Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni



Haya ni maelezo ya upande mmoja. Ni ngumu kutoa hukumu katika huu muktadha.

Kabla sijaenda mbali, hiyo wewe unaiita kumjaribu, kumbuka hakujua kama una mjaribu au unamaanisha, ulitaka Binti wa watu apokee namna Gani hizo taarifa?

Kumbuka uliahirisha kwenda kupeleka mahari, haujasema sababu ipi ilitokea na hiyo taarifa uliiwasilishaje upande wa wakwe.

Kama kweli unamhiraji na una maanisha, naamini unaweza kurekebisha makosa Yako mkayajenga.

Utatoa melezo Gani kwamba ulikua unamjaribu? Kwa sababu zipi na malengo Gani?
 
mpe muda
 
Nikiri tu kwamba huyu ndio mwanamke nilimpenda kwa moyo wangu wote.
Na pia nadhani ulijitoa sana kwake kwa kila kitu. Going forward be careful unapodeal na mwanadamu; na angalau uwe tayari kwa lo lote maana mwanadamu anaweza kubadilika wakati wo wote. Jitoe kwa upendo huku ukijua kuwa ni sadaka tu unatoa lakini siyo kwa kutegemea cho chote maana kusema kweli loyalty ya mtu huwezi kuinunua ama kwa material things wala upendo wako wa kweli. Mwanadamu anaweza kuwa kiumbe katili sana akiamua!

Lakini pia kama malengo yako yalikuwa safi kwa huyu binti (if your intentions were pure) basi ondoka na dhamira safi huku ukijua kuwa hukumpotezea muda wake...and the Universe will reward you handsomely. Mwache aende na mtakie mema ila usije ukashangaa huko mbele ya safari kama atataka kurudi tena.

Kwa sasa hakuna njia ya mkato. Kuumia ni lazima utaumia lakini utavuka. Kwa kadri muda unavyokwenda maumivu nayo polepole yatapungua; na nati hizo zinazokaza kwenye moyo zitaanza kuachia na furaha yako itarudi.

Na ni lazima uchukue tahadhari. Usije ukaishia kuchukia wanawake wote. Huyu hakuwa wako na imeonyesha hivyo. Hata kama ungelazimisha basi huko mbele ya safari ungeumia zaidi ya unavyoumia sasa. Angalia tu usije ukaenda huko ukilalama na kuita kila mwanamke ni laghai, mbwa na malaya. Hutakuwa sahihi. Na siku moja utakuja kumpata aliye wako ambaye atakuonyesha mwanamke mwema na waifu matirio yukoje. Endelea kumtafuta mwanamke huyo kwa roho njema, moyo safi na dhamira isiyo na mawaa na siku moja utampata tu.

Sasa umekua! πŸ‘πŸΌπŸ‘πŸΌπŸ‘πŸΌπŸ’ͺπŸ’ͺ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…