Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Tafadhali Bavaria tunaomba utupe na upembuzi yakinifu kuanisha matumizi yatakayo tumika mpka kufikia kupata fedha tsh 300,000,000/=. Kwani mpaka upata hii pesa lazima utakuwa umetumia pesa nyingi sana kwa ajili ya kulima, kupanda kupalilia n.k. Please pembua zaidi tuweze kuanisha mtaji, matumizi na faida itakayo salia baada ya kupata tsh 300,000,000/=.[/
SoQUOTE]
 
Taadhari,

Kuna kitu kinakosekana katika michanganuo yote niliyoiona hapa. Uzalishaji wa mazao sio kama wa kiwandani,i.e the volume/quantity of INPUTS determines the level of OUTPUT.

kuna vitu vitatu muhimu sana kuvizingatia na kuviweka katika hesabu, navyo ni:
() Magonjwa - Deseases
() Uharibifu - Farm loss
() Mavuno - Yield variance

Magonjwa huweza kushusha uzalishaji mpaka chini ya 30%. Kila mara mmea unaposhambuliwa unalazimika kuelekeza nguvu zake katika kupambana na ivyo usimamisha zoezi lolote la kurutubisha zao. Mfano mzuri ni wewe mwanadam ukiugua ugonjwa kama malaria, ngumu kufanya kazi yoyote na upelekea hata hamu ya kula kushuka sana.

Tambua ya kuwa mazao ukomaa na kuiva kwa nyakati tofauti pia uharibika haraka. Hii upelekea asilimia zaidi ya 40% ya mazao yanayozalishwa shambani kuharibika hata kabla hayajauzwa au kumfikia mlaji. Kwenye kitalu nyumba uharibifur ucheza kati ya asilimia 10 hadi 20.

Jambo la pili ni kuwa mazao utofautiana ukubwa na ubora hivyo kusababisha bei nayo kutofautiana. Katika shamba la ekari moja mazao ya kiwango cha juu huwa kama 10% - 20%, kiwango cha kati ni asilimia 40% mpaka 60% na kiwango cha mwisho 20% - 30%.

Bei ya soko inabadilika kutegemeana na mahitaji na wingi wa mazao sokoni, msimu ukikubali na mavuno yakawa mengi jua kuwa bei itatelemka sana. Hii ni sababu kuu mabenki mengi hayapendi kukopesha wakulima. Bei za mazao uyumba sana na uzalishaji hautabiliki kutokana na changamoto za hali ya hewa (hata kama unamwagilia).

KITALU NYUMBA (GREENHOUSE)
Hapa pamejaa UTAPELI mwingi sana.

Kitalu nyumba ni kilimo cha kisayansi mnoo. Kinahitaji elimu ya kiwango cha juu na uwezo mkubwa wa kutumia teknolojia kuhakikisha mazingira ya kitalu nyumba yanakuwa ni yale shahiki (ideal) kwa zao lako. Waholanzi na Waisraeli ni manguli sana katika hiki kilimo cha kitalu nyumba na tayari wana miundombinu mingi inayowezesha hilo kufanyika kwa ufanisi mkubwa. Kwa wenzangu wa huko Tanzania kwa kweli kuna changamoto nyingi sana kukuwezesha kufanikiwa na kilimo cha kitalu nyumba.

Jambo la WAZI na la kimahesabu (FINANCIAL) kuhusu kitalu nyumba ni kuwa uzalishaji wake ni wa gharama mno ivyo lazima walaji wawe na uwezo wa kumudu bei ya mazao yako. Ulaya na Japan watu wengi wanauchumi mzuri lakin pia ardhi ya kilimo ni ndogo na wanachangamoto ya hali ya hewa (barafu & kipindi kifupi cha jua kwa ajili ya Photosynthesis), wanaishia kuagiza sana bidhaa za kilimo. hii imetengeneza fursa kwa mataifa kama Israel, Malysia, Philipines, Kenya kuzalisha mazao ya kuuza nje.

