Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%
Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.
Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.
Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.
Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.
Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'
Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.
Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu
Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.
Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?
Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!
Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
Darasa la somo hili litolewe mara ngapi jamani nyie?
Wataalamu wa masuala ya malovedavi na mahusiano kwa ujumla, hutokeza humu mara kwa mara na kutoa darsa.
Wanakwambia kucheat kwa mwanaume hakumaanishi kumchoka mkewe ama haimaanishi hampendi.
Upendo unaouona anamfanyia mkewe ni upendo halisi na anampenda mkewe hasa.
Kinyume chake ni kwamba ukiona mwanamke anacheat, inamaanisha kapenda na kuvutiwa anakocheat, kwa hiyo mapenzi kwa mume wake hayapo, ama kama anaonesha mapenzi basi ni ya kuigiza.
Moyo wa mwanamke haugawanyiki kwenye kupenda.
Kwa hali hiyo basi, mwanaume anaweza akapenda multiple mamaz na penzi lake likagawika vizuri bila ya shida yoyote, ndiyo maana tunaoa mke zaidi ya mmoja na mapenzi yakastawi.
Mapenzi pamoja na kuhusiana na kupenda lakini pia ni sanaa, hasa inayohusisha matumizi ya lugha kwa tungo za riwaya pamoja na ngonjera, tungo za kubuni maneno ya kutongozeana.
Sasa kutongozwa kidogo tu na huyo mzee umebakia kumshangaa!
Basi na sisi wazoefu tunabakia kukushangaa kwa kuona unawashangaa watongozaji, mpaka tunaanza kudadisi umri wako sasa!
Nilichokufurahia una heshima zako, siyo mropokaji wa kuwavunjia heshima watongozaji kwa matusi.
Kwa nini haukutoa # za simu, haujamtendea haki huyo jamaa.
Unapotongozwa jiweke kwenye kundi ulilolichagua la kukubali ama kukataa.
Na kwenye kukataa yakupasa uwe na tungo tamu za kumfanya mtongozaji ajisikie raha na asijutie kukusemesha ama kukutana na wewe.
Halafu maneno ya kusema sijui mzee, mnene, mbaya nk nk kuuchambua wasifu wa mtu kwa muonekano wake, badala ya kuyachambua madini anayoyatema toka mdomoni mwake, unakosea sana.
Jenga uzoefu wa kumsikiliza mtongozaji namna anavyomwaga sera huku umemkazia macho ukimsoma toka kwenye paji lake la uso ili kuipata tafsiri ya maneno anayoyaongea na siyo kumkimbia kama mtoto wa shule!
Wewe unaitafsiri vipi karama ya M/Mungu kukupatia sura tamu, wadhania ni kwa ajili ya kukufurahisha mwenyewe, hapana ni kwa ajili ya kufurahisha watu wengine ama kwa lugha rahisi ni kwa ajili ya kukufanya upendwe.
Na mwaka huu utatongozwa sana tu kwa ajili ya uzuri wako acha kulaumu watu.