Nimeamini wanaume hawaaminiki

Nimeamini wanaume hawaaminiki

Mwanamke akipenda kweli kweli acheat lakini sio mwanaume hawajaumbwa hivyo Yani hayo sio maumbile
mwanamke hata akipenda kwelikweli anacheat tu, ila kwasababu unaamini anakupenda hawezi kufanya hivyo ndio maana huwezi kumfumania. mwanamke yeyote asiye na Mungu moyoni (asiyeokoka kwa kweli), anacheat sana na hata usipomkuta jua tu kuwa ameshawahi kukucheat. huu ndio ukweli mchungu. makazini huko, kwenye biashara, masafarini, au ukienda kazini kama wa kwako ni golikipa atapitiwa hata na houseboys au majirani. pona yako mwambie aokoke tu, na asiokoke kwenye makanisa ya uongo ya wauza mafuta hayo, aokoke kwenye makanisa yanayohubiri wokovu wa kweli. hapo hatakuogopa wewe, atamhofu Mungu.
Hata kuokoka nayo haisadii ni mtu tu mwenyewe kuamua moyoni mwake na kukataa zinaa
 
Habari!
Nimekutana na mkasa ambao umenifanya niamini wanaume sio watu wa kuwaamini 100%

Mimi ni mtu ambae muda mwingi najifungia ndani, lakini ikitokea nimekua mpweke sana huwa napendelea kwenda kwa jirani mwenye nyumba inayofuata baada ya kwetu.

Tumeshakua ni washkaji japo yeye ni mtu mzima kiasi, ana mume na watoto watano. Ila mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mshkaji wangu namwita Mama Cathe. Anapendana sana na mume wake familia yao ni bora yenye upendo, kuwaona wamekumbatiana na mume wake ni jambo la kawaida sana.

Nipo karibu nae nimejua baadhi ya mambo, mume wake huwa anarudi kila siku mchana kula, mama Cathe huwa anamsubiri mchana ili wale wote saa 9.

Kwa jinsi wanavyopendana usiku wanaweka msosi nje wanakula mume, mke na watoto kulishana ni jambo la kawaida. Siku zote ninavyowachora mume anampenda sana mkewe, nilikua naona hawezi hata kumsaliti, hata michepuko haijui. Nilikua naamini kuna wanaume ni waaminifu na huyu Baba Cathe nilimuweka kundi hilo kwa jinsi wanavyoishi.

Juzi asubuhi mama kanituma nikanunue mahitaji, natembea zangu kwenye uchochoro mpana nikasikia mtu ameniita 'Ephen!' nikageuka nyuma. Nakutana na Baba Cathe akaniambia 'Nilikuona wakati unatoka nikasema nikufate sababu kila siku navizia nafasi ya kuongea na wewe lakini siipati, kwani unaenda wapi?'

Mpaka hapo nikawa nimeshangaa sikutegemea hii kauli kutoka kwake, hapo anaongea kimahaba
Huyu mzee nilikua namuheshimu sana....Nikamwambia naelekea dukani.

Akasema 'basi naomba namba yako siku yoyote naweza kukupigia tukutane sehemu X, huwa unanivutia sana nahitaji tuongee zaidi' nikamjibu sina simu

Alarm ikalia kichwani kwangu kua ule uchochoro yeyote anaweza kutokea ikawa kesi, sikumjibu nikageuka nikaendelea na safari yangu. Mimi nipo mbele yeye nyuma hapo natembea chap niumalize uchochoro akawa anaongea maneno ambayo siwezi kuyaandika hapa.

Nikamaliza uchochoro na yeye nahisi huku nyuma aligeuza, muda wote nikawa najiuliza huyu mzee kapatwa na nini?

Kilichonishtua ni jana nimekaa kibarazani na mkewe mida ya mchana, karudi mke wake akasimama kumkumbatia, huyu mzee akanikonyeza. Namuona anakuja kwa kasi!

Wanaume wote kumbe wanacheat.....!
U mtu mzima sasa. Huwezi kumkaushia hadi umwanike??
 
Mwanamke akipenda kweli kweli acheat lakini sio mwanaume hawajaumbwa hivyo Yani hayo sio maumbile

Hata kuokoka nayo haisadii ni mtu tu mwenyewe kuamua moyoni mwake na kukataa zinaa
ukiokoka, ukajazwa Roho Mtakatifu, hata kusikia tu neno uzinzi, unahisi kama umesikia neno kinyesi vile. hapo ndipo utajua kuwa Nguvu ya Mungu ikiwa ndani yetu ndipo tunakuwa na uwezo kushinda dhambi bila hiyo hata ukiwa mlokole kimbia wanawake ukikaa nao karibu utazini nao tu. maana ya kuokoka ni kusamehewa dhambi na kukombolewa toka kwenye utumwa wa dhambi na utumwa wa vingine vyote. unapokombolewa toka kwenye dhambi mfano ya uzinzi iliyokufanya mtumwa wa kufanya uzinzi bila kujizuia, ni hatua kubwa mno ambayo Mungu ameiweka kwa ajili yetu. bila hivyo huwezi kushinda dhambi yeyote. hata petro kabla ya kujazwa Roho Mtakatifu aliapa kwamba hatamsaliti Yesu, ila baada ya siku ya pentecost alikuwa tayari hadi kufa hakumsaliti na alishafungwa gerezani mara nyingi kwasababu ya injili ya Yesu, wakati awali siku aliposulibiwa alikana kabisa kwamba yeye hahusiani na Yesu, wasimfananishe.
 
Back
Top Bottom