Nimeamua kupaki gari nitumie usafiri wa umma

Mmmmh kakaa..!!

Hilo gari lako ni bus nn mpaka km 20 ukatumia lita 4?

Maana kama kwenda km10 na kurud km10 sasa iweje utumie lita 4 kwa km 20?
Zinatakiwa ngapi mkuu
 
Hivi thamani ya pesa yetu imeenda wapi?

Nakumbuka zamani ilikuwa rahisi kutembea kutoma Makumbusho hadi Posta-Kariakoo, sijui imetokea nini siku hizi watu wansema eti hapo mbali.

Ukitoka makumbusho ukakata hadi kinondoni, kisha kinondoni hadi posta, na ukifika posta, kariakoo ni karibu sana, unapaswa kuwa na pesa ya kula na kunya maji tu.

Na makumbusho hadi kariakoo hata ukipita njia ya mwananyamala ukaibuka Tandale, uka unga mpaka magomeni na kisha kuibuka kariakoo bado siyo mbali kiivyo.

Zamani nilikuwa natoka Magomeni mwembe chai hadi Muhimbili kwa mguu, na sijawahi kupaona mbali. Nilipohamia Makumbusho ilikuwa vivyo hivyo, ila siku moja moja nilikuwa nikitusua deal napanda dala dala. Sikupenda kuzizoea kwasababu nilikuwa bado natengeneza foundation ya maisha yangu.

Juzi hapa mwanafunzi wa MUHAS anaishi Mkwajuni eti anapanda daladala, nikamuuliza kwanini usitembee, anasema mbali sana, nikamwambia sisi tulikuwa tunakatiza mkwajuni unaibukia wodi ya watoto uwanja wa mpira Muhimbili., au umbali umeongezeka ? akasema yeye hawezi kutembea, nilimuangalia nikasema ndio maana mnamaliza chuo na madeni mengi sana.

Nimetembea sana Dar es salaam hiyo, sioni kwanini nijitese. Naweza kununu baiskeli na life ikaenda vizuri tu, kwanini nimlipe boda au gari/daladal pesa yangu ya ujira wangu wote. Tujifunze kupunguza gharama maisha ni magumu ukiyaendekeza, yakikomaa nawe komaa nayo utafika tu.

Kwanini tunajiingiza gharama kuubwa bila kujua au ndio life style imebadirika?

Mna save vipi nyie wenzangu usawa huu.
 
Lecture wetu mwaka wa kwanza pale UDSM alituambia Kama mshahara wako ni chini ya 4M bhasi tusinunue gari.

Na Kama mshahara wako ni 4M-7M bhasi gari yako ni IST

Kama unalipwa 7M+ atleast unaweza nunua gari yoyote I sio idk CC2500


Nilimuelewa sana Yule mzee maana hata yeye hakua na gari wakati ule[emoji28]

Cha kushangazi vijana wengi akiwa na 2M kila mwisho wa mwezi tayari kashakopa kununua crown mwisho wake ndio huu kuona bei ya mafuta ni kubwa.

Siwasemi vibaya ila ukizigatia hiyo formulae hapo juu mafuta hayotokuja kua changamoto kwako.
 
Ushauri mzuri but hairuleout unuhimu wa gari. Gari ni muhimu sana hasa ukiwa na familia. Inadaidia kwemye mizunguko ya kifamilia na hata emmergence mbalimbali. Mimi nimepaki kitokana na kuona gharama zinakuwa kubwa sana, wakati naweza tumia cheap altenative.
 
Kwa sasa hali ya hewa ni mbaya sana, jua na joto ni kali sana. Ukitembea kwa mguu unapofika inabd uoge kwanza otherwise utanuka
 
Temeke - Ubungo ni buku 2 kwa bajaji.
Ubungo - Kimara ni buku 1 kwa bajaji.

Ukiifanya mara mbili ni buku 6. Gari wese pamoja na foleni si chini ya 20K kila siku 😂😂😂
 
Ubunifu mzuri, ukizubaa mshahara wako utaishia kwa mafuta na msosi.
 
Jamaa anataka kutufanya kama watu wote tunaishi, SANGAMWALUGESHA!! hatuijui dar, wakati ndio maisha yetu ya kila siku!!
 
Hoja yako haina mashiko, sasa umekimbilia mipasho!!
wateseka wasema mipasho 🐒

but worry out, suluhisho lake ni bidii zaidi katika kazi na kutengeneza mbadala wa kujipatia kipato zaidi na maisha yazidi kulainika zaidi...

Inawezekana 🐒
 
Kama una workmates ambao mnakaa the same location mgechangia mafuta .

Ila Kama hawapo tumia usafiri wa umma ili usije kushindwa kulipa Ada za watoto
Ila haya maisha bwana, yaani mtu unajinyima huishi maisha yako kisa majukumu kama watoto.

Sijui tutaishi lini?
 
wanao kaa mbagala, gongo la mboto na chanika wanafanya kazi posta na masaki japo wanalipa nauli lakini garama ya hiyo nauli kwa siku ni sawa na wanao miliki magari tu....nauli kwa mwezi laki4 mshahara laki7
Weka vizuri hesabu zako. Gharama ya nauli kutoka Gongo la Mboto hadi Posta, inalinganaje na gharama ya kuweka mafuta gari la kukutoa Gongo la Mboto hadi Posta? Tufanye hutaki adha za daladala; Ukiwa pale Mnazi mmoja kuna usafiri wa kutosha wa watu binafsi (gari ndogo, bajaj au pikipiki) kuelekea Gongo la Mboto na nauli yake ni kati ya sh. 2000/= na 3000/=. Tuchukue maximum sh. 3,000/=,. Je, sh. 6,000/= kwenda na kurudi zitaweza kukidhi mahitaji ya mafuta katika gari yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…