Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Sasa si mpaka awepo around, alisema miezi minne tangu April.
 
Tangu umeandika huu uzi hadi sasa umebakiwa na mwezi mmoja kwa mujibu wa Dr wako

Ila nikuambie kitu
Maandalizi ndo kitu kikubwa
Kitakachokusaidia
Kama wewe ni muislam na unaswali huna haja ya kuogopa


Swali sana swala za usiku tafuta sehemu wanazojenga miskiti toa dhaka na swadaka

Panda miti ya matunda
In shaa Allah
 
Pole sana mkuu. Kansa hii ni mojawapo ya kansa mbaya kabisa kwa sababu survival rate yake ni ndogo mno (chini ya asilimia tano kama sikosei). Hii inasababishwa na ukweli kwamba huwa haina dalili za kueleweka na mpaka mgonjwa akahisi kuwa kuna tatizo tayari imeshafika stage 4 na pengine kusambaa kwenye viungo vingine vya mwili. Kama ulivyotaja hapo juu, dalili yake kubwa ni kupungua uzito bila sababu za msingi. Mtu una kilo 100 lakini unapungua kilo 10 kwa kipindi kifupi tena bila sababu ya maana. Kwa watu wembamba tayari kama akina Steve Jobs (mwanzilishi wa Apple) hata hii dalili hakuiona kwa sababu tayari alikuwa mwembamba. Walihangaika wee mpaka kumuwekea ini jipya lakini haikusaidia. Ni kifo cha shida na mahangaiko sana.

Pole kwa kuondokewa na mzee wako. Yeye keshaikamilisha safari yake. Bado sisi na hatujui tutaondokaje. Wakati wetu ukifika tuombe tu tuondoke kwa amani na si hivi vifo vya kuteseka kwa maumivu ya muda mrefu usiku na mchana miezi na miezi [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Asante. Mihogo yaweza kuponyesha kansa (kama huu ushuhuda ni kweli). Tiba nyingi zimo kwenye vyakula na makampuni mengi ya madawa yanapigana kufa na kupona ili kufanya watu wasielewe hizi tiba mbadala. Steve jobs pia alijaribu kwanza kujitibu kansa yake kwa kutumia matunda na mizizi na alikataa kufanyiwa operesheni mapema.

Angalizo muhimu ni kwamba tuanze kula vyakula hivi hata kabla hatujaugua. Tumeanza kula mavyakula haya ya kizungu na kudharau vyakula vyetu vya kiasili na tayari kansa imecharuka. Tumeiga mifumo ya maisha ambayo siyo yetu.
 
You almost made me cry
 
Yupo Mungu muumba wa mbingu na nchi, Yeye hutoa na pia hutwaa!! Jikabidhi mikononi mwake. Kama ni mipango yake upone, hakika utapona kwa uweza wake.. Kama mipango yake ulale usingizi wa mauti, hakika utalala usingizi wa mauti. Lakini kunatumaini ng'ambo ya kaburi. Hakika waliomtumaini Mungu, kwa jina la mwanae Yesu Kristo, hao wataokolewa katika ujio wake kuihukumu Dunia, ila wanao chezea nafasi ya maisha kwa kumwabudu ibilisi na anasa zake, hao hakuna tumaini ng'ambo ya kaburi. Jisalimishe mikononi mwa Mungu leo hii, kwa Jina la YESU, Amen!!
 
was kidin boss nlitaka kujua na kuutukuza ufalme wa Mungu maana ni mwez wa 5huu naiona hii post
 
Taarifa za huyu MTU nani anazo?? Na Anaehusika na rambi rambi humu ndani ni nani? MUNGU Anisaidie nami nijue mwezi wangu wa Kufa, maana trh 09/08 yaani week 2 kutoka sasa Huyu ndg yetuAtamaliza zamu yake..
 
Taarifa za huyu MTU nani anazo?? Na Anaehusika na rambi rambi humu ndani ni nani? MUNGU Anisaidie nami nijue mwezi wangu wa Kufa, maana trh 09/08 yaani week 2 kutoka sasa Huyu ndg yetuAtamaliza zamu yake..
We umejuaje hayo? Je kam bado yupo hai?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…