Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi

Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi

Nimeipenda mkuu! Udhubutu umekusaidia!!
Watu wengi tunamawazo tu akilini lakini kudhubutu ni changamoto!!!
keep it up!
 
Thumb up! Sasa huo ndio USOMI! Sio kukariri "vitini" na kutandaza A kibao, Mkuu pambana. Mi nasaha zangu kwako, kaa mbali na zile timu 2 zinazobishana humu kama wanavosutana wale mashabiki wa wabana pua wawili, kaa mbali na "watoto" na pia kaa mbali na wana-hip hop!
 
Mkuu nikisoma hi I inanipa shauku ya kufany hili jambo langu la kujiajiri wKat nipo chuo thank you so much for inspiration [emoji119]
 
Nimeipenda mkuu! Udhubutu umekusaidia!!
Watu wengi tunamawazo tu akilini lakini kudhubutu ni changamoto!!!
keep it up!
Impressive keep it up
Hongera kwa kuthubutu mdau
Thumb up! Sasa huo ndio USOMI! Sio kukariri "vitini" na kutandaza A kibao, Mkuu pambana. Mi nasaha zangu kwako, kaa mbali na zile timu 2 zinazobishana humu kama wanavosutana wale mashabiki wa wabana pua wawili, kaa mbali na "watoto" na pia kaa mbali na wana-hip hop!
Yaani umenigusa sana ndugu. Hongera sana
Nimechukua no yako mkuu, nitakutafuta
Hongera sana, huko ndiko tunakoita ni KUJIONGEZA!
Mkuu nikisoma hi I inanipa shauku ya kufany hili jambo langu la kujiajiri wKat nipo chuo thank you so much for inspiration [emoji119]
Asanteni wakuu ngoja niendelee kupumbana.
 
Tatizo kubwa kwa sisi wanavyuo hatuwazi nje ya box,kila mtu akipata vilaki kadhaa(mwanachuo) anakimbilia kufungua banda la chipsi.OK fine malengo yako baada ya hilo banda?.

Ok Mimi ni mwanachuo wa mwaka wa pili,nimeamua kuja na ubunifu tofauti wa biashara yangu.Nimendunduliza nikafikisha laki sita na nusu na ninadream zakuja kuwa bakharesa hapo baadae.Unajua nimefanya nini?.

Nimetafuta vijana waaminifu wawili niliosoma nao wakafeli school.Mmoja yupo huko hom(mkoani) mwingine nimemtumia nauli elfu 50 aje dsm nikae nae geto(kashafika).

Nimechofanya yule wa mkoani(ninamuamini sana) nilimtumia laki nne na nusu,akanunua mchele kg 400.kilo kwa sasa mchele mpya ni 1000Tzsh.Kwahiyo apo ilienda sh laki nne.akabakiwa na sh elfu arobain,nmejumlisha na hela yakutoa mchele mashineni na magunia yakuuwekea.

Baada ya hapo akaenda tafuta usafiri ambao kila kg 100,wamemtoza sh elfu 10000.kwahiyo kg 400 akawa kamaliza ela mpaka mzigo kufika dar.

Sasa unajua nmeamua kuifanya vipi hii biashara.Mimi nauza kuanzia Kg 5. Kwa shilling 1800 kila kilo.Nmechukua oda ya mama ntilie wanao uza chakula chuo nacho somea,pia na baadhi ya mama ntilie wamtaani.

Pia nawauzia wanafunzi wanaojipikia kwenye magheto.Jambo la msingi nimelofanya nikuwa mtu akihitaji mchele ananipigia simu nampelekea mchele mpaka mahali anapokaa.
Kama itakuwa mbali sana ambapo nitahitaji usafiri basi itabidi kg1 mteja ainunue kwa sh 1900.

Mchele ninaouza quality yake kwenye maduka ya mitaani ni sh 2200.
Sasa nimeanza na hizi kg 400,ambazo nikiziuza kwa kg1, sh 1800. Nitatoa sh 720000.Na hii nategemea ndani ya siku 10, mpaka 12 nitakuwa nimeshaipata, kwahiyo awamu ijayo nitatuma kg zaidi ya 580 kama bei haitopanda

Tumekubaliana nahawa jamaa zangu wawili tutaanza kulipana japo hela ya sabuni baada ya miezi minne.Na huku nikiwa nimesubiri hela ya bum nitoe kama laki tatu niongezee ili mtaji ukue baada ya mauzo.

Pia nimekopa mizani nitakuwa nalipa kidogo kidogo kadiri mauzo yangu yatakavyokuwa.

Chakula ambacho nakula mie na huyu jamaa yangu kipo nje ya bajeti ya mtaji.

Na wewe mwanafunzi mahali ulipo/mtu mwenye mtaji mdogo waweza jaribu hii nahakika itakulipa.

Au kama mtu yeyote mwenye ushauri zaidi namna nitakavyoboresha zaidi anaweza kunisaidia(tusaidia).

Sitaki kazi.
.................
................

Update
...........
Nashukuru sana kwa member wanavyonipasapot, wapo wengine wanahitaji namba yangu ili waweze kuniunga mdogo wao japo kilo kadhaa napatikana kwa namba hii 0753980107 au 0679569625.

Popote pale ndani ya Dar nitakufikishia mchele utakaouhitaji. Kama ukipiga nisipopokea naweza kuwa nipo darasani piga namba hii 0718696135 kwa jamaa ninayesaidiana naye haka kabiashara.

Nitoe pia shukrani kwa member mmoja ingawa sifahamu anatumia jina gani humu JF lakini kaniunga Kg180.

Asanteni sana wadau.
Kuna MTU ana kg mia tano nikuunganishe naye? Kama mzigo umeisha?
 
Napata hofu kama kweli wewr ni mwana chuo maana haujaweza kutofautisha L na R
Sijaona kama ni tatizo kiasi hicho. Haya ni matatizo yatokanayo na matamshi ya lugha mama.waweza hata kuwa na degree saba lakini zoezi dogo la kutofautisha herufi hizo mbili laweza endelea.kwa mawazo yangu nadhani tujadili wazo la kibiashara alilonalo mjumbe hapa.
 
Watu wote waliodhubutu ndio matajiri wakubwa duniani; tafuta habari za coca cola ilivoanzishwa; hata Mungu anapenda watu wajasiri soma habari za Joshua katika biblia! Big up
 
Back
Top Bottom