Nimeamua kumuacha mwanamke niliyedumu naye kwa Miaka 7

Nimeamua kumuacha mwanamke niliyedumu naye kwa Miaka 7

Optimists

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2021
Posts
379
Reaction score
1,082
Wakuu nitakua nakosea?

Ni binti niliekutana nae zamani kidogo tokea nasoma form four nilimuacha madarasa mawili nyuma, tulikua marafiki tu ni mtu ambae tumedumu nae kama rafiki na mpenzi kwa miaka mingi sana, katika mihangaiko yote ya maisha ya shule, chuo na kitaa Niko nae mpaka Leo.

Kwanini nataka kumuacha?.

Mwaka jana baada ya kumaliza chuo huku yeye akiwa kitaa tu nilimpa mimba sikupinga nikamwambia as long as Mimi ni mwanaume nitapambana (nilipata sehemu ya kujishikiza), na pia ni mwanamke wa ndoto zangu so asitoe mimba nitalea na nitamuoa but mama ake akaitoa(kuna mambo mengi yalitokea hapa), ilo jambo lilinipa wakati mgumu sana but nikasamehe baada ya yeye kujiliza sana.

Mda umepita kidogo naona amebadilika kiasi, ninachomwambia afanye anisikii tena nikimwambia yaishe afanye maisha yake anajilizaa sana,imekua kama mchezo nikimwambia tuachane anajiliza but makosa anafanya mengi ya hovyo yanayojirudia.

Anapenda kupost wanaume akidai ni marafiki zake (marafiki ya konyo.....nilishamkataza habari za hao anaowaita marafiki maana "hakuna rafiki wa kiume kwa mwanamke asiyewaza kumla kimasihara" atajifanya rafiki mwisho wake ataliwa tu but amekua mzito kusikia.

Nimeweka standard zangu nikimwambia ajiweke karibu na Mungu anielewi anapenda sana mambo ya mitandao haswa kupost upuuzi usiokua na maana (sababu ya umri wake labda).

Nimerudi mjini sababu ya ubusy wangu wa kutafuta maisha nikamwambia tuonane (sio kufanya mapenzi) maana hapo kabla alikua analalamika sina mda nae tukakubaliana mda wa kumuona nimetoka zangu mbezi mpaka gongo la mboto namsubiria weeee anadai amepata dharula yuko Mwenge.

Nb..
Nimeona kama nafuga ujinga tu then kukaa na mpenzi miaka mingi isiwe guarantee ya kusema lazima muoane akibadilika ni vyema kujiondoa tu kuepusha vingi.

Huu mda nawekeza zaidi kutafuta maisha pia ushauri never trust a women akibadilika achana nae regardless mmekaa miaka buku.
 
Kwani yeye yupo ndani ya mipango yako?? Namaanisha anajua mipango yako juu yake na yeye anajua nafasi anayotakiwa kucheza ila anafanya kusudi ama?

Au labda ye anaona kama mnakuzana tu?

Kama anajua na kabadilika basi piga chini kama anaona ni mnapashana joto tu basi pasha joto mkuu usimuache kwa sasa.
 
Mwanamke anayejielewa na anaemuheshimu mpenzi wake hawezi post wanaume status labda nmwale anaojua wanafahamika kwa mpenziwe

Red flag nyingi lakin umekazania tu
Mjinga sana sio Mara moja au mbili na nikamwambia basi tuachane atajiliza siku nzima
 
Wewe hata week haijaisha tangu uamue kumuacha unaanza kushauri, muache kwanza ipite miezi sita ukiweza kumuacha kabisa ndio uje kutoa ushauri humu, vinginevyo atajiliza tena utamrudia!!!
 
Humu utapewa kila aina ya ushauri but at the end muamuzi ni wewe mwenyewe,

Fanya kile nafsi yako inataka.
 
Nimeona red alert nyingi kwenye maelezo yako lakini bado ukqendelea kukomaa naye tu ...any way as long umesha shtuka sasa ... usirudi nyuma tena utakuja geuka jiwe la chumvi
Maana huyo inaonekana amesha kuzoea kiasi kwamba kubadilika ni ngumu labda umhamishe mji
 
Sijamjua Jana Mkuu, ni miaka saba sasa ni mtu mzima sasa age ya 23 kama bado hajajua kipi ni kizuri kipi ni kibaya basi ni ujinga anafanya.
IMO mkuu binti wa miaka 23 ana akili ndogo, bado anahisi ana chances za kutosha. Temana nae.
 
Nyie ndio wale huko na mapenzi ya kuongea na simu hadi inachemka kama pasi. Kifupi ni kwamba nyote bado hajafika uelewa wa kua wapenzi tena wenye mlengo wa kuoana
 
Umeishi nae miaka 7, ulikua na mpango wa kumuoa.
Kwann ukufanya juhudi zozote za kuanza kuish karibu nae uone Kama atabadilika izo tabia zake au lah[emoji848]
 
Back
Top Bottom