Ukizungumzia kuzalisha kwenye kitalu nyumba na kisha utegemee kuuza masoko ya ndani, utakabiliana na changamoto ya gharama za uzalishaji. Kitalu nyumba sio mwanzo wa kupata mavuno makubwa na si uhakika wa kukuza uzalishaji. Bali usimamizi makini na wakisayansi pekee ndio utakao kupa mavuno bora na mengi.

Mwisho niwasihii, matatizo ya kiatanzania lazima yajibiwe kwa mbinu na nyenzo zinazopatikana nyumbani. Elewa kiini cha Kitalu nyumba ni nini, jambo gani limepelekea kubuniwa kwake. Kitalu nyumba ni jibu la changamoto zilizopo nchi za baridi/jangwa. Mungu ameribariki bara la Africa kwa kuwa na ardhi nyingi yenye rutuba, mito, maziwa na jua la kutosha kuwezesha kilimo kufunyika shambani na kutoa mavuno mengi.
 
mkuu nimependa sana uchambuzi wako, kwa kifupi kilimo hapa Tanzania kinalipa sana ila chataka uwe mvumilivu na umejitoa kufanya kilimo km ajira yako.

kwa hapa kwetu watu wengi wanaolima hawajasoma na km amesoma basi anaachia uangalizi wa shamba kwa mtu ambae hajasoma hence shamba linaendeshwa kienyeji.

km mtu umejitoa na unafanya kilimo km ajira hapana shaka utafanikiwa sana coz utazingatia mda wa kupanda na kuhudumia shamba (mbolea na dawa)

Mwisho kabisa watanzania wengi hasa wasomi hawapend ku-take risk ktk mambo yao ndo mana wasomi wengi maisha yao ni wastani mnoooo,ana nyumba na gari basi,hana asset yeyote ile ya MAANA.
 
Kilimo wizi mtupu....

Kilimo sio wizi mtupu ila kuna sehemu umekosea kwenye njia zako na ndo maana zimekuangusha.
Ushawahi kujiuliza haya makampuni makubwa ya kilimo yanafanyaje hadi kufanya mass production kwa mafanikio?
Usikate tamaa kama umedhamiria.
Simama endelea kupigana.
 
Ndugu yangu Milungwi angalia hiyo nilishamjibu mtu inaweza kukusaidia na kama bado niambie, kama uko tayari mimi narudi Bongo end of this week, naweza kukupeleka shambani kwangu ukaangalie ili ujifunze, wewe nieleze tu kama uko serious.

Mimi ni mtoto wa Mkulima nina asili ya kilimo ingawa kwetu huko Moro tunalima sana mpunga lakini nimeamua nifanye maamuzi ya uangalifu sana kwenye aina ya mazao ya kulima yasiyoleta usumbufu wa maradhi au kuathirika sana na ukame na ndo maana nikachagua kulima miwa Kilombero na mananasi Bagamoyo.

Mananasi yanapendwa kipindi chochote cha mwaka hata wakati wa jua kali na hayafi, mvua ikija tu yanachipua, kinachotakiwa ni palizi za nguvu na mbolea ya nguvu. Hekari moja ya muwa unaweza tumia mfuko mmoja wa mbolea lakini kwa mananasi kati ya mifuko 4-5 ya mbolea.

Angalia hapa kwa uangalifu na hayo ni mahesabu yaliyo sahihi kabisa hayana shaka ndani yake. Kwa gharama ya hapo chini hata ukiongeza asilimia 20 ya gharama bado unapata super profit.

Usikate tamaa, hata hekari moja ukiitunza vizuri inalipa. Angalia mahesabu ya hekari moja.

Shamba lenye visiki
Gharama za kuondoa visiki = 250,000
Kulima = 70,000
Kupiga hallo = 50,000
gharama za mbegu (16,000 kwa hekari moja) =1,440,000
Gharama za kupanda Tshs 15 x 16,000) =240,000
Kupalilia kama mara tano hivi Tshs 60,000 x 5 = 300,000
Mbolea mara mbili kabla ya kuvuna jumla mifuko 10 = 700,000

Jumla ya wastani wa gharama zote hadi unavuna (Total cost) = 3,050,000

Mauzo kwa bei ya wastani wa Tshs 800 kwa nanasi moja, mimi kwasasa hivi nauzi kwa Tshs 1000 kwa nanasi toka shambani kwangu na hakuna tax, kwa hiyo wewe utapata 16,000 x 800 =12,8000
Faida 12,800,000 - 3,050,000 =9,750,00 super profit.

