Nimeamini Kinachopiganiwa Gaza Ni Mafuta Na Gas

Nimeamini Kinachopiganiwa Gaza Ni Mafuta Na Gas

and 100 others

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2023
Posts
3,707
Reaction score
12,367
Shambulio la Israel hivi majuzi pale Gaza mjini Al-Mawasi katika mji wa Khan Younis, imepelekea nitafakari kwamba Israel imedhamiria kuisafisha Gaza yote na kuwaondoa Palestinians wote haijalishi itaua raia wasio na hatia kiasi gani ikiwemo watoto wadogo.

Hapo Al-Mawasi ndani ya Khan-Younis kusini mwa Gaza ndipo IDF iliwaambia wakazi wa Gaza waende hapo kuna humanitarian zone na ni sehemu salama kwao na familia zao mwishoni mwa mwaka 2023.

Eneo hilo la kibinadamu ambalo ukubwa wake ni kim1 upana na km 14 urefu, Israel iliwaambia wakazi milioni 1.8 kukaa kieneo hiko, hata hivyo eneo wakazi walisema eneo hilo ni dogo sana kuweza kutosha watu milioni 1.8 .

Israel iliahidi eneo hilo kama sehemu salama kabisa wakati ikiendelea na operation kupambana na Hamas na kuwatafuta viongozi wa Gaza katika mji wa Khan Younis.

AP24195556938404.jpg


IDF inasema ilishambulia eneo hilo ikilenga viongozi wawili wa Hamas mmoja wapo ni commander wa Hamas Mohamed Deif ambao walikuwa wamejificha miongoni mwa raia, Netanyahu katika kutoa maelezo juu ya shambulio hilo alisema walikuwa na dhumuni la kulenga viongozi hao wa Hamas ambao haijulikani kama wameuawa ama ni wazima.

Inasemekana zilishuka missiles 5 na mabomu 5 kutoka kwenye ndege za IDF, ukitizama tu shimo lililochimbwa na hio milipuko inatisha, unaweza kupata picha damage zone ilikuwa ni mbali kiasi gani na sauti yake tu iliathiri watu kiasi gani ikiwemo vitoto vidogo.

Naweza kusema hili shambulizi ni makusudi kuua raia walio kuwa hapo ili waondoke kwa kuwajaza hofu kwamba eneo hilo si salama tena kama walivyo wahakikishia wananchi wa Gaza mwanzoni na sasa wanawageuka kwa hoja zifuatazo.
  • Kauli ya Netanyahu kusema hana uhakika kama viongozi hao wa Hamas Mohamed Deif na Rafa Salama wamefariki katika shambulio hilo inaashiria IDF walifahamu fika hao jamaa hawapo hapo, hivyo ni makusudi kushambulia raia wasio na hatia.
  • Waliamua kutumia kigezo cha kulenga viongozi wa Hamas ili kufanya shambulizi la kushitukiza na kuua raia, kuna baadhi ya mashambulizi IDF huwa wanafanya wanatoa taarifa kwa raia watashambulia eneo fulani lakini hilo shambulizi jamaa wameshambulia ghafla.
  • Hata kama walikuwa wanalenga viongozi wa Hamas, hawakufahamu diameter of damage iakuwa kiasi gani? hawakufahamu kuna raia? missiles nzito kama zile hawakufahamu ule mlipuko ungelipua na kuua raia kwa umbali upi kutoka target? badala yake wamerusha missile pale pale raia walipokusanyika.
Baada ya hapo kuua watu 90 ambapo nasema inawezekana ni zaidi ya hao, na majeruhi 300 ambao wegine wana hali mbaya sana, Netanyahu akaja kuzungumza kirahisi sana kwamba walikuwa wakilenga viongozi wa Hamas.

Hii ni wazi Israel haihitaji tena wakazi wa Gaza, Israel inataka kuchukua eneo lote hilo, na waaompa ushirikiano ni USA ni nchi za Europe licha ya kufanya maigizo ya kinafiki kwamba wanahuzunishwa sana na kinachoendelea Gaza ili kusudi kuwafool wajinga.

USA na Europe wana support sana tu kinachoendelea Gaza hata hizo missiles ambazo zilitumia JDAM walizorusha hapo Al-Mawasi ni US made, JDAM ni kit inafungwa kwenye haya makombora ambayo sio PGM (precision-guided munitions ) au yanaitwa dumb bomb na kuyabadili kuwa PGM, yaani kombora ambalo unakuta limeshiba tu vilipuzi lakini halina uwezo wa kujiendesha kwenda kupiga sehemu kwa shabaha, unaweza ukalirusha kutoka ghorofani kama free falling body likaporomoka likafika chini likalipua watu, Sasa unapolifunga hio kit ya JDAM linakuwa smart, unakuwa umeli convert kutoka kuwa dumb na kuwa smart , hivyo unaweza kuliendesha kwa mifumo maalumu kama GPS ukalielekeza likaruka kwenda kupiga mahala fulan kwa usahihi mkubwa.

joint-direct-attack-munition-jdam-004.jpg

JDAM bomb.
Israel na kuua raia wote wale utasikia USA wakisema kauli fupi tu "tunalaani kitendo cha Israel kushambulia raia wasio na hatia na tunaomba vita isimame blah... blah... blah" kesho Israel inaua wengine inaendelea hivyo hivyo.

Sasa tutafakari kwa mapana kwanini hizi nchi za Europe na USA wanakuwa wabaridi sana mbele ya Israel? wanachozungumza na wanachotenda/hatua wanazochukua dhidi ya Israel kwa ukatili anaofanya ni tofauti sana na nchi zingine ambazo ziliwahi kushambuliwa na USA na washirika wake kwa sababu ambazo ukilinganisha na ISrael anachofanya, basi NATO ilibidi imuonye Israel mara moja na kikataa avamiwe kijeshi.

Sasa ndipo narudi kwenye lengo kuu la uzi.

Mwaka 1999 kampuni ya kimataifa ya gas na mafuta kwa jina la BG Group kutoka Uingereza iligundua kuna gas na mafuta kwa kiasi kikubwa sana pale Gaza marine, gas kwa kiasi cha 1 trillion cubic feet (28.32 km3) katika eneo la Gaza lililopo majini katika bahari ya Mediterranean , kisheria eneo hilo lijulikanalo kama Gaza marine ni sehemu ya Gaza kisheria na ipo chini ya Palestine kwa mujibu wa makubaliano ya Oslo Accords, eneo hilo lipo upande wa Palestine.

Map1-1024x640-750x469.png

Makubaliano ya Oslo yalikuwa ya aina mbili Oslo I na Oslo II.
Makubaliano ya Oslo I yalifanyika 1993 Washington DC nchini USA na Oslo II 1995 pale Egypt Taba 24 Sept 1995, siku nne baadae tarehe 28 Sept 1995 makubaliano yaliendelea kufanyika na kushuhudiwa na Bill Clinton aliyekuwa rais wa US wakati huo, wawakilishi kutoka Russia, Egypt, Jordan, Norway, na European Union pale USA Washington, D.C. waziri mkuu wa Israel kipindi hiko Yitzhak Rabin na kiongozi wa kisiasa Palestina Yasser Arafat wakati huo ndio wali sign makubaliano hayo.

Sasa ndipo uone, makubaliano ya Oslo walikubaliana eneo hilo la Gaza marine ni eneo la Palestine halafu mwaka 1999 kuelekea 2000 gas inagunduliwa Gaza marine 🤣.

Kuna eneo linaitwa Levant ambalo linatokea mto Jordan hadi bahari ya Mediterranean, eneo hilo linajumuisha maeneo ya West Bank, Gaza Strip, Lebanon, Cyprus, na Syria. Katika eneo hili kuna utajiri mkubwa wa gas na ndipo Gaza marine ilipo. Gaza marine inapatikana umbali wa km 30 hivi kutoka kwenye coast ya Gaza
Katika eneo hilo gas inapatikana umbali wa mita 610 chini kabisa ya maji.
Levant_Basin_Province-479x509.jpg


Baada ya makubaliano ya Oslo II, mamlaka ya Palestine ilipewa haki na uhuru wa kuweza kufanya maendeleo na kutumia sehemu yake ya maji itakavyo, mamlaka ya Palestine au Palestine Authority kifupi tuseme PA, PA iliamua kutumia uhuru wake na haki kuweza kufanya shughuli za kimaendeleo katika eneo la Gaza walilokubaliana na Israel kwenye Oslo accords.

Miaka minne baadae 1999, PA waliamua kuingia makubaliano na kampuni ya BG kuweza kufanya tafiti katika eneo hilo la maji kwa makubaliano ya kwamba wakikuta kuna mali eneo lolote la Palestine, basi BG watapewa stake ya mali hio, watapewa ruhusa kusimika mitambo yao ya uchimbaji na kujenga miundombinu kwa ajili ya uzalishaji wa gas kwa muda wa miaka 25.

BG wakaona ni good deal wakaingia mzigoni kuanza kufanya tafiti wapi kunaweza kuwa na gas au mafuta, ndipo hapo wanakuta kuna mzigo wa kutosha wenye thamani ya mabilioni ya dola, utajiri wa kufuru upo chini ya ardhi ya Palestine, toka hapo Israel ilianza choko choko ili jambo hilo lisifanikiwe.

Mwaka 2002 PA waliamua kutoa ruhusa rasmi kwa kukubali mapendekezo ya BG company kuanza kujenga mitambo na bomba la nishati hio kutoka Gaza marine hadi Gaza strip, Israel ikainglia kati na kusema hilo halitowezekana inabidi bomba hilo la nishati lielekee katka bandari ya Israel na pia Palestine inapaswa kuwauizia Israel bei ya chini sana ya nishati chini ya bei ya kawaida.

Mwaka 2007 baada ya Hamas kushinda uchaguzi, Israel iliamua kutumia nguvu kwa kutumia jeshi la majini kuzuia uendelezwaji wa ujenzi wa mradi huo unaofanywa na BG company, kampuni ya Israel ya gas iliwaahidi kuwapa mikataba ya kazi kampuni ya BG endapo tu watachelewesha mradi huo wa Gaza marine.

waalitumia jeshi kuzuia ujenzi usiendelee na wanaihonga kampuni ya BG iachane na hio kazi.

Mnamo Desemba 2008, kinyume kabisa na sheria za kimataifa, Israeli ilitangaza mamlaka juu ya eneo la Gaza Marine, na BG ilifunga ofisi zake. Royal Dutch Shell ilinunua maslahi ya BG katika Gaza marine kwa $52 milions mwaka wa 2016, hata hivyo baadae 2018 Royal dutch waliacha PA watafute muwekezaji mwingine.

Inasemekana kuna gas na mafuta mengi katika eneo la Palestine west bank na Gaza ambapo inaweza kupelekea kuleta maendeleo makubwa kwa taifa la Palestine.

Hata hivyo Israel iliendelea kuwazuia Wapalestina wasiendeleze na kunufaika na maliasili zao, kinyume na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa zinazosimamia nani ana haki ya rasilimali hizo.

Kuna uzi nilandika hapa jamiiforums mwaka 2021 Jan nikielezea kwanini Syria inashambuliwa, nikelezea kuhusu bomba la mafuta la nord stream, nilieleza mambo mengi sana hapa Je, Iran inaweza kugeuza Aircraft Carrier za USA kuwa Shipwreck?

Kiufupi nilieleza US hahitaji Russia kama msambazaji mkubwa wa gas ulaya, Qatar ndiye alikuwa anapewa kipaumbele kupewa kazi hio kupeleka gas pale Ulaya ili kum challenge Russia na kuharibu maslahi yake, Syria ni nchi imekaa kimkakati, imekaa njiani bomba la mafuta linapopaswa kupita kutoka Qatar, Assad akakataa pendekezo hilo la kupitisha bomba hilo la mafuta kuelekea Ulaya kutokea Qatar, ndipo mkong'oto ukaanza kumshukia, kwa sababu Assad alisimama kumtetea rafiki yake na mshirika wake Russia kwa kutetea maslahi yake, Russia ilipoona jamaa yake anatandikwa ikateremka kumkingia kifua Assad, pasipo Russia Assad asinge kuwepo na bomba la mafuta lingepita kuelekea Ulaya.

Dunia inakwenda kimaslahi zaidi, kila wanachofanya ni maslahi, ugaidi, haki za binadamu na blah! blah! ni sababu zinazotumika kutimiza malego ya watu yenye maslahi yao.



Soma kwa makini. hapa ndipo penyewe..

Katika vita kati ya Ulraine na Russia iliyopelekea hali mbaya ya upatikanaji wa nishati barani ulaya kutokana na hali ya vita kati ya Russia na Ukraine, uharibifu wa bomba la nord stream na vikwazo juu ya Russia, imepelekea hali mbaya ya kiuchumi na nishati barani ulaya kote.

Tukumbuke kwamba US katika juhudi zake za kuitaka Qatar kupeleka bomba Ulaya la gas kupitia Syria ilishindikana.
Sasa US na Ulaya wakaona sehemu pekee ya kupeleka gas kwenda Ulaya ni kutokea hilo eneo la Levant ambapo kuna gas ya kutosha na ndipo ilipo Gaza Marine, ukafanyika mkutano ambapo walikutana viongozi mbali mbali kutoka Israeli, U.S., Egypt, Jordan na Palestine kwa ajili ya kujadiliana jambo hilo.

Ndipo US na Egypt wakampa jukumu Israel kushughulika na suala hilo kwamba gas kutoka Gaza marine inawafikia Ulaya, Netanyahu baada ya kuchaguliwa tena December 2022 ndipo akapewa majukumu kuhakikisha suala hlo linawezekana.

Ndipo Israel 2023 June , Netanyahu akasema wanatoa kibali kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa mradi wa gas pale Gaza marine.

Hebu tafakari mali ni ya kwako, halafu kuna mlevi mmoja anakuja kusema kwamba yeye ndiye anakuruhusu uitumie au hapana na ufuate masharti yake.
Screenshot 2024-07-16 145516.png


Kiongozi wa Hamas Ismail Rudwan akasema "Tunathibitisha tena kwamba watu wetu huko Gaza wana haki ya mali zao za asili." (Juni 18)

Kiongozi mwingine wa Palestine akasema "Tunasubiri kujua nini hasa Waisraeli wamekubali kwa undani. Hatuwezi kutoa msimamo kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari," .

Sasa hapo ikaw wazi Palestine hawajapendezwa na makubaliano ya Israel.

Cha ajabu ni kwamba miezi miwili nyuma kabla ya Oct 7, Jeshi la marekani walianza kutengeneza kambi ya jeshi, miles 20 kutoka Gaza ilipo kwenye jangwa la Negev nchini Israel, walijenga kambi ya jeshi kwa thamani ya 35.8 million USD, huku Pentagon ikdai ni eneo la radar kwa ajili ya kuangalia makombora inayoshambuliwa Israel.

Uhalisia ni kwamba Kambi hiyo ni sehemu ya uwepo wa "siri" wa kijeshi wa jeshi la Marekani huko Israeli.


Tangu Oktoba 7, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameweka wazi kuwa Israel inakusudia kuwaua Wapalestina wengi iwezekanavyo ili kuwashinikiza wengine kuondoka Ukanda wa Gaza na kuhamia Sinai nchini Misri. Netanyahu amekuwa na msimamo mkali wa kukataa kuamuru kusitishwa kwa mapigano ili kuruhusu misaada kukomesha mauaji ya kimbari yanayotekelezwa huko Gaza.

Ndio maana Netanyahu ana kiburi na hasikilizi mtu, wakubwa wamekwisha muambia asafishe Gaza yote, Egypt naye ni mnafiki ameamua kuwauza Palestine kwa maslahi, Jordan pia n.k, Palestine wanapambana kivyao ni Mungu tu na mataifa kama Lebanon, Iran n.k wanawasaidia.

Suala Oct 7 siungi mkono walichofanya Hamas, lakini walitengenezewa mazingira wafanye tukio lile.

Gazakids.jpg


Hivyo wale wazee wa kukurupuka nadhani nimewafumbua macho kwa kinachoendelea Gaza, hakuna suala la udini, hakuna ukabila, shida ni mali iliyopo pale Gaza na vita inayoendelea huko Russia na Ukraine.

Trump atakapoingia madarakani vita ya Gaza itakwisha, Russia itaendelea na biashara yake ya kuuza gas Ulaya, unaweza usiamini lakini ndivyo ilivyo, ndio maana jamaa wameanza kumlenga jemedari Trump afe, hata US military complex industry US hawataki Trump aendelee kupumua, kina Lockheed, Northrop, Boeing n.k kwa ujumla mashirika yanayojihusisha na biashara ya silaha hawataki kusikia kuna kiumbe anaiwa Trump.

Biashara ya silaha ina utajiri mwingi.

Tukutane 2025.
 
Ikiwa Insu ni Mafuta ama Gesi IDF ingelikuja kuteka Zanzibar ama Tanzania kwa Raia ambao hawajui hata kurusha jiwe.
Acha kukurupuka kuongea upuuzi usioujua, uzi wenyewe hujasoma, kama hujasoma usilete makalio yako mbele kuja ku comment, nimeelezea hapo sehemu inaitwa Gaza Marine ambayo ni rahisi kupeleka gas Ulaya, nimeeleza sehemu hio inaitwa Levant basin.

Sasa gas kutoka Tanzania itafikaje Ulaya kwa njia ya bomba? tumia akili basi mzee usiwe unakurupuka.

