Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Folk.
Mungu akupe maisha,upate kushuhudia UKUU wake.Naamini bado upo hai.
 
Ok now change to be a better person from your heart
Tena endelea kujitafakari then chukua hatua
Siwez sema am such bad person lakin vile vile am not a good one, ila ki uhalisia asaiv ukiniuliza "Are you a bad person or good one?" to be honest from my heart "Am a bad person". Hakuna binadam asiyejijua, Kama ishawah kukutokea waweza ukae uwaze "hv mimi n mtu mwema/mzuri au laa?" na nakuhakikishia wewe huwez kujidanganya mwenyewe basi jibu utakalo lipata ndo ukweli na ukijidanganya unajua kbsa umejidanganya ili kujifrahsha au kujipa matumain, kwa ufup nafsi yako haiwez ikakudanganya wewe mwenyewe, binadamu tumepewa uwezo wa ku ji tathmini wenyewe, unajijua/jielewa zaid ya mtu mwingne yeyote. Unaweza ufanye mambo ya kuonekana mwema kwenye jamii lakn wewe mwenyewe nyuma ya pazia unajijua kama hio sio roho yako bali unajivalisha, Pia jamii inaweza ikuone mtu mbaya lakn ukweli unajua kbsa wewe si mtu mbaya na ni kweli, sio watu wabaya wote wanaonekana wabaya na sio watu wazuri wote wanaonekana wazuri(usipoteze mda kujidhihisha kua wewe n mwema) tena mara nying ni kinyume chake, nafsi halisi ya mtu ni siri yake yeye na muumba.
Mm najijua si msafi kbsa wala mchafu kbsa kwa maana hio siwez simama machoni pa Mungu. NIMEAMUA KUANZA KUJIFUNZA TARATIBU NAMNA YA KUBADILIKA(hayo maneno yaelewe vzr) nasema hvyo nikijua ya kua suala la kubadilika hasa kiroho si suala la kuamua bali linaanza taratb kwanza kwa kumruhusu Muumba wako aufanyie kaz moyo wako. Nafanya maamuz haya kwanza nikijua ya kua wengi tunakurupukaga kuamua hv ila hatukawii kurud tulikotoka, pili nikijua weng tu wasahaulifu(unasikitika mara moja, unaumia mara moja, unaamua mara moja mwisho unasahau mara moja) yote haya nayatambua. Jpili njema, Leo kanisan kumeingiliwa tena naenda kukaa mbele sitak vishawish. Nisipo anza kubadilika kpnd hk basi nguvu ya zida inahtajka
 
Huyo daktari amekosea..kwa technology tulionayo hapa bongo so far ni ngumu kujua zimebaki siku ngapi kulingana na ugonjwa husika..ula km yeye ameweza haya ni kheri..

I believe wote tutasherehekea mwaka mpya mkuu..i believe
Sio kweli, mimi wazazi wangu wote 2 niliandaa mazishi yao wakiwa wazima tunaongea. Baada ya kuambiwa na dr. Kuwa wana chini ya siku10 za kuishi. Wote walikufa katika mda uleule ambao dr. Alisema
 
Sio kweli, mimi wazazi wangu wote 2 niliandaa mazishi yao wakiwa wazima tunaongea. Baada ya kuambiwa na dr. Kuwa wana chini ya siku10 za kuishi. Wote walikufa katika mda uleule ambao dr. Alisema
mmh!
 
Kijana wala usiwe na hofu hutakufa kwa agizo la mwanadamu,Mwanadamu hana uwezo huo kukatisha mpango wa Mungu.Nataka kujua uko wapi nikupe msaada na uishi umri wako kama Mungu alivyokuahidi nitafute kwa Whatsup No.0623507595 Naahidi kukupatia msaada wa kukuondolea janga hilo la kutamkiwa kifo kabla ya mpango wa Mungu. kama huna whatsup basi tuma sms ya kawaida tutaongea.Do it now ! Sihiitaji hela yako hata senti tano pls.
 
Sio kweli, mimi wazazi wangu wote 2 niliandaa mazishi yao wakiwa wazima tunaongea. Baada ya kuambiwa na dr. Kuwa wana chini ya siku10 za kuishi. Wote walikufa katika mda uleule ambao dr. Alisema
Ni kweli kabisa, hata muhimbili hapo wanaweza kujua.
 
Uzi naona uliwekwa April, 2018 na leo ni August, 2018. Sasa cha ajabu ni kuwa umekuja tena na maneno kuwa huenda ukafikisha miezi 8. Pole sana, ila kidume usikate tamaa ya kuishi. Wala hayo maumivu siyo ya kukuua bali kukufanya umtafute Muumba wako zaidi. Ningelitamani kifo cha jinsi hiyo ili nipatane na Mungu kwani najua sasa naiacha dunia niende kwingine na huko kuna uchaguzi. Upatane na Muumba uende kwake au umkatae uende kuzimu.
Yoh. 14:6 anasema; Mimi ( Yesu) ndiye njia, kweli na uzima. Mtu haji kwa Baba (Peponi) ila kwa njia ya mimi(Yesu Kristo). Hakuna nabii mwingine yeyote aliyesema hayo ila huyu mmoja tu. Mwamini yeye uende unakojua yaani mbinguni aliko.
 
marehemu baba yangu alifariki na ugonjwa huu Kansa ya kongosho(CARCINOMA HEAD OF PANCREASE) mwaka Jana mwezi wa kumi..kwakweli alipitia maumivu makali sana yan alikongoroka akawa kama MTU anayeugua UKIMWI alibaki mifupa tupu hata kukaa ilikua shida mana nyama matakon hamna kwahiyo alikua anaumia muda mwing alikua analala huu ugonjwa ni hatar tulitafuta tiba lakn ikashindikana akafia muhimbili...huu ugonjwa unamfanya mgonjwa apoteze hamu ya kula,inasabisha nyongo kutoingia tumboni kwahiyo choo kinakua cheupe kama chokaa,yan akila muda huo huo kinatoka,weight loss hii kila siku anapungua bila Ku notice,baba yangu alikua na 100kg siku ya mwisho tunampima alikua na 43kg yan kuna muda nlikua nalia nasema mungu ampumzishe mana alikua amechoka sana,kumbu kumbu zilishaanza potea...niliweza Ku google ugonjwa huu nikaona moja ya chanzo cha maradhi haya ni MTU kuwa na mawazo au msongo mkali wa mawazo na nikalinganisha na mzee wangu nikagundua ni kweli mana baba alikua ametengana na mama aliishi maisha ya upweke mpaka hapo ugonjwa huu ulipoonza na ilimchukua mwaka 1 na nusu mpaka anafariki dunia
Pole sana Mkuu
May his soul RIP!
 
Nimedhoofika sana. Nitakufa punde.
Amini hutakufa bali utaishi maana ni ahadi ya Mungu, nakuomba ujaribu kwenda kwenye maombi Mungu wa Mbinguni aliyeumba mbingu na nchi atakuponya, utakuwa mzima na utayasimulia matendo makuu ya Mungu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom