Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Bado hazijafika mkuu Sasa sijui tatizo Nini, halafu pm yangu ya JF sijui ikoje naweza tumia meseji au ujumbe leo nikaupata kesho Sasa inakuaje wakuu Nini tatizo....
Ingia kwa browser. Usitumie jf application, maana inaumwa
 
Yote kwa yote Dr ana nafasi yake.
Mbona wanawekaga Matarajio ya kujifungua na yanakuwa kweli!ata Magonjwa pia.
Dr naye hiyo taaluma kapata toka kwa Mungu au tuseme Atlanta

Nilipenda posti zile za kumtia moyo na kujaribu hata kumtafutia Dawa na zaidi zile za kumwambia ni Muda wa kushikamana na Mungu wake/kumrudia Mola kwa imani yake.

Nyingine ni kuumizana na kuendelea kumwibia Mgonjwa na kumtaabisha.

Mf:Njoo uokoke,Njoo kwa Mchungaji flani,Naamini Mungu mwenyewe Ndiye aliyetuambia tutakufa ,huko kwa Mchungaji atapigwa sadaka na kutaabishwa japo siyo wote.Ukifikiria sana pia Kunawagonjwa wengi tu na wanapo patikana Panafahamika kwanini hao wasinyooke huko?pia tuliona walioponywa kwa kuombewa uponyaji. pia wanao Fufua Mbona tunayajua Makaburi Mengi na Ndugu zetu nao walisha kufa.
Mtasema ni imani ,Swali waliofufuliwa na Yesu Kama Lazaro aliomba yeye Marehemu?kama siyo Mbona hata ss tulio okoka Mbona hatuwaombei Ndugu zetu? Hatuna imani?kama hatuna imani wamwiteje mwingine aje aamini hambacho huamini?
Niwashukuru Nduguzangu Waislamu kwani hawana mihemko hiyo na ukifwatili posti wengi Ndio waliotumia neno:Ajipatanishe na Mola wake kwa Imani yake na kuendelea kutafuta tiba.
Ila ndio hivyo Japo inauma Kwa kumpoteza Ndugu yetu, Mungu Ndiye Mpangaji wa yote na kw Sababu azijuzo yy.

Lipo funzo/Mafunzo kubwa/Makubwa sana kwetu Ndugu zangu wana Jf kw hili la Ndugu yetu.MUNGU Aturehemu pia.
 
Mitayari nimezipata info zake, jamaa zake pia nimewasiliana nao na hata picha zake nimezipata mkuu....
Na inasemekena jamaa alikata pumzi huku akiwa mwenye tabasamu, na waliokua karibu nae wanasema nikama alikua mwenye amani na tayari alimrudia Mungu wake
Tunaotarajia marejeo ya Kristo mara ya pili kuwafufua watakatifu wake, tunaimani tutaonana naye tena asubuhi ile njema
 
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4.)

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Pia soma > Atakayenisaidia hili nitampa Tsh milioni moja taslimu

Bye bye Mother earth.
mkuu naandika haya nikiwa nabubujikwa na machozi, kwanza nianze kwa kumtukuza Mungu kwa uumbaji wako, niseme kwamba Mungu hakeagi kila jambo linatendeka kwa waja wake lina maana yake, naamini kwamba Mungu bado anakuhitaji kuwa mtumishi wake endelea kumutukuza kuna siku utajua ni kwa nn haya yatokee juu yako, naziona mbingu zimefunguka juu yako na malaika wema wamejipanga kukuketisha katika kiti cha enzi,

nenda ndg yetu dunia hii si yetu ipo mbingu ambayo ndo makazi yetu ya milele, wafurahiao duniani pengine inaweza kuwa tofauti sana kule mbinguni.
safari ni yetu sote hakika naliita jina lililokuu kwa unyenyekevu kuu likawe ndo tumaini pekee kwa mda huu mfupi uliobaki kwa upeo wetu wanadamu, lango la mbinguni li wazi kwa ajiri yako.

amen
 
Hapa sio sawa mkuu, labda nikutumie PM
Usisambaze picha za marehemu bila ridhaa yake mkuu, ni injustice and a crime.
Hakutaka kuweka wazi mambo yake mengi kwa consent yake iweje wewe ufanye hivyo.
Heshimu haki yake ya usiri.
Angetaka kuweka wazi angetuambia hadi kwao tukaenda kula wali kwenye msiba but hakupenda iwe Hivyo na sisi tuiache Hivyo. Umepata bahati ya kupewa taarifa za kifo chake, Shukuru.
 
Kwakua alijua kuhusu kifo chake, na hakuamua yeye binafsi kuweka picha zake humu.... Basi nadhani nivyema tukayatendea haki mawazo ama maamuzi yake.....
New #1,003
Sasa hapa kutuma hutaki,,pm zimeshasambaaa,,,si bora utume tu,,ni yaleyale,,watu wa pm ndo wa hapa
 
i lost my friend nilisoma nae shaaban robert anaitwa Patrick Kibwana alifariki tarehe 22 June mwaka huu kama sikosei . Age 28 alikuwa na amefariki kwa Cancer ya Kongosho sasa sijui huu uzi ni wa nani . but i miss kaka yangu bestie yangu wa darasa Patrick Kibwana. forever love bro . love u
Pole sana mkuu,kaondoka bado mdogo sana jamaa.Mungu amrehemu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom