Habari wanaJF, mim ni kijana niliyekuwa ninajichunga na kuijari sana afya yangu kiasi cha kuwa na mabox ya vipimo vya H.I.V rapid test ghetto, ikiwa kama nimejichanganya bas nawahi dawa za PrEP,
Dawa za PrEP nimemeza round mbili yaani 2017, 2020 baada ya kucheza rough.
nilikuwa napima maambukizi na mwenza wangu mara kwa mara, Ivi sasa mwenza wangu anamalizia masomo ili mwakani July tuanze kuishi pamoja. sasa mwez Agosti mwaka huu nimekutana na mwanamke ambae tunameet na kusekx na uwa tunacheki afya sasa mwez huo nikapuuza kwakuwa tulicheki afya mwez May nikamla then maisha yakaendelea,
Mwez Octoba juzi tu nikajaribu kupima peke yangu ghetto nikakutana na mistari miwili CONTROL na 1, nilipima zaid ya mara tano apo apo gheto inasoma mistari miwili. Dah pressure ikawa kubwa.
Nikaenda Hospital napo inaonesha nipo POSITIVE, wakanianzishia dawa za ARV's adi sasa ninamaliza wiki tangu nianze dozi za ARV's. next wiki wananianzishia na dozi ya miezi sita ya Anti-T.B...
Juzi nipo YouTube nakuta kuna shuhuda nyingi sana kwamba kuna Mtaalamu anaponesha ili janga from POSITIVE to NEGATIVE anaitwa TR. MSIGWA, jaman waungwana kuna yeyote mwenye hakika na ili jambo ata ndugu yake alipata kupona kwa uyu docta maana kichwa kinawaka saiz sielewi, nikapata mawasiliano yake akaniambia dozi ni shilling 280k ya siku 45 inaitwa (4A9).
Wajameni ivi ili suala linaukweli dawa iyo ya Asili inasaidia kwa yeyote aliyawahi pata experience hii ata kwa ndugu yake kuhusu uyu mtaalamu TR. MSIGWA na dawa yake ya 4A9 maana ninawiki tu tangu nianze kumeza ARV's lakin naihis hali ya kuzichoka tayar. .
nawasilisha: