Nimeamini katika dunia hii hakuna Mwanamke mbaya

Nimeamini katika dunia hii hakuna Mwanamke mbaya

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Mwaka juzi kuna mwanamke ambaye tulikutana naye kwenye sherehe, Mwanamke huyo aliniomba namba zangu za simu nilimpa. Tukawa tuna chat naye kawaida tu.

Siku moja tu akaniambia ananipenda. Nikamuambia nitamjibu. Muda ambao nilikaa kimya bila kuongea naye nilikuwa na fikiria na kujaribu kumpa nafasi katika moyo wangu ila kiukweli nilikuwa sina hisia kabisa kwake,

Na sababu kubwa ilikuwa sura yake nilikuwa naona ana sura mbaya kinoma na pia alikuwa yupo kishamba zaidi yaani alikuwa havai kama wanawake wa kisasa mivalio yake yeye alikuwa anavaa kama hawa mama zetu wa zamani tu vitenge na kanzu ndefu za ajabu ajabu.

Hiyo ikawa sababu ya mimi kumpiga chini na kublock namba yake whatsApp na na kwenye simu number
Nikampotezea kabisa.

Sasa jana si nimekutana naye kumbe ameshaolewa na kiukweli kabadirika kinoma demu amekuwa mzuri mpaka natamani tena muda urudi ni mkubalie halafu nimtengeneze zaidi ya huyo jamaa wake.
 
Kuna mmoja nimemkataa pia nishapiga one time lkn.. ako na coloured teeth ..hana jeupe hata moja, na chunusi ni nyingi.ila kaumbika balaa yule akipata mtu amuoshe meno na dawa chunusi ziishe watajigonga wengi sana pale ....me siwezi mfanyia hayo maana badae atasema me sio type yake
 
Mwaka juzi kuna mwanamke ambaye
Tulikutana naye kwenye sherehe
Mwanamke huyo aliniomba namba zangu za simu nilimpa. Tukawa tuna chat naye kawaida tu.
Moyo tulia mjini kuna mali za wenyewe. Utakufa ukijaribu kusogelea mali za watu kaa kwa pattern shwaini.
 
Back
Top Bottom