Nimeambukizwa virusi vya UKIMWI (H.I.V)

Nimeambukizwa virusi vya UKIMWI (H.I.V)

Habari wanaJF, mim ni kijana niliyekuwa ninajichunga na kuijari sana afya yangu kiasi cha kuwa na mabox ya vipimo vya H.I.V rapid test ghetto, ikiwa kama nimejichanganya bas nawahi dawa za PrEP,

Dawa za PrEP nimemeza round mbili yaani 2017, 2020 baada ya kucheza rough.

nilikuwa napima maambukizi na mwenza wangu mara kwa mara, Ivi sasa mwenza wangu anamalizia masomo ili mwakani July tuanze kuishi pamoja. sasa mwez Agosti mwaka huu nimekutana na mwanamke ambae tunameet na kusekx na uwa tunacheki afya sasa mwez huo nikapuuza kwakuwa tulicheki afya mwez May nikamla then maisha yakaendelea,

Mwez Octoba juzi tu nikajaribu kupima peke yangu ghetto nikakutana na mistari miwili CONTROL na 1, nilipima zaid ya mara tano apo apo gheto inasoma mistari miwili. Dah pressure ikawa kubwa.

Nikaenda Hospital napo inaonesha nipo POSITIVE, wakanianzishia dawa za ARV's adi sasa ninamaliza wiki tangu nianze dozi za ARV's. next wiki wananianzishia na dozi ya miezi sita ya Anti-T.B...

Juzi nipo YouTube nakuta kuna shuhuda nyingi sana kwamba kuna Mtaalamu anaponesha ili janga from POSITIVE to NEGATIVE anaitwa TR. MSIGWA, jaman waungwana kuna yeyote mwenye hakika na ili jambo ata ndugu yake alipata kupona kwa uyu docta maana kichwa kinawaka saiz sielewi, nikapata mawasiliano yake akaniambia dozi ni shilling 280k ya siku 45 inaitwa (4A9).

Wajameni ivi ili suala linaukweli dawa iyo ya Asili inasaidia kwa yeyote aliyawahi pata experience hii ata kwa ndugu yake kuhusu uyu mtaalamu TR. MSIGWA na dawa yake ya 4A9 maana ninawiki tu tangu nianze kumeza ARV's lakin naihis hali ya kuzichoka tayar. .

nawasilisha:
Mdogo Angu soma hapa ni muhimu USIACHE Nitaandika maelezo marefu kwa sababu inahitaji kuongea zaidi ili uweze kuelewa plz nitajaribu kufupisha kadri navyoweza !

Polee Sana!

Matatizo tumeumbiwa binadamu,Kikubwa ni kuamini kwamba kila linalotukuta lina sababu Japo si Rahisi kuijua sababu kwa mara moja!

Kwanza kabisa Unaonekana bado upo kwenye denial na bado huamini kama Kweli unaweza kuwa na maambukizi, tuliza akili Mdogo wangu huu wakati ulionao ni wakati ambao akili yako bado haiamini kila kitu na inaamini sana kuwa bado muda unao na unaweza kupona na kuondoa Virusi hivyo mwilini..

Huu ni wakati ambao akili yako inaamini kuwa HIV ni kifo na kumbe swala hilo si la kweli!

Kwenye wakati huu wengi sana hupotea na tunapoteza Wengi kwa kukosa washauri wenye uelewa mzuri wa maswala ya maambukizi na wengi huamini kila kitu wanachoambiwa na kuona mitandaoni, Na huku wengine wakitapeliwa Pesa nyingi sana huku tatizo lao likibaki pale pale..

Huu ni wakati ambao unapaswa kutulia na kufata ushauri wa Daktari na washauri wengine mahali ambapo umeanza huduma ya Tiba na matunzo nafikiri kuliko wakati wowote ule....

Mpaka Sasa Si WHO, CDC,CRO, Medspace wala NIMR waliotangaza Dawa ambayo huenda ni mbadala wa ART..
Japo bado baadhi ya reseaech na procedure zinaendelea....

Kwahiyo ukitoa pesa ili kupata suluhisho la hilo tatizo lako utakuwa unaibiwa....

Na mdogo wangu naomba nikushauri katu asije mtu yoyote kukudanganya kuhusu Kuacha kutumia Dawa za ART kwa kigezo utumie Dawa zake...

Kwa sasa katika mwili wako kuna High production ya Virus wanamultiply sana na ndo maana ni wakati mbaya sana kuacha kunywa dawa!
HIV virus Si kirusi kinacho attack nutrients za mwili kwamba utakunywa dawa yenye protein ili kuzidisha protein na kufanya Waondoke mwilini...

NGOJA NIKUPE SOMO KUHUSU HIV NA DAWA ZA ART ZINAVYOFANYA KAZI ILI UPATE UELEWA KUWA ART NI BORA KULIKO HIZO MITISHAMBA

HIV Ni ina kirusi cha RNA na kinafahamika kama Retrovirus kwa kuwa kina tabia ya kujibadili na kuwa DNA kwa Kujichanganya Na vinasaba vya Mwili wa binadamu na hapo ndo huweza kubadili baadhi ya commands kwenye mwili na ku alter information za kawaida za mwili na kuamrisha mwili kutengeneza Wadudu ama virusi wengi kadri iwezavyo...

Utengenezwaji huu na upangwaji wa Virusi (Virion)
Hufanyika kwa haraka sana ndani na nucleas na nje ya nucleas ya Cells za binadamu katika hali hiyo cells nyingi hushindwa kuhimili Hali hiyo na nyingi huwa weak na kuharibika...sana sana hizi Tcells aina ya CD4 Kwakuwa ndiyo attachment yake na receptor au kufuli l funguo yake ndipo lilipo...

Kuna hatua kadhaa hufanyika ili kirusi kiweze kutengenezwa na kuharibu cells hatua hizo ni...
  • Kufungamana au kujishikiza kwenye cells ambayo ni cells ya CD4 (CD4 receptors- CCR5) kwa lugha nyingine huitwa Binding au Attachements
  • Kuungana au Fusion kirusi huingia ndani ya cells na kutoa vitu vyake vilivyo ndani..
  • Kujibadilisha kwa lugha nyingine huitwa Reverse transcription--kwakuwa RNA ni vigumu kuweza kufanya transcription (Kutoa order katika miili yetu kumbuka order hutoka kwa DNA na hutumwa kwa mfumo wa mRNA) virusi hufanya reverse transcriPtion yaani hujibadili kutoka HIV-RNA na kuwa HIV DNA na hapa ndo shida huanza..
  • Hatua inayofuata ni kujizalisha kwa wingi inavyowezekana ili kupata virusi wengi hatua hii huitwa Replication..
  • Kwa kuwa Ndani ya cells katika replication ni utengezaji wa material tu hatua hii hufanyika Kupanga material zote zilizotengenezwa huitwa assembly
  • Hatua ya mwisho ni budding ni kutoka kwa ile ile virus zilizotengenzwa ili zikomae na kwenda kufanya hatua hizo kwenye cells nyingine....
Nafikir umeelewa kuhusu hizo hatua zote...
Hakuna dawa yoyote ya mitishamba itakayozuia hatua yoyote kufNyika....
Sasa ART ina kazi moja wapo ya kuzuia hatua hizo kufanyika ili kuzuia uharibifu wa cells zaid na kuongeza kinga kwa kufanya hivyo...

Kuna dawa za ART Zinazuia kufanyika kwa...
binding/attachments tunaziita CCR5 antagonist pia zipo Post attachment inhibitors
Pia zipo zinazuia hatua ya Fusion (Fusion inhibitors)
Hatua hizi za mwanzoni huwa ni ART za sindano na kwa Tanzania bado hatujawahi kuwa nazo kwa sababu ni ghali...
Na hatua zinazofuata zote huwa na inhibitors zake..
Lengo la kuzuia HIV kufanya hivyo vyote ni ili ishindwe kuzaliana na Mwili utashughulika na HIV zilizokuwa weak na hazieleweki through engalf system ya macrophages..

Sasa kwanini nimekuambia yote haya kwa sababu ya kukujengea Kujiamni mwenyewe kuwa bado Una nguvu na wala Usiwaze kuhusu hicho unachowaza uko sawa na kutumia dawa kutakuweka katika afya nzuri sana..

Ukiacha kutumia dawa kwa hali yoyote ile utasababisha usugu wa Dawa (Drugs Resistance) ambayo inaweza kupeleka kufail kwa matibabu ya ART (ART drugs Failure) na ukifika huku inakuwa ni hatari sana...kwa sababu ART tena haitaweza kufanya chochote kwwnye mwili wako..

Kwahiyo jitahidi unywe dawa kwa wakati na baada ya miezi sita Angalia hali ya virusi kama unatumia dawa na lishe bora unaweza kujikuta upo kundi la watu walio na kiasi kidogo sana cha HIV (TND for HIV in HVL- Target Not Detected for HIV in HIV VIRAL LOAD)..

Najua ni Safari ndefu lakini ni fupi kama utajiamini na kuondoa hofu yoyote..
Asante kwa muda wako..
Na kama una swali unaweza kuuliza

NB: hakuna mtu aliyepima HIV positive baada ya muda akawa negative unless kafanya Bone Marrow transplant na yenyewe huwa ina 5% ya curetage...
 
Bilionea la Virusi
Pole kaka jitahidi kufuata taratibu
Kupata Ukimwi sio mwsho wa maisha
 
Chai jabaa[emoji478][emoji478][emoji261][emoji261]
FB_IMG_1689244373343.jpg
 
Tangazo lako umeliweka kitaalamu sana.
 
Pole sana, zingatia dozi utaishi muda mrefu kama ilivyo kwa wengine

kwa tiba asili huwa nasikia kumenya kisha kuchemsha cactus ni dawa ila hakuna mrejesho credible mpaka sasa

View attachment 2802367

huko mitandaoni jihadhari kuna matapeli wanajinadi ni madokta, wachungaji, ustadh, waganga, ni mabingwa pia wa kuandaa shuhuda za kuvutia wateja.
Kwa sisi tunaoangalia tabia za mimea kuhusianisha na dawa (wagangawaganga) cactus inasound kama inaweza kuwa dawa🤔

Si unaona vyenye ilishagundua kwa mageuko ya miaka na miaka namna ya kujilinda na wanyama na wadudu. Huwa hailiwi ile kizembe.

Basi kuna uwezekano inaijua Code ya ulinzi binafsi na ukiinywa inaweza kuufundisha mwili kujilinda tena.

Maana kirusi cha ukimwi kimsingi ni ka taarifa fulani kauzushi na kauongo (wrong code is a Virus to the system) kanakouambia mwili na seli zake kwamba mambo ya kujilinda sio issue. Kuwabania wadudu wengine kuishi sio vizuri we achia tu🙄. Ndo mtu anapata ukimwi.

Dawa ya taarifa ya uongo wrong code/virus ni kupata taarifa ya ukweli true Code from cactus in this case maybe. Si mna akili tafuneni wenyewe
 
Habari wanaJF, mim ni kijana niliyekuwa ninajichunga na kuijari sana afya yangu kiasi cha kuwa na mabox ya vipimo vya H.I.V rapid test ghetto, ikiwa kama nimejichanganya bas nawahi dawa za PrEP,

Dawa za PrEP nimemeza round mbili yaani 2017, 2020 baada ya kucheza rough.

nilikuwa napima maambukizi na mwenza wangu mara kwa mara, Ivi sasa mwenza wangu anamalizia masomo ili mwakani July tuanze kuishi pamoja. sasa mwez Agosti mwaka huu nimekutana na mwanamke ambae tunameet na kusekx na uwa tunacheki afya sasa mwez huo nikapuuza kwakuwa tulicheki afya mwez May nikamla then maisha yakaendelea,

Mwez Octoba juzi tu nikajaribu kupima peke yangu ghetto nikakutana na mistari miwili CONTROL na 1, nilipima zaid ya mara tano apo apo gheto inasoma mistari miwili. Dah pressure ikawa kubwa.

Nikaenda Hospital napo inaonesha nipo POSITIVE, wakanianzishia dawa za ARV's adi sasa ninamaliza wiki tangu nianze dozi za ARV's. next wiki wananianzishia na dozi ya miezi sita ya Anti-T.B...

Juzi nipo YouTube nakuta kuna shuhuda nyingi sana kwamba kuna Mtaalamu anaponesha ili janga from POSITIVE to NEGATIVE anaitwa TR. MSIGWA, jaman waungwana kuna yeyote mwenye hakika na ili jambo ata ndugu yake alipata kupona kwa uyu docta maana kichwa kinawaka saiz sielewi, nikapata mawasiliano yake akaniambia dozi ni shilling 280k ya siku 45 inaitwa (4A9).

Wajameni ivi ili suala linaukweli dawa iyo ya Asili inasaidia kwa yeyote aliyawahi pata experience hii ata kwa ndugu yake kuhusu uyu mtaalamu TR. MSIGWA na dawa yake ya 4A9 maana ninawiki tu tangu nianze kumeza ARV's lakin naihis hali ya kuzichoka tayar. .

nawasilisha:
Ngono ni underated tu. Hakuna chochote cha ziada zaidi ya athari uliyo ipata na upotezaji wa fedha zako.

Tuendelee kupiga kazi.
 
Hakuna tangazo ila ninawasiwasi na pesa yangu maana mzungu alishasema hakuna dawa itakayokurudisha kuwa Negative tena. nipo mkoani nawaza kuagiza maana matapeli ni wengi. Ninahamu na kuicheza hii kamali lakin ninamashaka.
Kuna jamaa huwa anatibu na kuponyesha kabisaaa yeye yupo Tanga maeneo ya Lushoto lakini hapa Dar ana ndugu yake lakini changamoto ipo kwenye kumpata maana anaishi Kurutini ni Ukonga ndani ndani kwa Wakurya wafuga Kuku. Pole sana Mkuu
 
Mkuu unapona kabisa na ata nikipima baada ya mwaka au miaka haisomi kitu. Kuna yeyote unayemfahamu aliyepona kwa muda mref still ni Negative
 
Kuna mmoja alitoa ushuhuda mahali. akisema alipata hizo herbs kwa mganga/mtaalam fulani ambaye hakumtaja jina. alisema baada ya kutumia izo herbs vipimo vilionesha hana tena hiv. ila baada ya muda fulani kupita alipima tena na kukuta bado alikuwa ve+.

kwaiyo angalia kuna matapeli wapo kimkakati kutafuna kidogo ulichonacho kwa mgongo wa kukutibu. kwa ushauri ungekubali tu maji yameshamwagika endelea na dozi na kufuata masharti unayopewa utakuwa sawa tu. maisha mengine yaendelee.
Wasiwasi wangu mim ndio upo apo, isije ikawa dawa zake za asili zinafanya kazi ya kuificha damu kwenye kipimo isiDetect ikatokea mstari nmoja alaf baada ya muda ikarudi kwenye hali ya Positive
 
Lipia tangazo, inaonekana siku nyingi toka 2018 ni mwanachama wa ARVs, umekuja kumtangazia huyo mwamba hizo dawa...

View attachment 2802365
Kuna jamaa huwa anatibu na kuponyesha kabisaaa yeye yupo Tanga maeneo ya Lushoto lakini hapa Dar ana ndugu yake lakini changamoto ipo kwenye kumpata maana anaishi Kurutini ni Ukonga ndani ndani kwa Wakurya wafuga Kuku. Pole sana Mkuu
Wew usituvuruge wew msambaa anapiga nyanga anaweza wapi kucheza na gonjwa kama ile tuachee yaani msambaa na vikofia vyao vya uzii [emoji16][emoji854] alafu akae porini huu ugonjwa ukipata dawa umetusua [emoji120] bongo bado mangombe kibao ndio mana babu wa roliondo alipiga mihela [emoji16][emoji16]
 
Je ulipata dalili zozote ukaamua kupima? Au uliona ucheki tu.
Hapana sikupata dalili zozote zile ni vile sabab nilikuwa nimekaa tu alone ghetto nikaona nijipime maana vipimo ninavyo vingi ndio nikakutana na ilo dude. Dah ndani ya wiki nimepungua kilo6.
 
Kwa sisi tunaoangalia tabia za mimea kuhusianisha na dawa (wagangawaganga) cactus inasound kama inaweza kuwa dawa[emoji848]

Si unaona vyenye ilishagundua kwa mageuko ya miaka na miaka namna ya kujilinda na wanyama na wadudu. Huwa hailiwi ile kizembe.

Basi kuna uwezekano inaijua Code ya ulinzi binafsi na ukiinywa inaweza kuufundisha mwili kujilinda tena.

Maana kirusi cha ukimwi kimsingi ni ka taarifa fulani kauzushi na kauongo (wrong code is a Virus to the system) kanakouambia mwili na seli zake kwamba mambo ya kujilinda sio issue. Kuwabania wadudu wengine kuishi sio vizuri we achia tu[emoji849]. Ndo mtu anapata ukimwi.

Dawa ya taarifa ya uongo wrong code/virus ni kupata taarifa ya ukweli true Code from cactus in this case maybe. Si mna akili tafuneni wenyewe
Huu ni utaalamu wa wataalamu, sio rahisi mim na jamii inayonizunguka kulifahamu ili
 
Back
Top Bottom