Nimeamua 'kusilimu' je, kisheria na kiimani nitaruhusiwa kuongeza wake nikihitaji?

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2017
Posts
6,097
Reaction score
7,199
Chukulia katika mazingira ambayo ninauhuru (wa kikatiba) kuchagua dini yyte ile ninayoitaka. Na uhuru huu ninayo haki ya kuutekeleza wakati wowote ule. Sifungwi kubaki kwenye dini fulani.

Katika mazingira ya kuwa nimeoa mke kwa ndoa ya kikristo ambayo inaruhusu mke mmoja tu kwa mume mmoja na inatambulika hivyo kisheria. Nikiwa kwenye ndoa hiyo, kesho nikaamua kubadili dini na kuwa muislam na huko ninaruhusiwa kuwa na wake hadi wanne.

MASWALI:
1. Kwakua nitakua nimekana dini yangu ya awali, Je sheria itaendelea kumtambua huyu mke wa ndoa ya kikristo?

2. Hata kama tumeamua kuishi pamoja kama wanandoa (yeye abaki kuwa mkristo), je nitakua na uhuru kisheria kuongeza wake?

3. Hata kama tumeamua kuishi pamoja (na mke wangu naye abadili dini na kuwa muislam), je tutakuwa tumefunga ndoa au tutahitaji kuoana upya?

Nielewesheni kisheria na kwa imani ya kiislam pia.
 
Namba 3 ndio chanzo cha majibu ya maswali yako yote..
Ukibadili dini kisheria ya dini mnapaswa kufunga ndoa upya otherwise mtaendelea kuzini tu..

2. Unaruhusiwa kuoa lakin utambue huyo ndio atakuwa mkeo halali yule mwingine mnazini tu, yampasa abadili dini mfunge ndoa ya kiislamu

1. Sheria ipi unaizungumzia, kiserikali atatambulika kama mkeo ila ndani ya dini ya kiislam huyo si mkeo.. yawapasa mfunge ndoa halali.
 
Hapo namba 1: sheria itawatambua hawa walioongezeka kama wake halali?
 
Majibu!
1.Sheria ya kiislam itamtambua mkeo ikiwa na yeye amesilimu(amekuwa muislam)
2.Kama yeye akibaki kuwa mkristo ww utakuwa unazini (utapata dhambi) kwa mujibu wa sheria za kiislam kwa kuwa uislam haukubali ndoa ya muislam na asiye muislam(lazima mke &mume wawe wote waislam)
3.Wote mukibadili dini (mukiwa waislam)hamtatakiwa kufunga ndoa mpya ila ndoa yenu ile ile muliofunga mkiwa wakristo inatosha,Ispokuwa kama wakati mulipokuwa wakristo hamkufunga ndoa basi hapo ndio itawalazimu kufunga ndoa.
 
Namba 3 ndio chanzo cha majibu ya maswali yako yote..
Ukibadili dini kisheria ya dini mnapaswa kufunga ndoa upya otherwise mtaendelea kuzini tu..

2. Unaruhusiwa kuoa lakin utambue huyo ndio atakuwa mkeo halali yule mwingine mnazini tu, yampasa abadili dini mfunge ndoa ya kiislamu

1. Sheria ipi unaizungumzia, kiserikali atatambulika kama mkeo ila ndani ya dini ya kiislam huyo si mkeo.. yawapasa mfunge ndoa halali.
Ucjibu kitu usokijua huyo mke wake ataendelea kua mke wake hata kama akiwa katika dini yake na akisilimu nae mwanamke ndoa itaendelea kubaki ile ile ya kwanza na mwanamke atakae oa wa pili pia ni mkewe halali
 
Chukulia katika mazingira ambayo ninauhuru (wa kikatiba) kuchagua dini yyte ile ninayoitaka. Na uhuru huu ninayo haki ya kuutekeleza wakati wowote ule. Sifungwi kubaki kwenye dini fulani.

Katika mazingira ya kuwa nimeoa mke kwa ndoa ya kikristo ambayo inaruhusu mke mmoja tu kwa mume mmoja na inatambulika hivyo kisheria. Nikiwa kwenye ndoa hiyo, kesho nikaamua kubadili dini na kuwa muislam na huko ninaruhusiwa kuwa na wake hadi wanne.

MASWALI:
1. Kwakua nitakua nimekana dini yangu ya awali, Je sheria itaendelea kumtambua huyu mke wa ndoa ya kikristo?

2. Hata kama tumeamua kuishi pamoja kama wanandoa (yeye abaki kuwa mkristo), je nitakua na uhuru kisheria kuongeza wake?

3. Hata kama tumeamua kuishi pamoja (na mke wangu naye abadili dini na kuwa muislam), je tutakuwa tumefunga ndoa au tutahitaji kuoana upya?

Nielewesheni kisheria na kwa imani ya kiislam pia.
1.sheria ya kiislam itatambua ndoa yenu ikiwa na yeye mkeo atabadili dini na kuwa muislam.
2.
Ila angekuwa alishakufuata mpoo iman moja ungemtaka ridhaa yake ya kuongeza MKE na akikukatLia hauruhcw kuoa
Samahani unazungumzia dini gani mkuu?
Ktk uislam mume akitaka kuongeza mke mwingine ataoa hata kama mke wake wa kwanza hajaridhika na ndoa itakuwa sahihi kwa mujibu wa uislam
Pia ifahamike kuwa mke haombwi ridhaa bali anapewa taarifa na c vinginevyo!

Labda ikitokea mume walikubaliana(ilikuwa ni sehemu ya sharti la kuoana) na mke wake kabla ya kufunga ndoa kuwa yeye mume hataoa mke wa pili mpaka yy mke aridhie hapo ndio mume atawajibika kutaka ridhaa ikiwa makubaliano yao yalionesha wanaweza kuacha kama ataoa mwingine.
 
Kwa sheria za Tanzania mke wako anabaki kuwa mke wako hata kama ungebadili dini kwenda dini ya kishetani kama mlifunga ndoa na mkapewa kile cheti cha ndoa chenye nembo ya bibi na bwana ambacho ndicho cheti inayotambulika kisheria. kama ilifungwa kanisani nanabaki kuwa mke wako vile vile maana ndoa za kaninsani hadi kifo kiwatenganishe.

Wewe kama unabadili dini kwa sababu ya kutaka kuongeza mke hiyo dini kiimani pia haina msaada kwa maisha yako ya rohoni maana huendi huko kwa ajili ya kuimwabudu Mungu wako bali kuhalalisha tamaa yako ya kimwili.
 
Back
Top Bottom