Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi

Nimeamua nithubutu ingawa nina mtaji pungufu ya laki saba. Nawe waweza jaribu mahali unapoishi

Luhanyula Bigup sana mkuu, wewe ni role mode wa vijana wengi hasa wanachuo, hope unaweza kubalance muda wako vizuri na masomo. mtu anaweza kukopi idea yako ila hawezi kukopi spirit uliyonayo, endelea na hiyo bidii katika kazi, na hongera sana kwa kutokua mchoyo wa mawazo, umekua ukishare kila changamoto unazokutana nazo, huna kinyongo na mtu, uko real katika maisha. Believe me siku moja utakua mfanyabiashara mkubwa sana na haya maisha unayoyaishi leo yatabaki historia na funzo kwa vijana wengi. Ningekuwa naishi Dar hakika ningekua mteja wako ili kukuunga mkono.
 
Thank you brother,ubarikiwe sana kwa mchango wako huu murua mkuu.
You touch my heart brother, nimepitia ugumu kama wako japo mimi nilijikita kwenye ufugaji ila kwa sasa namshukuru mungu naona faida nzuri, na michango mingi niliipata kupitia JF jukwaa la uvuvi na ufugaji, kuna watu hawana roho za kwanini kumsaidia mtu.
 
Mwaka sasa umeisha namshukuru Mwenyezimungu hali si mbaya ingawa kuna changamoto za hapa na pale,lakini nimeweza fungua banda lingine.
Hongera sana...Mungu aendelee kukubariki....Vipi kwa sasa biashara ya mchele imefikia wapi
 
Hongera sana...Mungu aendelee kukubariki....Vipi kwa sasa biashara ya mchele imefikia wapi
Biashara inaenda vizuri kabisa watu wanaohitaji niwe nawaletea niwengi sana,na pia kwa sasa huwa naleta na mahindi pia.
 
Barikiwa sana mkuu, jitahidi urasimishe biashara yako ili iwe rahisi kujiendesha yenyewe hata kama haupo karibu au umebanana na kazi zingine, kumbuka ukiwa na kakampuni ka usambazaji katakusaidia kuvutia wateja wakubwa zaidi kama hoteli n.k
 
Safi mkuu namimi nilinunua mpunga nikaweka stoo walaki tano mwaka 2016 mwezi wa sita nikaja kuuza mwezi wa tatu nikapata million.so hata ya kuweka mpunga stoo baada ya mda unakoboa unauza mchele inalipa sana
 
Nunua vitu online kwa bei ndogo pokea posta pale then uza mara mbili yake hadi tatu. Easy tu but kuwa makini.
 
Safi mkuu namimi nilinunua mpunga nikaweka stoo walaki tano mwaka 2016 mwezi wa sita nikaja kuuza mwezi wa tatu nikapata million.so hata ya kuweka mpunga stoo baada ya mda unakoboa unauza mchele inalipa sana
Yea hiyo pia ni nzuri.
 
Barikiwa sana mkuu, jitahidi urasimishe biashara yako ili iwe rahisi kujiendesha yenyewe hata kama haupo karibu au umebanana na kazi zingine, kumbuka ukiwa na kakampuni ka usambazaji katakusaidia kuvutia wateja wakubwa zaidi kama hoteli n.k
Sawa mkuu ushauri wako ntaufanyia kazi.
 
Basi nunua bitcoins au nenda ka trade forex utapiga hela mingi. Soma kuhusu bitcoins na forex. Tafuta threads humu
 
Back
Top Bottom