Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Unaweza kunicheck kwa hii no 0715162344 naweza kukupa CBA na masterplan ya matikiti
 
Je waweza nijulisha ni mbegu gani unatumia katika kilimo cha mahindi na sifa zake! Me ni mkulima mchanga nahitaji uzoefu wenu tafadhari
Mkuu huyo aliyepata gunia 43 alitumia maji ya kumwagilia au alitegemea mvua tu?
Huyu anategemea mvua. Bado hapa nchini kuna maeneo bado mvua ni nzuri hasa za masika. Mfano mkoa wa Iringa wilaya kama mufindi. Lakini anapractise kilimo cha kisasa. Na kikubwa anacheza na afya ya udongo na technologia ya zero tillage. Lakini pia spacing yake inampa miche mingi kwa eneo.
 
Inategemea unalimia wapi?

Kaskazini wanalima kisasa,wamesoma na wanamwomba Mungu,hawa hupata gunia 20.

Mikoa mingine inayoomba mizImu hupata gunia 9
Daah! Mkuu umetisha sana. Hapa nakubaliana na wewe
 
Inategemea na mahali unapolima.kisiasa ni gunia 30-40.ki uhalisia ukifuata kanuni 10 za kilimo bora ni gunia 10-12.milele na milele
 
Inategemea unalimia wapi?

Kaskazini wanalima kisasa,wamesoma na wanamwomba Mungu,hawa hupata gunia 20.

Mikoa mingine inayoomba mizImu hupata gunia 9
Hahahaa mkuu umenichekesha...hahaahaa mikoa tofauti na kaskazini wanatumia mizimu gunia hazizidi 9 kwa ekari.
 
Naam swali lako ni pana sana. Mfano nyanda za juu kusini wao ndio wanaoongoza kwa kuzalisha zaidi. Wao mvua zao ni ndefu na wanaweza kupanda mbegu inayokaa shambani hadi siku160 kukomaa.

Hii inazaa sana mandhali tu mbolea itakuwepo. Hapa panawezekana kupata tani 40 kwa mkulima mtaalamu. Ukanda pwani mvua zao fupi na.mbegu zao fupi na hivyo kiwastani mkulima mtaalamu akivuna saaana ni hizo gunia 15 hadi 20.

Kumbuka kadiri unayoipa mbolea ardhi ndivyo utavyovuna
 
Je waweza nijulisha ni mbegu gani unatumia katika kilimo cha mahindi na sifa zake! Me ni mkulima mchanga nahitaji uzoefu wenu tafadhari
Mbegu zipo nyingi sana lakini ni location specific. Lazima ununue ambazo zimeshathibitishwa kwenye zone yako
 
Inategemea unalimia wapi?

Kaskazini wanalima kisasa,wamesoma na wanamwomba Mungu,hawa hupata gunia 20.

Mikoa mingine inayoomba mizImu hupata gunia 9
Mngekuwa mnalima kisasa na mmesoma na mnamuomba huyo Mungu wenu si mngekuwa mnailisha Tanzania nzima nyinyi,acha logic zako za kijinga..kwa mahindi nyanda za juu kusini ndo wakulima hodari, hizo pumba ulizoandika wapelekee hukohuko
 
Asante kwa darasa zuri sisi wakulima tumekuelewa. Mimi niko Tanga mbegu niliyotumia ni seed. co vp unaweza kunisaidia sifa ya hii mbegu?
 
Asante kwa darasa zuri sisi wakulima tumekuelewa. Mimi niko Tanga mbegu niliyotumia ni seed. co vp unaweza kunisaidia sifa ya hii mbegu?

mbegu za seedco zipo za aina nyingi na zina namba na sifa tofauti lakini nyingi zinakomaa muda wa kati kuanzia siku 130
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…