Nimeahidiwa Q-Net kuwa bilionea baada ya miaka mitano

Kuna best friend wangu amejiunga na hao watu mimi nikiwa away, nimerudi amenishawishi nimekataa sasa amevunja kabisa urafiki na mimi kisa nimekataa kujiunga na Q-net, hao jamaa wamehamia mikoani tafadhali wapeni taarifa na ndugu zenu wa mikoani huko wawe makini.

Sent from my SM-S9 using JamiiForums mobile app
 
Hapana we kaka usimpoteze mwenzio hivyo huyo ni mtz mwenzio usione anapotea ukamuangalia hivyo.

Sent from my SM-S9 using JamiiForums mobile app
 
. Nimechoka kuwa maskini.

USHAURI JAMANI!

Unaweza kupata 5.5m yakuwekeza uchaguzi hadi uchaguzi lakini unaona huna pesa. Kwann usiendelee na biashara iliyokupa hiyo milioni 5 unazotaka kuchezea? Iwapo kila mwaka utatunza 5.5 baada ya miaka 5 utakuwa na 27+ milion. Utanunua saa hata ya milioni ambayo ina thamani kuliko hiyo ya 5m. Muulize huyo aliyekupa hilo wazo, hapendi ndugu zake wawe bilionea?
 
Kumbe watz mitaji tunayo shida akili tu ya biashara...
We ukiona umewazaa chakufanya hukioni nenda kabet ili hela yako iende kihalali kuliko kutumatuma hovyo. Hao Q-net hawana tofauti na wale "Hiyo hela tuma kwenye namba hii..."


Kichwa BoX
 
Kumbe watz mitaji tunayo shida akili tu ya biashara...
We ukiona umewazaa chakufanya hukioni nenda kabet ili hela yako iende kihalali kuliko kutumatuma hovyo. Hao Q-net hawana tofauti na wale "Hiyo hela tuma kwenye namba hii..."


Kichwa BoX
Na akibeti akatusua hata kwa odds 3 kila siku, kwa mwezi anakuwa na si chini ya 150 milioni[emoji3][emoji3][emoji3] ee Mungu saidia asiione hii comment maana anaonekana anapenda mserereko. Hakawii kuanza kubeti.
 
Ajabu ni kwamba hadi kuna watu wanaingia hii mikenge.
Hiyo ni ponzi . Ni deci nyingine tu.
Formula ni ile ile. Mtafute mjinga mmoja ili akusaidie kutafuta wajinga wengine
 
Daah...! Good idea. [emoji108]
 

Waeka mbali na watoto.
Usijekusema hatukukuonya
 
Hata mimi nina milioni 10 sielewi chakufanya..! nimekwama nipeni idea
 
Hao watu wa kuwekezea kwa jina lako kwenye kampuni unawapata wapi kwa mtaji huo? Huu ni utapeli kama utapeli mwingine hakuna mahali popote duniani unaweza kupata ela kirahisi tu, ni lazima jasho likutok.
 
mimi yupo dada ninaemfahamu muda mrefu nae yupo kwenye hizi mambo za kutafuta hela kwa njia hii ya tree network anakaribia miaka mitano anahangaika na hawa jamaa wa foreverliving basi kila siku haishi kuniomba hela ya kula mpaka leo hajatoka na alinishawishi sana nijiunge nikamwambia mpaka nione wewe umetoka ndio ntajiunga. so hizi ni biashara za wajanja wachache wakitumia njia ya UPATU.
 
Mtu una milioni 5 na nusu isiyo na kazi na bado unajiita maskini?
 
Kuna Mzee alikopa hadi pesa bank ili apate mara 2 zaidi [emoji16][emoji16]yaani we acha tu, mwisho walikula pesa na hakuna alichopata.
Kuna dada aliacha kazi bureau baada ya kudanganya na mwenzake, akakopa pesa akapeleka Qnet, mbona alikimbia mji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…