Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Stay positive, tumia vyakula organic, endelea na maisha yako kama kawaida, you never know, kuna watu wengi ambao wamevuka makisio ya madakitari wakaendelea kuishi na wengine wamepona maradhi yao kabisa.
And above all jikabidhi kwa Mwenyezi Mungu uendelee kumtukuza.
Best wishes bro
 
Maskini
Last seen yake may sijui alijiua?
Au miezi minne haikufika

Au huenda yuko ICU
 
ndo maana nikauliza, kama yuko hai si aje hapa awe anatuaga washikaji zake?? Ili tumpatie salamu zetu?? Wewe hutaki kufa unataka uushi milele??
Mkuu, kama kweli aliambiwa hivyo na ni kweli basi kwa sasa toka aweke uzi wake huu sidhani kama atakuwa ktk hali ya kuingia humu.
 
Kifo ni lazima huwezi kukwepa kila chenye mwanzo kina mwisho.Sema ni mapema ila usiogope , pokea kama unavyopokea x- mas au new year
 
Daktari sitegemei kama anaweza kutoa majibu ya aina hiyo kwa mgonjwa! Kuna lugha fulani ya jinsi ya kuhudumia na kutoa majibu kwa mgonjwa si rahisi rahisi namna hiyo. Watu wa kuhudumia wagonjwa wa ishi kwa matumaini wanalijua hili iweje daktari aliyesomea miaka mitano?

Mkuu inawezekana Dr. Akasema hilo. Nakumbuka niliwahi kukutana na dada mmoja wa kizungu huko Ngorongoro aliambiwa atakufa kwa cancer ndani ya miezi 6. Hivyo akawa anatalii duniani na boyfriend wake kama sehemu ya kuaga dunia na kutumia fedha zake. Alikuwa mdhoofu sana huyo dada. Kwa bahati mbaya sikupata akili ya kuchukua mawasiliano ya boyfriend wake kujua kama kweli alikufa ndani ya hiyo miezi 6.
 
dah! kuna watu tuna shida sana humu duniani .. utadhani tuliomba au kulazimisha tuzaliwe vile !
nakufikiria sana rafiki yangu mzuri nakuombea wepesi wa machungu uliyonayo lakini pia kama ni safari imewadia basi.... Mungu na akufupishie siku za mateso yako maana kama ni mlango umeshaufikia....
Hapo pigania imani yako....hiyo itakuponya... .. usife moyo ili uje kuwa shahidi!
 
Pole mkuu. Kuambiwa hivyo na dokta haimaanishi ni lazima iwe hivyo.

Hata marehemu Steve Jobs alikuwa na aina hiyo ya kansa. Na kama sijakosea iligundulika when he was on early twenties. Na chanzo cha hiyo kansa ni kwamba he was exposed to mercury at the age of 14.

Doctors gave him like 6 months of living (Kama sijakosea). But he survived kwa muda mrefu sana beyond what doctor's predictions.

So, stay strong broh.
 
Huu uzi unatia simanzi sanaaa,
Hapa kila mtu ndio anamkumbuka Mungu wa mbinguni, lakini kitambo kidogo tunasahau tunaendelea na ubaradhuli wetu, Mungu atusaidie kwa kweli maana kwa akili zetu ni mtihani mzitoo.
Yaani tunajisahau Sana Mungu atusaidie tupate ufahamu wa kumjua na kumtumikia yeye wakati wote.
 
Hapa duniani wote ni wapita njia. Kila mmoja wetu ataaga maisha haya tuliyonayo kwa aina yake na ni vema kutojua siku wala saa ya kuondoka kuliko kuwa na 'deadline' kama ya mwenzetu. Inaumiza sana ila pengine ni vema kujua kama hivyo ili ujiandae kwa kuweka mambo yako sawa. Wengi hatuogopi kufa bali tunaogopa kuwaacha wale tunaowapenda sana. Kifupi ni kwamba unapozaliwa tu tayari unakuwa candidate wa kufa. Maisha yetu yanatawaliwa na mambo 3 makubwa hapa duniani ambayo kwa kifupi yamepewa herufi 3 za BCD. B= BIRTH, C= CHOICES na D= DEATH. Haya mambo 3 hayakwepeki kwa kila binadamu. Pole sana mwenzetu. Mwenyezi Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu unachopitia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom