Nimeamua kuanzisha kilimo cha Korosho Manyoni - Singida

Nimeona mikorosho kadhaa itigi na maeneo ya kongwa
Mkuu hii ni nchi ya kitropiki, korosho inastawi kila mkoa wa Tanzania.
Tunapenda sana badala ya kutumia maarifa tuliopewa shuleni. Tumekazana kuiponda elimu yetu badala ya kuitumia.
Kitu kikubwa ni jinsi gani utapambana na ukame.
Sisi waafrka tunataka kuwa kama mbuzi, vipi Jangwani wapande mazao sisi tushindwe ? Kuna documentari ipo you tube inaonesha Saudi Arabia walivyoamua kuotesha mpunga Jangwani kwa kushirikiana na wachina. Ipo siku warabu watajitosheleza chakula kwa kulima Jangwani, sisi tunashangaa tu.
 
Mtoa mada tunaomba update kila hatua ili kuhamasishana. Wazungu warabu hawawezi badili uchumi wetu bali sisi we nyewe.
 
Si ndiyo?
 
Nikukatishe tamaa tu,kila zao wakoloni walishalijaribu katika kila mkoa, korosho ni pwani na kusini,huko zitakusumbua sana,na pili huitaji kuacha kazi ili ulime, fanya vyote
Manyoni wakati wa mkoloni ilikuwa Dodoma kwa hiyo alime zabibu?
 
Wazo la kuacha kazi ni utoto huo!

Pia fanya utafiti vizuri Manyoni huko kuna watu wamelima wakaangukia pua naskia mashamba mengi yapo kwenye mapito ya tembo miche ikianza kutoka mwaka au miwili tembo wanapita wanatafuna
 
Nakushauri panda miembe ya kisasa...mazao yanayolazimu kuuza kupitia Ushirika usiyaamini.
 
Naomba taarifa hii Kwa mwenye nayo. Hali ya hewa ipi inafaa Kwa kilimo cha korosho?
 
Wazo la kuacha kazi ni utoto huo!

Pia fanya utafiti vizuri Manyoni huko kuna watu wamelima wakaangukia pua naskia mashamba mengi yapo kwenye mapito ya tembo miche ikianza kutoka mwaka au miwili tembo wanapita wanatafuna
kama tembo nashauri afuge nyuki kuzunguka shamba..na kuacha kazi sio wazo la kitoto wengi wanafanya kazi wasizo na furaha nazo na kuogopa kuishi bila mshahara...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…