Nimeamini wanaume hawaaminiki

Nimeamini wanaume hawaaminiki

Rafiki yangu alinikaribisha kwake akaniambia uhuru ni vema tuwe tunatembeleana nikakwambia nitafanya hivyo nikioa
Nakushauri usipende kwenda kutembelea nyumba za walio olewa tembelea spinsters kama wewe au bachelors huko kwingine acha watu waishi kwa amani
Huwa siendi mara kwa mara, na nikiebda tunakaa kibarazani kama mume wake atakua amerudi wao wanaenda ndani mimi nakua busy na simu.
 
Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
Huko kwenu wale kuku mnaofuga, majike wapo wangapi kwa jogoo mmoja?
 
kumbe kuna watu mna dunia yenu. sasa wewe uliambiwa wapi kuwa wanaokumbatiana na kulishana hawacheat.
binadamu wote ni sawa na afrika ni moja 😆 😆 😆
badilika ,acha utoto
 
Mwanamke mwenye hekima huwa hashangai mumewe akimcheat ndivyo tulivyo haturidhiki na K moja

Mfano mzuri ni aliyekuwa raisi wa Marekani Bill Clinton kwa miaka 2 alikuwa akimcheat mkewe Hillary Clinton kwa kutoka na secretary wake.

Na mkewe Hillary alijua lakini hakwenda mahakamani kudai talaka kwa sababu alijua ndivyo tulivyo mpaka leo ndoa yao inatimiza miaka 49

Uzuri ni kwamba wanaume tunacheat with no emotions ni tamaa tu ndio maana tukishamwaga tamaa zinaisha ila upendo wetu kwa wake zetu unabaki palepale

Men are polygamous by nature
 
Kwahiyo hapo ndio umemaliza research yako kuwa wanaume wote wanacheat,hiyo tabia yako ya kuwa na rafiki mke wa mtu ndio itakugharimu,kwa maisha kama hayo nimewahi kushuhudia mtu kaacha mke na kuhamia kwa rafiki wa mkewe.Usijaribu kushindana na shetani kwa kutumia akili zako mwenyewe,usipoangalia utashtukia tu siku moja mko chumba kimoja na Baba Cathe mmejifungia mlango...
Mama Cathe ni mtu naelewana nae hata mama angu ni rwfiki yake mkubwa
Sema Mumewe ndo anataka kuleta mambo ya kiwaki...
 
Back
Top Bottom