Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

😂😂😂😂 kwani corona inakaa milele mkuu?

Mkuu kumbuka sasa hivi vilio vyote unavyoviona humu, corona haijamaliza hata mwezi hapa nchini na wala hatujaingia lockdown. Na ukweli ni kwamba, hata dawa ya corona ipatikane leo, itachukua si chini ya mwaka kwa hali kuanza kurudi kama ilivyokua mwanzo. Sasa niambie ni wafanyabiashara wangapi wanaweza kujiendesha kwa kipindi hicho bila income yoyote?
 
Covid 19 amekuwa hatari kuliko hatari yoyote duniani kwa sasa, wanaosema hili nalo litapita ni kweli lakini litaacha madonda makubwa na makovu yake huenda watu wakafa kwa sonono na kiharusi.

Huko bank ndio sijui na vibanda vyetu watapiga minada au itakuwaje, manake kuna wenzangu waliamua kufanya nyumba zao bond, dadeq!! Nadhani 2020 na 2021 itakuwa miaka migumu mno, sio kwa mjasiriamali tu hata mwajiriwa.
 
Shogangu alikuwa anategemea Hotel kuuza kuku wake wa nyama.
Sasa wiki ya pili hakuna biashara kuku wameshakula faida na kiasi cha mtaji alichofanya ni kuwachinja baadhi kuwaweka kwenye friza wengine amewajza na mabarafu kwenye madeli anatembea nao kwenye gari ikitokea zali njiani kakuta kibanda vha chips anauza.
Eee Mungu tunaomba toba na rehema, wewe ni Mungu unaerehemu, ni Mungu unaeponya, ni Mungu unaesamehe. Samehe Baba, ponya Baba na uturehemu pale tulipokwenda kinyume na mapenzi yako, Baba tunaomba utuvushe kwenye janga hili, tunajua kuna magonjwa mengi yanayochukua uhai wa binadamu lakini katika hili tumeshindwa Baba, dunia imejaa hofu na woga, dunia inaomboleza, hatujui mwisho wetu utakuwaje, Mungu tunaomba maisha yetu yarudi kama tulivyokuwa tukiishi siku zote, tumekutenda dhambi lakini Baba kumbuka rehema na uondoe ghadhabu juu ya nchi, watu wanaangamia kwa njaa, maisha magumu kwa kuwa hakuna kazi, watoto wanatamani kwenda shule lkn hawewezi tena, kumbuka rehema sawa sawa na neno lako kutoka Habakuki 3:1-2..Amen!
 
Well hii thread ni kwa ajili ya wote tuliaoathiriwa kiuchumi directly na corona. Najua kila mmoja atakuwa ameathirika kwa level yake lakini nawaongelea wale waliopigwa pigo takatifu. Mfano anayefuga kuku wa kizungu atapeleka wapi na alikuwa anategemea watu wa catering kwenye mashughuli, watu wa catering na mapambo jamani eeee ndo hivo tena tupige goti tu naimani Jehovah adinai atatusikia.

Kuna wale wanaofanya biashara za importation na exportation jamani poleni sana wenzangu hiki kilio chetu sote.

Hotels, wafanyakazi na wajasi wnaotegemea watalii.

Wamiliki wa mashule jamani mbaya zaidi kipato hakuna lakini lazima ulipe mikopo ya bank na ulipie fixed costs.

Wauza uji mihogo n. K mashuleni poleni sana.

Sasa usiombe corona ikuathiri kwa kiasi kikubwa na huku una mkopo sijui bank sijui microfinance haloo hao watu wanajifanya kama vile hakuna kinachoendelea wao wanataka rejesho tu ilihali mikopo wamesitisha na pengine hata wao mishahara wamepunguziwa kwa kiasi fulani ila sasa kwa kupiga simu na kudai hao balaaa.

Kama mimi mkurugenzi na muanzilishi wa kampuni ninalia lia njaa fikiria wale wa chini yangu hali ikoje?

Shughuli za uzalishaji hakuna lakini fixed costs kama hela ya pango na ulinzi lazima nilipie natoa wapi mimi hizo ilhali sizalishi?

Binafsi nimefunga ofisi nimefunga na nyumba nimerudi kwa bi mkubwa vijana wa sasa wanasema kurudisha jezi eee ndo nisharudisha jezi hivo.

Na hii ni biashara yangu changa sana niliyoipambania usiku na mchana isimame. Ninmeipambania haswa wanaojua nini nachofanya humu na tuna mawasiliano ya karibu wanaelewa.

Lakini corona imeipenda zaidi.

Ooo kuna watu watakuja na sera zao hapa huna saving sijui akiba uncertainties bla bla nyie ndugu kama ninavyosema kujiajiri ni kugumu sana hasa kukuza biashara jamani ukisema utoe laki uweke akiba unawaza hii laki si nikinunua kitendea kazi fulani kitasaidia mauzo yaongezeke? Basi unachukua ile hela unaongeza vitendeo kazi.

Wajasiriamali na wafanyabiashara mliokuwa kwenye game mda mrefu hongereni sana na SHIKAMOOOOONI maana najua mmevuka vizingiti vingi.

Wale jirani zangu jamani nishatoka kijijini nimerudi mjini kwenye ugali wa bure mnaweza kuja tu kunisalimia.
Kufa kufaana Mimi nakusanya saa hizi raw material naweka store after Corona kama nitavuka salama tatengeneza margin profit.Japo project zingine zimesimama sababu ya corona
 
Poleni aisee. Kuna nchi nyengine kama unadaiwa deni lako linastopishwa mpaka lockdown iishe.riba haiongezwi. Hata kama huna kazi kuna hela unalipwa. Wafanyakazi wa private sector serikali inawalipa mshahara wao asilimia 80. Asilimia 20 unalipwa na muajiri

Nchi gani hiyo?
 
Hv anayeenda kununua nyapu alafu aende gest kuinyandua .
Nahisi akili yak itakuwa haipo sawa kwa kipind hiki
Hata kwenye dhiki ya namna gani uchakataji papuchi uko palepale tu. Labda kama wewe mwenyewe utasitisha zoezi
 
Back
Top Bottom