Nimeamini wanaume hawaaminiki

Nimeamini wanaume hawaaminiki

IMG_2927.jpg
 
Time will tell,ila kwa mwandiko huu tayari ushamwa~demire baba cathe,hata na hivyo kamata fursa hio before its too late!
 
Wewe ni nani kwani? Mbona kama unajitoa [emoji28][emoji28]
Sasa nimeshaleft group kitamboo, na sina nachojua kuhusu uanaume, inakuaje hapo?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nisaidie bas.
 
Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
Acha kwenda nyumba za watu. Kaa kwenu chaumbea.
 
Sasa hapo ame cheat vipi mbona unamsingizia.
Namba hujampa
Hujamsikiloza
Unasema anacheat.
Angekuwa kafanya tukio nawe ndio muhusika ningeamini
Wanaume ni waaminifu mnomno mno
 
Back
Top Bottom