Nimeamini wanaume hawaaminiki

Nimeamini wanaume hawaaminiki

Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
We sema umemtega mzee wa watu yaishe.
 
Kila siku unakuja kwa mke wangu .. kufanya nini !? Unakuja na vinguo vya ajabu ajabu

na nimekugunduwa kwa muda mrefu sana unatamani mapenzi yetu na mke wangu.

Unatamani uchukuwe nafasi ya mke wangu kwa mapenzi ninayomuonesha.. ?

Una upweke mwingi sana ndio maana muda mwingi unajifungia ndani, haukitani na wanaume wengine huko nje hadi uje kwangu kunitega!?

Kwa kifupi umenitega kwa muda mrefu sana na siku ile uchochoroni ni shetani tu alinipitia , siwezi kumsaliti mke wangu maana nina mpenda sana

Ndugu wananchi tuwe makini na hawa wanawake.. walianza kutumia na shetani tangu karne hizo.. tukianzia kwa adam na wengine

Maanguko mengi ya no wanaume huanzia kwa wanawake wanaojihusisha nao!

Tuwe makini

Wanawake ni manipulator wazuri sana! Na mabingwa wa ku flip the script
 
Hayo unayaona yataisha tu muda utaamua!kukumbatiana na mbwembwe kibao huisha mapema tu!!

Uanaume ni kazi ngumu sana sio rahisi hata kama mngepewa nyie uanaume mngefeli tu!!

Kubeba future ya watoto na mama yao ni mzigo wa misumari inayowafanya wengi wasitamani ndoa!!Mali zetu ni pesa iliyopo mfukoni,chakula tunachokula,mavazi na ke ulienae kitandani Kwa wakati husika,the future belongs to women and children's not men!!

Ndio maana sisi me Kila mmoja ana retreat Kwa tabia yake,wengine ulevi,wengine hiyo na mchanganyiko!!

Waliowatulivu ni wale wenye matatizo ya kiafya na kiroho ,lakini rijali kabisa can't settle with one!we were made for that!
Asnte kwa comment hii kaka.
 
Mnajiendekeza!

Hapana, i can i assure you ni kitu natural...kinakuja tu bila hata ku-control...

Lakini ajabu ni kuwa, mwanaume hawezi kuacha mpenda mke labda mke awe na kiburi, dharau na vitu kama hivyo...
 
Sio kuzingua, lazima tukuulize maswali. Hii mada umejaribu kutuchafua wanaume, hivyo lazima tuweke mizani sawa.
Hujawahi kucheat? Hadi unalalamika?
Yule anayekuitaga neighbour ni nani yako au kisa sijawahi kukuuliza? Mfwiiiiiii😂
 
Back
Top Bottom