Nimeamua liwalo na liwe!

Nimeamua liwalo na liwe!

Gharama ya kujenga aina hii ya ghorofa hata kama ni chumba kimoja, inaweza kuwa sawa na kujenga vyumba vitatu, sebule, dinning na store ardhini.

Sio kweli mkuu zingatia vipimo ni mita 5 kwa 5
 
Nakushauri kama bajeti imebana tumia mfumo huu, na katikati ya hizo ghorofa usimimine slab, tumia mbao au zile bati ngumu na chuma.

Mkuu hii Hapana hapo ukitema mate chini huwezi kusikia hata kamlio chake,nataka niwe juu kidogo
 
Samahani mkuu, nilikutania tu , hata vipimo sijui. Ni hili neno ghorofa limeniogopesha bila kuchanganua mambo.
 
Bora uvumilie upambane utafute Hela ujenge ghorofa la maana kuliko kua na haraka kujenga vitu vya ajabu

Unataka nijenge ghorofa kubwa ili iweje mkuu!?, mimi nachotaka ni ghorofa ya chumba kimoja tu [emoji276]
 
Hebu fanya hivi, andaa pesa ya vitu vifuatavyo:
Mchanga Mendes 1
Kokoto Mende 1
Mawe fuso 1
Chuma:
12mm PC 8
10mm PC 30
8mm PC 10
Binding wire bandle 1
Cement mifuko 50
Tank la maji(Lita 2000) itafaa zaidi
Tofali sijui (maana sijui utatumia aina ipi kulingana na ulipo.
Kwa ufupi ukiwa na 10M itakusogeza sana.
 
Unataka kujenga wewe au mimi mkuu?,yaani pesa yangu unipangie matumizi [emoji28]ndio ile ukiagiza chai [emoji477]️ lazima uletewe na chapati mbili [emoji276]nayetaka kujenga ni mimi chumba juu sebule chini kama inavyoonekana kwenye picha
Nimecheka hatariii asbh nilkkuelewa tofauti ila sasa hv nimekusoma
 
Hebu fanya hivi, andaa pesa ya vitu vifuatavyo:
Mchanga Mendes 1
Kokoto Mende 1
Mawe fuso 1
Chuma:
12mm PC 8
10mm PC 30
8mm PC 10
Binding wire bandle 1
Cement mifuko 50
Tank la maji(Lita 2000) itafaa zaidi
Tofali sijui (maana sijui utatumia aina ipi kulingana na ulipo.
Kwa ufupi ukiwa na 10M itakusogeza sana.

Shukrani sana kiongozi [emoji1376]matofali nataka kutumia haya haya ya block,kwa hiyo milioni 10 mkuu nitaweza kukamilisha boma?
 
Back
Top Bottom