Nimeahidiwa Q-Net kuwa bilionea baada ya miaka mitano

Nimeahidiwa Q-Net kuwa bilionea baada ya miaka mitano

Wanakutisha tu na kukukatisha tamaa ili usiwe millionea.

Hapo mdogo wangu hesabu tu siku, hizo biashara zinalipa sana. Shida kwa wengi ni mtaji tu wa hiyo mil 5.

Kajiunge haraka sana, mimi ningekuwa hata na mil 2 tu ningewafata niwabembeleze nijiunge
Hapana we kaka usimpoteze mwenzio hivyo huyo ni mtz mwenzio usione anapotea ukamuangalia hivyo.

Sent from my SM-S9 using JamiiForums mobile app
 
. Nimechoka kuwa maskini.

USHAURI JAMANI!

Unaweza kupata 5.5m yakuwekeza uchaguzi hadi uchaguzi lakini unaona huna pesa. Kwann usiendelee na biashara iliyokupa hiyo milioni 5 unazotaka kuchezea? Iwapo kila mwaka utatunza 5.5 baada ya miaka 5 utakuwa na 27+ milion. Utanunua saa hata ya milioni ambayo ina thamani kuliko hiyo ya 5m. Muulize huyo aliyekupa hilo wazo, hapendi ndugu zake wawe bilionea?
 
Kumbe watz mitaji tunayo shida akili tu ya biashara...
We ukiona umewazaa chakufanya hukioni nenda kabet ili hela yako iende kihalali kuliko kutumatuma hovyo. Hao Q-net hawana tofauti na wale "Hiyo hela tuma kwenye namba hii..."

Kichwa BoX
 
Na akibeti akatusua hata kwa odds 3 kila siku, kwa mwezi anakuwa na si chini ya 150 milioni[emoji3][emoji3][emoji3] ee Mungu saidia asiione hii comment maana anaonekana anapenda mserereko. Hakawii kuanza kubeti.
 
Ajabu ni kwamba hadi kuna watu wanaingia hii mikenge.
Hiyo ni ponzi . Ni deci nyingine tu.
Formula ni ile ile. Mtafute mjinga mmoja ili akusaidie kutafuta wajinga wengine
 
Unaweza kupata 5.5m yakuwekeza uchaguzi hadi uchaguzi lakini unaona huna pesa. Kwann usiendelee na biashara iliyokupa hiyo milioni 5 unazotaka kuchezea? Iwapo kila mwaka utatunza 5.5 baada ya miaka 5 utakuwa na 27+ milion. Utanunua saa hata ya milioni ambayo ina thamani kuliko hiyo ya 5m. Muulize huyo aliyekupa hilo wazo, hapendi ndugu zake wawe bilionea?
Daah...! Good idea. [emoji108]
 
Nasema hivi 29m+ Ni idadi ya kupika. Watanzania tupo 59m+, hiyo ina maana 29m+ ni nusu ya watanzania wote. Inatakiwa mtu kuwa mjinga wa kiwango chako, ili kuamini kuwa watu wazima yaani 18yrs+ ni sawa kabisa ya walio chini ya umri huo. Halafu mbali ya utata huo wote 29m wajiandikishe, halafu wapiga kura wawe 1/3 ya waliostahili kupiga kura.

Iko hivi;

Kuna dada fulani hivi tuliwahi kufahamiana huko nyuma, alinipigia simu na kunijulisha kwa kina kuwa kuna mchongo fulani hivi kashawishika kujiunga nao ni wa Q-net. Wenyewe unatakiwa mtu unahudhuria semina zao mbili then utatakiwa kujiunga kwa shs. Milioni tano na laki tano (5,500,000/-) kwa kima cha chini. Pesa hio unailipa kwenye account yao in terms of dollars Hong Kong au Malaysia. Ukishailipa unachagua moja ya bidhaa zao eidha saa, mikufu, au vito vingine vya thamani vilivyotengenezwa kwa madini.

Ukishamaliza hio process unakuwa tayari partner, sasa na wewe unaanza kutafuta watu wengine wa kuwaunga ili biashara iendelee. Utatakiwa kuunga watu mfano wa tree diagram au ngoe kwa wale waliowahi kusoma hesabu za ngoe, utaunga watu kulia kuanzia wawili na kuendelea na kushoto hivohivo. Unaeza unga mfano, kulia watu kumi na kushoto watu kumi. Gharama ni hiohio (mil. 5.5) kila mmoja. So the way wanavyoingia ndivyo na wewe kwenye account yako inafura mihela, maana kwa kila anayejiunga wewee unapata gawio.

