Safi kijana umeamua kujilipua. Fuata haya.
1.Piga chini marafiki bakiza wawili tu wa msingi.
2.Chagua kazi, usifanye kila kazi achana na wakina usichague kazi, hii itasaidia kuacha kutangatanga bila maslahi.
3.Muda wako ni bidhaa ni fedha, msaada ukiona utazidi nusu saa, charge hata 1000. Kuna time nilikwama sehemu, hawa wakina whatsapp Gb,sijui simu imefanyaje mwendo ni buku.
4.Inaendelea ktk muda, storiza kusukuma muda achana nazo au zisizidi 45 dakika kakae hata ndani tu.
5.Jenga tabia ya kununua bidhaa duka moja na kuwa mwaminifu(rafiki wa tatu huyu)ukikwama unaweza kopa kidogo.
6.Jifunze skill mpya ambayo inaweza kukufanya u survive mfano kuendesha chombo cha moto pikipiki au gari.
7.Ukipata hela nunua bidhaa zinazoweza kuzalisha, sio subwoofer,Tv hauna huo muda kwa sasa..bora ununue kitabu. Nunua kitu kama kompyuta unaweza kuwaambia watu mtaani unaweka muvi kwa buku kadhaa. Watangazie wadada na wamama wa hapo ulipopanga,watawaambia wenzao.Nunua flash za mafungu uzia geto reja reja ukitoka mitikasi.
HIZO ZOTE NI INTERMISSIONS wakati unaitafuta MISSION kubwa ili usishindwe kula na kulipa kodi.
Mtaani hapo kama kuna gap la ulinzi mcheki mjumbe akujumuishe kwa malipo usikae bure, na usilale sana lala masaa manne hadi matano tu.
8. Usione noma man, yule rafiki wa tatu mwombe uweke hata bidhaa moja au mbili dukani kwake hata karanga.
9.USISIKILIZE DHIHAKA NA MAJIGAMBO YA WATU KILA MTU ANA NJIA ZAKE NA MAGUMU YAKE,KAMA YEYE KAWA BLESSED NA NJIA RAHISI NI YEYE NA HAKUSAIDII KITU.
Kama kejeli za waliokujibu huko juu wakikuona mzembe. We waza hao wote ni mik*n*u tu fanya yako.