Habari wandugu, ashukuliwe Mungu kuwa tuwazima na anatupigania kwenye changamoto za maisha.
Kwa hali ya kiuchumi ilivyo kwa sasa inatubidi kutafuta miradi tofauti tofauti ili kumudu hali ya sasa. Kwa mtazamo wangu naona sasa ipo haja ya kuitumia ardhi tulio nayo kutuletea maendeleo na sio kukaa na kulalamikia hali ngumu ya maisha.
Katika hayo naombeni kujuzwa kuhusu kilimo. Cha;
1: maparachichi.
Kilimo hiki kipoje, kinahitaji hali ya hewa ya namna gani?
Ni maeneo yepi hapa nchini yanafaa kwa kilimo hiki.?
Vipi kuhusu masoko yapoje?
2:. Matikiti major:
Hapa pia naomba kujuzwa, nifanye nini ikiwa nataka kulima matikiti maji,
Changamoto zake zikoje?
3: Mahindi:
Kilimo hiki kinaonekana kudharaulika lakini kila uchao unga unapanda bei.
Hivi ni njia zipi Bora za kilimo cha mahindi?
Ni mbegu zipi ni bora zaidi kwa hapa nchini hasa kwa mkoa wa morogoro?
Kwa wale wataalamu wa kilimo naomba mnijuze hayo, naamini itasaidia wengi wenye nia kama yangu.
Natanguliza shukurani zangu kwenu.