Nimeelezea kwanini gas kutoka Levant inahitajika kipindi hiki ambacho Russia gas yake haifiki Ulaya na Ulaya wanahitaji gas.
 
Acha kukurupuka kuongea upuuzi usioujua, uzi wenyewe hujasoma, kama hujasoma usilete makalio yako mbele kuja ku comment, nimeelezea hapo sehemu inaitwa Gaza Marine ambayo ni rahisi kupeleka gas Ulaya, nimeeleza sehemu hio inaitwa Levant basin.

Sasa gas kutoka Tanzania itafikaje Ulaya kwa njia ya bomba? tumia akili basi mzee usiwe unakurupuka.

Nimeelezea kwanini gas kutoka Levant inahitajika kipindi hiki ambacho Russia gas yake haifiki Ulaya na Ulaya wanahitaji gas.
Ameandika kauli ya kijinga kabisa! Na umemjibu vyema.
 
Ameandika kauli ya kijinga kabisa! Na umemjibu vyema.
Haya ndio majitu nisiyo yataka hoja halina linataka comment yake iwe ya kwanza kuuliza ujinga tu.
US yenyewe haipeleki gas Ulaya kwa njia ya bomba na wanachimba gas, gharama ya ujenzi wa hilo bomba na usimamizi itakuwa hasara kupeleka hadi Ulaya, halafu mtu anakuja kukuambia kwanini wasije Tanzania kuchukua gas, yaani wajenge bomba la gas kutoka Tanzania hadi Ulaya?
 
Ugunduzi wa nishati katika Mediterania ya Mashariki unabadilisha mienendo ya kikanda katika Bonde hilo. Washiriki wakuu - hasa Cyprus, Misri na Israel - wanachukua hatua kufikia uhuru wa nishati na wanatafuta fursa za mauzo ya nje. EU, ambayo ina nia ya kupunguza utegemezi wake wa nishati kwa Urusi, inaweza kuwa mteja katika siku zijazo.

Usije kuuliza kwanini Egypt anawaangalia tu Palestinians Gaza wanavyopigwa, ni kwa sababu na yeye ni mnufaika mkubwa wa biashara ya gas, eneo la levant ndio mahala Ulaya inapatazama zaidi kama chanzo cha kupata gas.

Hivyo Egypt na Israel lao ni moja.
 
Haya ndio majitu nisiyo yataka hoja halina linataka comment yake iwe ya kwanza kuuliza ujinga tu.
US yenyewe haipeleki gas Ulaya kwa njia ya bomba na wanachimba gas, gharama ya ujenzi wa hilo bomba na usimamizi itakuwa hasara kupeleka hadi Ulaya, halafu mtu anakuja kukuambia kwanini wasije Tanzania kuchukua gas, yaani wajenge bomba la gas kutoka Tanzania hadi Ulaya?
Hata ingelipeleka kwa njia ya meli bado gharama ni kubwa sana.

Ila ndiyo kawaida ya watanzania; anaandika ujinga ila mwenyewe anaona ameandika cha maana.

Si ajabu wakaja wenzake wakampa likes na kumuunga mkono halafu kwa pamoja wakashangalia.
 
Hata ingelipeleka kwa njia ya meli bado gharama ni kubwa sana.

Ila ndiyo kawaida ya watanzania; anaandika ujinga ila mwenyewe anaona ameandika cha maana.

Si ajabu wakaja wenzake wakampa likes na kumuunga mkono halafu kwa pamoja wakashangalia.
Kwa sababu ni weupe, ndio maana nimeelezea kwa kirefu, kwa sababu wengi huu mgogoro hawaujui, unaandika hoja mtu anakuita mvaa kobazi, mvaa dera, kichwani mweupe, haelewi dunia inaendaje ye kashiba wali na maharagwe anaona aandike anachoona.
 
Hata wakiachia mateka unadhani vita itaisha?
Kama Israel ingekuwa inataka mateka, isingeshambulia kiasi kile, hata wao walijua kwa haya mashambulizi yetu hata mateka watakuwa wanakufa huko walipo...

Na kweli Hamas walikuja kukiri kwamba baadhi ya mateka wameuawa na mashambulizi ya anga ya Israel, ukikaa chini ukatafakari kwa akiliutagundua ni nini kinatafutwa pale Gaza.

Israel haina umuhimu na hao mateka inatumika kama sababu.
 
