
Back
Top Bottom