Google, fanya kila utakalo lipata huko. Nilikua na tatizo kama hilo na hua linajirudia rudia. Natumia maji ya kawaida ( room temperature? Asubuh nnapoamka tu cha kwanza ni maji. Asali mbichi sichanganyi chochote, kijiko kimoja kabla ya kila mlo.
Kuna kipindi hua naamua kukimbia umbali mrefu kupandisha na kushuka vilima, choo kinashuka!!! Au zoezi la situps vyote hivyo hua vinanisaidia sana vilevile juis ya ukwaju.
Wengi tu tuna hili tatizo sema ndio hivyo tena kila mtu na siri yake. Kukosa choo kuna tesa sana yaani ni kupata choo ni jambo la kawaida sana ila ukiikosa utajisikia vibaya utakua na mawazo sana. Pole sana najua unayopitia ila jitaidi uende na hospital hata zaidi ya mbili unapima na kulinganisha majibu.