Taadhari,
Kuna kitu kinakosekana katika michanganuo yote niliyoiona hapa. Uzalishaji wa mazao sio kama wa kiwandani,i.e the volume/quantity of INPUTS determines the level of OUTPUT.
kuna vitu vitatu muhimu sana kuvizingatia na kuviweka katika hesabu, navyo ni:
() Magonjwa - Deseases
() Uharibifu - Farm loss
() Mavuno - Yield variance
Magonjwa huweza kushusha uzalishaji mpaka chini ya 30%. Kila mara mmea unaposhambuliwa unalazimika kuelekeza nguvu zake katika kupambana na ivyo usimamisha zoezi lolote la kurutubisha zao. Mfano mzuri ni wewe mwanadam ukiugua ugonjwa kama malaria, ngumu kufanya kazi yoyote na upelekea hata hamu ya kula kushuka sana.
Tambua ya kuwa mazao ukomaa na kuiva kwa nyakati tofauti pia uharibika haraka. Hii upelekea asilimia zaidi ya 40% ya mazao yanayozalishwa shambani kuharibika hata kabla hayajauzwa au kumfikia mlaji. Kwenye kitalu nyumba uharibifur ucheza kati ya asilimia 10 hadi 20.
Jambo la pili ni kuwa mazao utofautiana ukubwa na ubora hivyo kusababisha bei nayo kutofautiana. Katika shamba la ekari moja mazao ya kiwango cha juu huwa kama 10% - 20%, kiwango cha kati ni asilimia 40% mpaka 60% na kiwango cha mwisho 20% - 30%.
Bei ya soko inabadilika kutegemeana na mahitaji na wingi wa mazao sokoni, msimu ukikubali na mavuno yakawa mengi jua kuwa bei itatelemka sana. Hii ni sababu kuu mabenki mengi hayapendi kukopesha wakulima. Bei za mazao uyumba sana na uzalishaji hautabiliki kutokana na changamoto za hali ya hewa (hata kama unamwagilia).
KITALU NYUMBA (GREENHOUSE)
Hapa pamejaa UTAPELI mwingi sana.
Kitalu nyumba ni kilimo cha kisayansi mnoo. Kinahitaji elimu ya kiwango cha juu na uwezo mkubwa wa kutumia teknolojia kuhakikisha mazingira ya kitalu nyumba yanakuwa ni yale shahiki (ideal) kwa zao lako. Waholanzi na Waisraeli ni manguli sana katika hiki kilimo cha kitalu nyumba na tayari wana miundombinu mingi inayowezesha hilo kufanyika kwa ufanisi mkubwa. Kwa wenzangu wa huko Tanzania kwa kweli kuna changamoto nyingi sana kukuwezesha kufanikiwa na kilimo cha kitalu nyumba.
Jambo la WAZI na la kimahesabu (FINANCIAL) kuhusu kitalu nyumba ni kuwa uzalishaji wake ni wa gharama mno ivyo lazima walaji wawe na uwezo wa kumudu bei ya mazao yako. Ulaya na Japan watu wengi wanauchumi mzuri lakin pia ardhi ya kilimo ni ndogo na wanachangamoto ya hali ya hewa (barafu & kipindi kifupi cha jua kwa ajili ya Photosynthesis), wanaishia kuagiza sana bidhaa za kilimo. hii imetengeneza fursa kwa mataifa kama Israel, Malysia, Philipines, Kenya kuzalisha mazao ya kuuza nje.
Ukizungumzia kuzalisha kwenye kitalu nyumba na kisha utegemee kuuza masoko ya ndani, utakabiliana na changamoto ya gharama za uzalishaji. Kitalu nyumba sio mwanzo wa kupata mavuno makubwa na si uhakika wa kukuza uzalishaji. Bali usimamizi makini na wakisayansi pekee ndio utakao kupa mavuno bora na mengi.
Mwisho niwasihii, matatizo ya kiatanzania lazima yajibiwe kwa mbinu na nyenzo zinazopatikana nyumbani. Elewa kiini cha Kitalu nyumba ni nini, jambo gani limepelekea kubuniwa kwake. Kitalu nyumba ni jibu la changamoto zilizopo nchi za baridi/jangwa. Mungu ameribariki bara la Africa kwa kuwa na ardhi nyingi yenye rutuba, mito, maziwa na jua la kutosha kuwezesha kilimo kufunyika shambani na kutoa mavuno mengi.