Aliyefaulu kusoma hili gazeti au kitabu cha mleta mada atupatie mukhtasari, kwanza atujuze kama ni mvaa kobazi ili nijue namjibuje.
Yaani wavaa kobazi akili mlinyimwa, mshambulie na kuua watoto wa Wayahudi kisha mchukue wengine mateka halafu mkipigwa kibano mnaanza kuandika andika nyuzi ndefu sijui mafuta sijui pumba gani.
Na mtapigwa tu, kama kweli pana mafuta hapo, mliacha kuyatumia mkaona muwekeze kwenye ugaidi wa dini yenu.
 
Ugunduzi wa nishati katika Mediterania ya Mashariki unabadilisha mienendo ya kikanda katika Bonde hilo. Washiriki wakuu - hasa Cyprus, Misri na Israel - wanachukua hatua kufikia uhuru wa nishati na wanatafuta fursa za mauzo ya nje. EU, ambayo ina nia ya kupunguza utegemezi wake wa nishati kwa Urusi, inaweza kuwa mteja katika siku zijazo.

Usije kuuliza kwanini Egypt anawaangalia tu Palestinians Gaza wanavyopigwa, ni kwa sababu na yeye ni mnufaika mkubwa wa biashara ya gas, eneo la levant ndio mahala Ulaya inapatazama zaidi kama chanzo cha kupata gas.

Hivyo Egypt na Israel lao ni moja.
Kama ikiwa Israel anamepatiwa nafasi hii, ushirikiano baina yake na Urusi itakuwaje?

Kama Urusi iliingia Syria ili kunusuru uchumi wake, na hata kwa sasa bado ananufaika pakubwa kwa kuwa nchi za Ulaya zinanunua kwa wingi gesi ya Urusi kupitia kwa India.

Urusi tunamuweka kwenye nafasi gani katika hili? Uhusiano wake na Israel utakuwaje?
 
Aliyefaulu kusoma hili gazeti au kitabu cha mleta mada atupatie mukhtasari, kwanza atujuze kama ni mvaa kobazi ili nijue namjibuje.
Yaani wavaa kobazi akili mlinyimwa, mshambulie na kuua watoto wa Wayahudi kisha mchukue wengine mateka halafu mkipigwa kibano mnaanza kuandika andika nyuzi ndefu sijui mafuta sijui pumba gani.
Na mtapigwa tu, kama kweli pana mafuta hapo, mliacha kuyatumia mkaona muwekeze kwenye ugaidi wa dini yenu.
Wewe ndiye chizi mwingine hapo unaandika taarabu, uzi hujasoma , aisee sihitaji wachangiaji, na sio kwamba ukisoma mi nitaingiza pesa hii sio youtube.

Hata hoja zangu huwezi kujibu. relax mzee.
Huna unachokijua kuhusu mambo yanayoendelea duniani, sana sana unajua kusema mvaa kobazi..
 
Kama Israel ingekuwa inataka mateka, isingeshambulia kiasi kile, hata wao walijua kwa haya mashambulizi yetu hata mateka watakuwa wanakufa huko walipo...

Na kweli Hamas walikuja kukiri kwamba baadhi ya mateka wameuawa na mashambulizi ya anga ya Israel, ukikaa chini ukatafakari kwa akiliutagundua ni nini kinatafutwa pale Gaza.

Israel haina umuhimu na hao mateka inatumika kama sababu.
Kwanini Hamas waliwashambulia Israel wakiwa kwenye sherehe zao .. watajuta sana na bado
 
Wewe ndiye chizi mwingine hapo unaandika taarabu, uzi hujasoma , aisee sihitaji wachangiaji, na sio kwamba ukisoma mi nitaingiza pesa hii sio youtube.

Hata hoja zangu huwezi kujibu. relax mzee.
Huna unachokijua kuhusu mambo yanayoendelea duniani, sana sana unajua kusema mvaa kobazi..
Huyo ni shoga na chizi hapo hapo huwa hajitambui kabisa yeye kazi yake kutafuta habari Israel kapiga sijui Iran imepigwa ana mapenzi na Israeli sababu ya ushoga wake.

Nikirudi kwenye thread, ni kweli wamegundua Gaza kuna mafuta na gas nyingi sana, kwa hio US na Israel wanataka kuwaondoa wa Palestine hapo ili Israel achukue hio Oil na Gas.

Israel anawambia raia wa Gaza nendeni sehemu flani kuna usalama huko, wakienda Israel anafanya genocide afu anasema target ilikuwa kuna fununu kamanda wa Hamasi alikuwa pale, yote ni uwongo mtupu.
 
Back
Top Bottom