Nimeamua kuondoka kwa kaka na kujitegemea

Nimeamua kuondoka kwa kaka na kujitegemea

Kama utajizuia kufanya zinaa, kunywa pombe , kamari na kujitahidi kujizuia na yale yasiompendeza Mtoa Ridhki...
.... Mimi nakuombea "inshallah" mwaka hauishi huu utaona mabadiliko chanya.
 
Kila la kheri kamanda Mungu akubariki
 
Nimesema labda wewe unapinga kabisa mkuu, kwani we unamjua jamaa!??
Jamaa simjui na hakuna nilipopinga nilichompa ni ushauri huwezi ukafanya Mambo kwa kukurupuka, nikampa mfano wa yule jamaa alienda muleba akaanza kutapatapa humu anaomba MSAADA wakati kwao aliondoka mwenyewe akaenda muleba eti kutafuta maisha hamjui mtu hana ramani akaanza kuomba kazi kwenye ofisi za utalii so what? Fanya Mambo kisomi sio unakurupuka ukipata shida unaanza kusumbua watu na kutiatia huruma
 
Habari za muda wakuu jana niliomba ushauri kuhusu kuhama kwa kaka yangu.

Kiukweli najilaumu sana kuchelewa kuanza maisha kwa sababu ya kusubili ahadi za ndugu toka nikiwa na miaka 23 nimekuwa nikiahidiwa msaada na mbaya zaidi mimi ndio nilikuwa nipo nyumbani na mama huko mkoani, Nimekuwa pale kwa miaka mingi huku ndugu zangu wakiwa dar.

Kila wakija walikuwa ni watu wa kuniahidi kunisaidia jambo ambalo limenifanya kubweteka.

Nimeishi hapo mpaka pale kaka yangu alipokuja kunichukua mwishoni mwa 2019 yeye pia baada ya kunileta ajajitoa kwa dhati kwa ajili ya kunipa msingi bora japo uwezo wake kifedha c haba na kaajili watu wengi ila mimi amekuwa akiniunganisha kwenye kazi za kuangaika sana mpaka sasa sina maendeleo yoyote nafsi inaniuma sana maana nimechelewa sana kuanza kujitegemea now nina miaka 32 kiukweli naona aibu kuendelea kubaki hapa kwa bro.

Sina msingi wala mtaji ila niluchoamua from now nikuuza simu yangu na kwenda kupanga mengine yatajulikana mbele ya safari najua ni uamuzi mgumu lakini nimeamua kwa moyo wa dhati kwenda kujitegemea.

Nimechelewa sana nafsi inaniuma mno sina furaha kwakweli ila nilichoamua ndicho hicho. Na hakuna kurudisha mpira kwa kipa naenda kuhastle kiukweli.

Naombeni baraka zenu ndugu zangu.
Pole ila wahenga walishasema mtegemea cha ndugu hufa masikini vile vile biblia imeandika Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu hvyoo jitafute ujipange upya muda bado upo ni heri umeshtuka na 32 kuna wenzio walishtuka na 40 na kuendelea
 
Nimecheka kama mazuri🤣🤣
 
Pole ila wahenga walishasema mtegemea cha ndugu hufa masikini vile vile biblia imeandika Alaaniwe amtegemeaye mwanadamu hvyoo jitafute ujipange upya muda bado upo ni heri umeshtuka na 32 kuna wenzio walishtuka na 40 na kuendelea
Nimecheka kama mazuri🤣
Kila la kheri kamanda Mungu akubariki
Amina mkuu
 
Uamuzi mzuri, ila ungejipa kama mwezi hivi,.inawezekana spirit hiyo imechochewa zaidi na hisia kuliko uhalisia, baki Kwanza kwa broh, then fanya michakato ukiwa hapo, ukitoka atleast uwe na pakushika, mtaani kugumu sana sio km unavyofikiri wew, jipange usije poteza ubingwa au kujiingiza kwenye madawa ya kulevya.
Kaka mimi nafsi yangu inanituma hivo yani naskia kabisa msukumo wa ndani ya moyo naamini mungu atanibariki japo changamoto azikwepeki
 
Ndio maana nikakwambia plan yako sio unakurupuka je umeandaa mazingira gan uko unakokwenda? Km umejiandaa go ahead champ one day yes no retreat no surrender,
Plani yangu ndio japo nitasota mwanzo lakini naamini baadae mambo yatakaa sawa
 
Kama utajizuia kufanya zinaa, kunywa pombe , kamari na kujitahidi kujizuia na yale yasiompendeza Mtoa Ridhki...
.... Mimi nakuombea "inshallah" mwaka hauishi huu utaona mabadiliko chanya.
Amina boss wangu naamini huu ujumbe sio bure
 
Kama nakufahamu vile[emoji28][emoji28]

Jikaze mkuu ugali wa shikamoo haufai
 
Mkuu kila la kheri huko itafahamika uko uko, wewe kapambane Ila hakuna kurudi home hata ufe
hicho ndicho naenda kukisimamia zaidi siwez rudi home maana hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwangu mwenyewe
 
Back
Top Bottom