Nimeamini mjini akili tu

Nimeamini mjini akili tu

Tuliosoma Cuba tunajua ni haramu hiyo, kama ni legal mbona utetezi mwingi wenye wasiwasi ndani yake?
Sio ishu haramu kabisaa
Ni halali
Asee nalipa kodi tra
Nina leseni
Nina ofisi
Tatizo lenu mnaamini kwamba kila ishu ya hela nyingi lazma iwe haramu...sio kabisa.
Manyanza waambie wenzako
 
Na wewe uibiwe nini kwanza jaman?🤣🤣🤣
Maana hata cha kuibiwa huna.
Ndo hvyo hela tunapiga sana tu na kodi tinalipa na leseni zipo

Sina cha kuibiwa, ndo maana huwa hamuolewagi, mnafuata wanaume wa watu, na kufikiro mna uzuri, kumbe wachafu tu na adabu hamna, Mtazeeka mkitembea na wanaume wa watu.
 
Kwa hiyo ukimdaka mjinga mmoja anakulipa mshahara uliokuwa unapata kwa miezi sita kwa mara moja.
Hatuwezi jua labda huyo mzee alikufundisha udaktari kitengo cha upasuaji
 
Ngoja niupige pige kwanza maisha yabadilike ili hata nikikwambia uamini. We ntakwambia ila sio leo...
Daahhh ...udugu wangu mpk ujenge ghorofa sasa
[emoji3526][emoji3526][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Beauty with brain. Safi sana.! Kuna madume mengi huku kelele za bure kumbe maoga kweli kweli[emoji28] ila wewe mwanamke umethubutu.

Ni kweli Watanzania wengi(tafiti zisizo rasmi) ni waoga na hawajiamini kabisa, siyo kwemye shughuli zao za kazi au kujieleza, kote ni tia maji tia maji.
Unamsifia wakati hajakueleza anachofanya? Wewe nawe umekuwa mjinga mwingine.
 
Penye tatizo ama ignorance Kuna hela.

Mfano Kuna mradi mmoja nauwaza unamiliki boda unampa kijana ,Hawa akina mama wanabakia home , wanafua,Wana watoto wananyonyesha,wanacheki series,tamthilia,wanapiga soga wanakuwa wavivu wa kwenda magengeni kufanya maemezi lunch nakuwa na app yangu Kama Uber wanatuma Oda zao nazo asubuhi nanunua Kama nyanya za 300,kitunguu Cha 200,dagaa 1000, mchicha wa 500,

Mafuta ya kula ya 200 nampelekea mafuta wananilipa kwa mwezi ama kila mmama anatoa 250 Mana natafuta eneo ambalo ni congested. Maana ukipata Kama Kaya buku ivi unalaza kitu Kama 200k unamzidi mwenye PhD anayelilia kutoteuliwa u rc pia.


Nyingine unapika chakula unakuwa na mdada unatafuta networks wale wavivu wa kupika ama mabachelor unawapelekea lunch wakiwa maghetoni Mana wapo wasiopenda kutoka kama vile mkiwa loji ndani kwa ndani unaletewa msosi hamshuki chini mana mko na nguo laini,Hawa Kuna service Kama ya 500,

Hiyo ya sokoni kununua mahitaji ni idea nzuri sana, ila sasa uangalie maeneo wanayoishi wenye nazo kidogo. Maana huko kwingineko budget ya matumizi tia maji tia maji.
 
Salama?

Dah kila siku najifunza hapa duniani....NIMEAMINI MJINI NJOO NA AKILI TU ...HATA USIPOBEBA NGUO UKIWA NA AKILI UTAZIPATIA MJINI.

Sasa basi Kuna mzee mmoja niliunganishwa nae anisaidie ishu moja hivi....sasa bwana nikashangaa sana huyu mzee maisha yake yote anaishi hotelini..I mean kwa siku analipia elf 60 hadi 70 za kulala (inaweza kuwa ndogo kwako ila kwangu kubww sana kwa siku) na muda wote anapiga ulabu wa gharama tena akiwa na kampani ya mtu hadi 6 mpaka jogoo anawika. Nikawa najiuliza huyu dingi anashinda hotel anakesha bar pesa anatoa wapi??

Basi binafsi ishu aliyopaswa anisaidie hakunisaidia badala yake akawa ananikaribisha niwajoin mida ya jioni wakiwa wanapata mambo yao. Katika story zake Alisema ameona nina akili sana so nitampatia utajiri so niwe mpole nimsikilize (najua mtabisha kwakuwa mnaniona kilaza sana humu).

Akawa ananituma kumfanyia kazi zake binafsi kwa kunituma sehemu mbalimbali. Nikaamua kuwa mjinga tu kwamba niwe namsikiliza na kufanya kazi zake bila hata malipo.

Sasa akanipatia mchongo flani ...mwanzoni niliuona mgumu sana kwakuwa hadi umu identify mteja sio kazi rahisi . Huu mchongo unatumia ujinga wa watanzania na utapiga hela ndefu tu.

Basi bwana baada ya kama mwezi hivi nikaanza kupata wateja... Yani salary yangu ya miezi 6 wakat nimeajiriwa nkaipata kwa mwezi mmoja. Inshort ule mchongo unafanya kazi na glass ya wine umerelax kabisaa kikubwa uwe na laptop, simu na data. Of course na connection kidogo. Yani mteja mmoja tu kwa mwezi anatosha unaishi kama mkuu wa idara ngazi ya mkoa.

Nikaamini kwamba mjini inatakiwa akili tu nguvu uache kijijini. Watanzania wengi ni wazito, hawajiamini, waoga sana na wavivu kufanya ishu zao hata zile ndogo sana....sasa wachache wajanja wanatumia huo udhaifu kuishi mjini.

Sijutii kumfahamu yule dingi.
Mwisho Ongea na watu vizuri ....unayedhan hana maana anaweza kuwa wa manufaa kwako. Aliyeni connect na huyu dingi ni bolt driver tu baada ya kuniskia naongea kuhusu ishu flan nikiwa mkoa flani kwa mapumziko.
Uzi tayari

Note: mchongo sitautaja kabisa. So msiniulize sana. Hiyo ni password ya maisha.

Kingine sitaki mtu PM. Nimetoa mfano wa maombi ya vyuo tu.... kwamba ukiutumia vizuri ni fursa. Kwani watu wa stationery wanafanya nini? Hadi kuangalia salary slip ya mwalimu wanachaji buku 3 na wapo Town wana hela kwa kutumia ujinga wa watanzania wakiwemo walimu. So jiongeze

Nyie mlioko PM msijisumbue sitajibu.
Fee nachaj kihalali kabisa in USD beibee (najua mnasonya ila ndo hvo tafuta ujinga uutumie kama fursa pia ongea na watu vizuri). Kodi tunalipa na leseni zipo.
Hakuna mchongo wowote hapa zaidi ya "Tuma kwenye namba hii"
 
Mimi nimeeleza uzoefu. Kuwa huwa tukitaka mtapeli mtu tunajihami sana. Tena huwa tunakataa kuwa hatutoi kabisa siri ya ushindi... Na akija mtu tunaweza hata ku mblock ili aje alalamike kuwa hatutaki toa siri. Hii inatufanya tuaminike zaidi ili sasa yule ambaye tuta mset aje aliwe kichwa vizuri
Asee kuna jamaa kaja inbox me hata sijamjibu na sitegemei kumjibu.
Kama ww tapeli usione kila mtu tapeli. Be positive jifunze hata kwa kupita kwenye vistationery tu vya mtaani utapata kitu.
Sasa kama salary slip tu mtu analipa adownlodiwe ndo ishu kubwa.
 
Mimi nimeeleza uzoefu. Kuwa huwa tukitaka mtapeli mtu tunajihami sana. Tena huwa tunakataa kuwa hatutoi kabisa siri ya ushindi... Na akija mtu tunaweza hata ku mblock ili aje alalamike kuwa hatutaki toa siri. Hii inatufanya tuaminike zaidi ili sasa yule ambaye tuta mset aje aliwe kichwa vizuri
Anyways amini vile unaamini.
 
Nakadori mpendwa huna baya, nifungulie code hata kwa uchache. Mchongo eti ni B2B au B2C?
Code siifungui hata mniite majina yote mabaya yaliyoko dunian. Kikubwa I make my living though legal ways ....I don't care backing dogs wanachosema.
Siku zote mbwa anambwekea asiyemfahamu.
 
Back
Top Bottom