Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Huu uzi umenifundisha mambo mengi sana wakuu..umejaribu na katika kujaribu kwako umefanikiwa kwa plan B ambayo nina imani umeipata kupitia plan ya kwanza ya kulima.

Wakuu dodoma naweza pata wap mashamba ya kukodi?nataka kulima ufuta na mtama mweupe nani ana uelewa na mazao haya..nina mpango wa kuanza na hekari 10 tu yaani 5 ufuta na 5 mtama mweupe.mwenye kujua basi naomba anijuze.
 
Kama upo serious ni-PM na unipe namba zako tuwasiliane,me nina mashamba ya kukodisha Wilaya ya Kongwa kuna sehemu inaitwa Mkoka,ni njia ya kwenda Kiteto.Usafiri wa kutoka hapo kwenda Dodoma mjini upo mwingi mara tatu kwa siku na usafiri wa kwenda na kurudi Dar ni daily!
 
Habari za kazi na pilika za maisha wana Forum. Ninatafuta mashamba ya kukodi, ninahitaji heka 20 , ninaishi Mbeya kama kuna mtu mwenye taarifa za upatikanaji wa mashamba nitashukuru kama atanisaidia,asanteni.

Nenda kawaone wakuuu wa Itende JKT ama nenda kamsamba aua Kapunga Rice scheme
 
Wakuu ninahitaji ekari 50 kwa kuanzia, ni kwa matumizi ya kulima ufuta na mahindi maeneo ya kongwa dodoma, je ni sehemu gani ya kongwa itanifaa zaidi? na ekari moja ninaweza kununua kwa shs ngapi? Na ninaweza kupata namba ya simu ya muhusika/wahusika? Asanteni.
 
Mkuu sana ELnino, vipi maendeleo ya shughuli za kilimo Turiani?
 
ELNINO,

Mbona umepotea mkubwa? au mambo yalienda ndivyo sivyo?
 
Ama jamaa kishakua fisadi na hataki kuongea nasi,au deal ili bounce na anaona soo kurudi kutupa feedback.
 
Na mimi nashindwa kuelewa kabisa

Nadhani yuko bz na kiwanda cha chakula cha kuku pande za Dar kusini. Mmoja wa jamaa zetu humu ndani jf alinitonya siku moja, na inaonekana plant yake inalipa vizuri na imemfanya awe bz na kukusanya raw materials.
 
El Nino if you dont mind walau utu update na progress. Last time you wrote this thread ilikua 18th March 2010. Umeshavuna mara ngapi mpaka sasa na ume expand kama ulivyosema tayari au imekuaje?

Changamoto gani umekumbana nazo katika kulima kwako kwa mara ya pili kama solo agriculturalist?

Na je bado unalima mahindi au umesha divesify?

Please
 
Progress?
 
Bado alikua na fursa ya kutoa progress hapa jamvini na kutujuza maendeleo ya kilimo chake kilichoathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Kama alivyotujuza azma yake ya kulima mara ya pili willingly ndivyo alivyopaswa kutoa progress report ili wadau tujue pia tunajipangaje.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

Mkuu hekimatele tafadhali pitia uzi wote kuanzia mwanzo, Ndugu elnino amekuwa akitoa updates mara kwa mara na wengi tumenufaika na darasa hili.
 
Last edited by a moderator:
ELNINO,

Unajua nilivyosoma uzi wkao kwa mara ya kwanza ulinihamasisha sana nikaenda kukurupusha pori kubwa nikaanza kupunguza visiki. Kumbe baadae mzee ulichemsha sasa dah energy yote ikapungua aisee.
 
Hongera mkuu penye nia pana njia, mie mwenyewe ipo siku nitarudi kwenye kilimo kwanza maana niliwahi kujaribu nikala loss kwa kuwa nilikuwa nategemea mvua, kikubwa ni kukomaa hasa palizi ya kwanza na ya pili hakikisha unasimamia palizi maana ukichemsha hapo utavuna mabua.

Pia usikate tamaa hata kama hutopata kile ambacho umekusudia jaribu tena msimu mwingine. Mie mwenyewe najipanga mkuu ipo siku nitarudi tena kwenye kilimo kwanza maana kiukweli kilimo ukikichukulia serious kinalipa na uzuri unaweza fanya kazi za kilimo huku unafanya kazi nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…