Sasa mimi niliamua nifanya mass production ili hata kama bei itapungua bado nitapata faida kubwa kwa ajili ya economies of scale.

Anza leo usingoje kesho.

Kila la kheri
 
nimependa sana!ila nimawazo mazuri sana!kinachotakiwa niwapi tukope tununue tufanye kilimo!
 
Tunashukuru kwa kutuamsha vichwa , sisi tume zoea kukaa mlimani city tuu kuteketeza noti
 
mkuu ntafutie shamba la kukodi,,,ela za boom nikalimie na mimi maana chuo kikiisha ni mfulio tu,,,ntumie na bei ya kukodi
 
mkuu ntafutie shamba la kukodi,,,ela za boom nikalimie na mimi maana chuo kikiisha ni mfulio tu,,,ntumie na bei ya kukodi

Hizo hela za heslb ukiziweka kwenye kilimo inabd uwe makini sana vingnevyo kama familia siyo imara unaweza kuahirisha masomo kwa mda. Jitahidi sana uwe na msimamizi mzuri.
 
Vp kwa Korogwe Tanga, mda upi mzuri kwa kilimo hiki? Msaada
 
Unaweza kupanda pale mvua za february zinaanza, panda mahindi ya muda mfupi.

Unavuna kabla hayajakomaa.
 
Ingawa mimi ni mwajiriwa lakini deep inside nimejitambua kuwa mimi ni mkulima na mfugaji.
Kwa miaka kadhaa iliyopita nimekuwa nikisoma, kutathmiin na kupanga mipango mbali mbali ya kilimo na ufugaji na kuitekeleza kwa kiwango kidogo sana.
Sasa mwaka huu nimepata mabadiliko ya kikazi ambayo nataka niyatumie kutimiza ndoto zangu.
Nitaanza utekelezaji mwezi ujao na kama nikifanikiwa in shaa Allah mwisho wa mwaka nitawaletea mrejesho.

Mkuu naomba mrejesho kwenye ufugaji
 
ni kweli Bavaria nimeangukia pua mara ua tatu sasa kwa kutegemea wafanyakazi, yaani nimepata hasara mpaka nimeamua kuachana na kilimo kwa sasa.
Watanzania wengi hatuna hulka ya kufanya mambo kwa weledi wa hali ya juu.
Simama mwenyewe mkuu, ukiweka mkono wa mtu wa nje tegemea kulia.
 
ni kweli Bavaria nimeangukia pua mara ua tatu sasa kwa kutegemea wafanyakazi, yaani nimepata hasara mpaka nimeamua kuachana na kilimo kwa sasa.

Pole mkuu so tatizo hapa si kilimo bali ni wewe mwenyewe which is ok sisi ni binadamu tunajifunza kwa makosa either yetu wenyewe au ya wengine. Cha muhimu kuwa positive kwa yaliyokukuta na kuona kuwa ilikuwa nafasi yako kujifunza kwamba mambo yapi hupaswi kuyafanya utakaporudi tena shambani na yapi unatakiwa kuyafanya ili ufanikiwe.
 
Nina kuku wa mayai 500 ambao wana miezi miwili sasa.
Mbuzi watatu, kuku wa kienyeji 15 na koo moja linalalia.

Niko mbioni kununua ng'ombe wa maziwa, bata na kanga.
Ndio nakamilisha ujenzi wa mabanda.
Hongera kwa kuleta mrejesho
 
ni kweli Bavaria nimeangukia pua mara ua tatu sasa kwa kutegemea wafanyakazi, yaani nimepata hasara mpaka nimeamua kuachana na kilimo kwa sasa.

Kama umeajiriwa achana na ajira ingia kwenye kilimo au achana na kilimo kabisa.
 
Back
Top Bottom