Sasa patamu aliponiaambia ni kuwa nikiwa na partiner kumi kulia na kumi kushoto, nahao partiner wangu wakafanya hivo, na partner zao wakafanya hivo, na wa kwao tena wakafanya hivo yaani hivohivo na kuendelea, baada ya miaka mitano nakuwa bilionea wa kutisha hapa nchini.

Akanisisitiza faida unaanza kuiona kuanzia nikiwa na pertner wawili. So juhudi yangu ya kupeleka watu kwenda kuungwa kwenye branch account yangu ndivyo ntakavyozidi kuwa milionea.

Mimi niko mkoani Singida ila wao hao Qnet ofisi yao ipo Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.

Sasa ndugu zangu wanajamvi kabla sijafanya maamuzi magumu nimeona hichi kitu nikilete hapa kupata ushauri kabla sijakurupuka. Nimechoka kuwa maskini.

USHAURI JAMANI!
Waeka mbali na watoto.
Usijekusema hatukukuonya
 
Hata mimi nina milioni 10 sielewi chakufanya..! nimekwama nipeni idea
 
Hao watu wa kuwekezea kwa jina lako kwenye kampuni unawapata wapi kwa mtaji huo? Huu ni utapeli kama utapeli mwingine hakuna mahali popote duniani unaweza kupata ela kirahisi tu, ni lazima jasho likutok.
 
Iko hivi;

Kuna dada fulani hivi tuliwahi kufahamiana huko nyuma, alinipigia simu na kunijulisha kwa kina kuwa kuna mchongo fulani hivi kashawishika kujiunga nao ni wa Q-net. Wenyewe unatakiwa mtu unahudhuria semina zao mbili then utatakiwa kujiunga kwa shs. Milioni tano na laki tano (5,500,000/-) kwa kima cha chini. Pesa hio unailipa kwenye account yao in terms of dollars Hong Kong au Malaysia. Ukishailipa unachagua moja ya bidhaa zao eidha saa, mikufu, au vito vingine vya thamani vilivyotengenezwa kwa madini.

Ukishamaliza hio process unakuwa tayari partner, sasa na wewe unaanza kutafuta watu wengine wa kuwaunga ili biashara iendelee. Utatakiwa kuunga watu mfano wa tree diagram au ngoe kwa wale waliowahi kusoma hesabu za ngoe, utaunga watu kulia kuanzia wawili na kuendelea na kushoto hivohivo. Unaeza unga mfano, kulia watu kumi na kushoto watu kumi. Gharama ni hiohio (mil. 5.5) kila mmoja. So the way wanavyoingia ndivyo na wewe kwenye account yako inafura mihela, maana kwa kila anayejiunga wewee unapata gawio.

Sasa patamu aliponiambia ni kuwa nikiwa na partiner kumi kulia na kumi kushoto, na hao partner wangu wakafanya hivo, na partner zao wakafanya hivo, na wa kwao tena wakafanya hivo yaani hivohivo na kuendelea, baada ya miaka mitano nakuwa bilionea wa kutisha hapa nchini.

Akanisisitiza faida unaanza kuiona kuanzia nikiwa na partner wawili. So juhudi yangu ya kupeleka watu kwenda kuungwa kwenye branch account yangu ndivyo ntakavyozidi kuwa milionea.

Mimi niko mkoani Singida ila wao hao Qnet ofisi yao ipo Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam.

Sasa ndugu zangu wanajamvi kabla sijafanya maamuzi magumu nimeona hichi kitu nikilete hapa kupata ushauri kabla sijakurupuka. Nimechoka kuwa maskini.

USHAURI JAMANI!
mimi yupo dada ninaemfahamu muda mrefu nae yupo kwenye hizi mambo za kutafuta hela kwa njia hii ya tree network anakaribia miaka mitano anahangaika na hawa jamaa wa foreverliving basi kila siku haishi kuniomba hela ya kula mpaka leo hajatoka na alinishawishi sana nijiunge nikamwambia mpaka nione wewe umetoka ndio ntajiunga. so hizi ni biashara za wajanja wachache wakitumia njia ya UPATU.
 
Mtu una milioni 5 na nusu isiyo na kazi na bado unajiita maskini?
 
Kuna Mzee alikopa hadi pesa bank ili apate mara 2 zaidi [emoji16][emoji16]yaani we acha tu, mwisho walikula pesa na hakuna alichopata.
Kuna dada aliacha kazi bureau baada ya kudanganya na mwenzake, akakopa pesa akapeleka Qnet, mbona alikimbia mji.
 
Back
Top Bottom