Nimeamua kuigeuza nyumba ya ghorofa banda la kuku

Huuzi hiyo nyumba? Nina 150 nikupe kesh
Mkuu, kuna kipindi niliishi chumba kimoja, kula misosi ya bei rahisi ili tu hii nyumba itokee.
Its a priceless house. Na hivi nimeijengea kilimani ilinilazimu kuchimba sana chini ili kupata level.
Hiyo nyumba yote ya chini nimejengea zege.
Yani tofali, tofali, katikati zege!
 
Hongera sana, nami nimeanza mchakato kama wako before 2030 ntakuwa kwenye kaghorofa kangu uchwara
 
Ili upate mlion 5 kwa mwez kama faida ulitakiw uingize kias gani cha mauzo ya kuku hao?
 
Umesema upo mkoani vipi huo mradi wa ufugaji nani atausimamia? Mradi wa namna hiyo unahitaji usimamizi wa karibu ili uweze kufikia shabaha ya kutengeneza milioni 5 kwa mwezi.
Pia kwa muonekano, hilo eneo si rafiki wa ufugaji wa kuku.

Kuku ni kichomi asee!
 
Huwa najiuliza mtu kama wewe unauwezo wa kujenga mjengo kama huo ulikuwa unashindwa nini kununua kiwanja kizuri na ujenge kwa ramani na makadirio bora ili uwekezaji wako angalau uwe na tija in future.

Huo uchafu uliousimamisha hapo ni zao la kukurupuka na ukosefu wa maarifa.
 
Ushauri wa bure hiyo hela ya kuku anzisha mradi wa kufunga nguruwe huko kwenye kiwanja chako kingine.

Kama imani yako hairuhusu anza project ya mbuzi aina ya Gala hawa ni wazuri na wanazaa mapacha baada ya miaka miwili utakauwaja kushukuru.Ila jua tu sokoni bei ya mbuzi ni yamoto🔥🔥🔥.Ila ni ufugaji bora na wa uhakika.Hela yako haitapotea kama kwenye kuku.

Ukiamua kua mkulima unaweza pia ukaanza na ufugaji wa sama aina ya sato.Hapa anza na bwawa moja na uwe na angalau 10 millioni.

Kuku wanahitaji comitment ya nguvu na mtaji mkubwa sana.

#kwa ushauri zaidi njoo pm.
 
Kwa utafiti wangu mdogo ni kuwa biashara ambayo mwenyewe haupo karibu kuangalia mara kwa mara mambo yanavyoenda mara nyingi utaishia kuibiwa na kupoteza pesa. Camera zinaweza saidia kidogo sana kufanya remote follow up. Hi biashara unayotaka kuifanya itakugharimu uwekezaji mkubwa na bado itahitaji uweke msimamizi au wasimamizi wa hao kuku,bado utahitaji mtaalam wa mifugo na still itakubidi upate mafunzo ya biashara yenyewe. Huenda hii nyumba yako ikahitaji marekebisho fulani fulani ili kuwezesha hao kuku kuishi na kutaga hayo mayai. Lakini kwa kuwa ni kitu umeshaamua kukifanya basi fanya. Ila naona kabisa ukipata ROI ndogo na kuipata hii ROI itahitaji kufuatilia sanaaaaa mradi wako.
 
Operation cost za kuwezesha kutengeneza hiyo faida utapata changamoto nyingi kwenye hiyo location but it's possible. Hard, very hard but possible.
 
Mradi wa kuku wa mayai utapiga hela mkuu nakusapoti
 

Mkuu, nawajua mabosi wengi wanaolipwa milioni kumi lakini hawana hata chumba kimoja kutokana na mindset kama ya kwako.
Kwa sasa Dar viwanja havishikiki. Sehemu prime kama Goba viwanja vinacheza kwenye milioni 60 hadi 200.
 
Kuiezeka ni gharama kubwa kuliko kujenga mabanda ya kuku nyuma ya hio nyumba. Sioni mantiki wala sababu ya kutuambia unataka kugeuza nyumba yako banda la kuku. Ungejenga mabanda huko nyuma kwa gharama nafuu tu.
 
VInyesi vya mifugo vinaathiri sana kuta.
Ukifugia kuku humo utashusha thamani ya jengo lako.
MAAMUZI NI YAKO LKN.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…