Nimeamini wanaume hawaaminiki

Nimeamini wanaume hawaaminiki

🤣🤣Eeeh Sasa mume mwenye mahaba hivyo utambamba saa ngapi,?Ila Kaswende ndio itazua tafrani
1. Ogopa sana mwanaume akiwa romantiki kupitiliza, unaibiwa😂😂

2. Wanaume wakali wakali kwa wapenzi wao huwa waaminifu kiasi hilo weka akilini
 
Kuna msemo flani kwenye biblia wengi hawauelewi.

Unasema hivi...

(Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

Yohana 8:44)

Robert Heriel Mtibeli
Afafanue
 

Naturally Mwanaume ni polygamist.
Hiyo kuoa mke mmoja ni artificial tuu.
Hakuna mwanaume ambaye moyo wake upo kwaajili ya Mwanamke mmoja.

Ukiona wanaume wanaoa na wapo na mke mmoja ujue wanajitesa na kujizuia Sana. Tuseme wana-fake kwaajili yenu tuu.

Ila kama wakiambiwa na kupewa Uhuru WA kuwa na wake wengi basi wote wangefanya hivyo. Na hapo automatically neno cheating linakosa maana.

Anaye-cheat ni Mwanamke.

Kiasili Mwanamke hasa mtu mwenye jinsia yake kike hupenda na hujivunia kuwa na mwanaume mmoja.
 
Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
Kama una taka kumpa mzee ale, We mpe ajilie sawa ?
Acha maneno mengi, mkamilifu malaika tuu huko mbinguni.

KULA NYAMA NYAMAZAAAAAAAA.
 
Kuna msemo flani kwenye biblia wengi hawauelewi.

Unasema hivi...

(Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

Yohana 8:44)

Robert Heriel Mtibeli
Afafanue

Kuoa wake wengi sio tamaa.
Na haijawahi kukatazwa popote kwenye kitabu chochote cha kidini.

Wanaokataza Watu kuwa na wake wengi ndio wamebuni njia zao wenyewe kupambana na nature na bahati mbaya nature haijawahi kushindwa na ndio maana siku hizi neno MICHEPUKO imechukua haramu ya neno ndoa za Mitala
 
Back
Top Bottom