Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
Hutakufa bali utaishi ili uyasimulie matendo makuu ya Mungu. Kama bado uko hai na ukapata fursa ya kusoma post hii, basi ujue Mungu yuko upande wako. Uelewe kuwa:
1. Adui mkubwa na tatizo kubwa la mwanadamu siyo magonjwa wala umaskini bali ni DHAMBI.
2. Muasisi wa dhambi ni shetani. Kupitia dhambi magonjwa yalipata mlango wa kumtesa mwanadamu.
3.Mwivi (shetani) huja ili kuiba, kuua na kuharibu.
4. Yesu alikuja ili tuwe na uzima kisha tuwe na uzima tele.
5. Nguvu ya mauti ni dhambi.
KWA HIYO mchakato wa kuondokana kabisa na tatizo lako ni kama ifuatavyo:
1. Ng'oa kabisa mzizi wa tatizo katika maisha yako ambao ni dhambi. Tekeleza hilo kwa kutubu dhambi zako kwa Mungu kwa dhati ya moyo wako wote!! Mkaribishe Yesu katika moyo wako kama unavyoweza kumkaribisha mgeni nyumbani kwako. Mwambie akusamehe dhambi zote na umkubali kama Bwana na mwokozi wa maisha yako yote kwa maneno yako na kwa kinywa chako na kwa sauti yako mwenyewe. Fanya yote haya kwa dhati.
2. Mwombe Yesu kwa Jina lako akuponye magonjwa yako yote.
3. Tafuta mtu aliyeokoka na anasali kanisa linaloamini wokovu na kuishi maisha matakatifu. Wako wengi na kila kona. Msimulie hatua uliyochukua na atakupa ushauri zaidi na kukupeleka kanisani ambako utaonana na mchungaji. Napendekeza kanisa la TAG, KLPT, au FPCT ambayo ninayafahamu vizuri. Usipoteze muda kwa "mitume na manabii" wa kileo!! Hutaweza kupambanua ni yupi ni wa kweli na yupi ni tapeli!!!
Ukifanya yote hayo kwa moyo wako wote kwa dhati, nina uhakika Mungu atakusaidia na hautakuwa wa kwanza. Halafu njoo hapa ulete mrejesho. Mungu ni mponyaji. Ukiokoka mauti haitishi tena maana ni mlango tu wa kuingilia mbinguni. Lakini hautakufa mapema kiasi hicho!!!!!